Monday, December 30, 2013

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATOA TAHADHARI KWA WAUAJI WA TEMBO


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALIITAARIFA KWA UMMA
Itakumbukwa kuwa Serikali iliamua kuanzisha “Operesheni Tokomeza Ujangili” kufuatia kukithiri kwa vitendo vya ujangili katika maeneo yote yaliyotengwa kisheria kama Mapori ya Akiba; Hifadhi za Taifa na Hifadhi za Misitu katika miaka ya karibuni. Hata hivyo, Serikali iliamua kusitisha operesheni hiyo kwa muda.

Kufuatia kusitishwa kwa Operesheni Tokomeza, matukio ya uvunjaji wa sheria za hifadhi kama vile uingizaji holela wa mifugo katika maeneo ya hifadhi; ujangili wa tembo pamoja na uvunaji wa miti katika hifadhi za misitu yanaonekana kushamiri. Aidha, kumekuwa na ongezeko la kuvamiwa watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na hata kuwasababisha madhara yakiwemo vifo na majeraha. Baadhi ya matukio hayo ni pamoja na:
·        Majangili kuua takriban tembo 60 katika Hifadhi/Mapori ya Selous, Rungwa, Burigi na Katavi na Ngorongoro. Hawa ni takriban tembo wawili kwa siku. Ikumbukwe kuwa wakati wa kipindi chote cha operesheni kilichodumu kwa mwezi mmoja ni tembo wawili tu waliokuwa wameuawa.  
·        Watumishi wa Pori la Akiba Mkungunero (Kondoa) waliokuwa doria kuvamiwa na kundi la watu wapatao 80 waliokuwa na mikuki na silaha nyingine za jadi  tarehe  24 Desemba, 2013.
·        Kuuawa kwa Askari mmoja wa wanyamapori aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Magengere (40) na mwingine, Bwana Yahaya Ramadhani (34), kujeruhiwa vibaya na Wafugaji walioingiza mifugo ndani ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Jumuiya (WMA) Ukutu (au JUKUMU) iliyoko Morogoro vijijini tarehe 6 Decemba, 2013.
·        Mtumishi mmoja wa wanyamapori, Sajidi Majidi, kujeruhiwa kwa kuchomwa mkuki kichwani na kuvunjwa mkono na wafugaji walioingiza ng’ombe katika Eneo la Ramsar la Kilombero tarehe 14 Novemba, 2013.
·        Kukamatwa kwa gari lililokuwa na mizoga 20 ya swala wilayani Simanjiro siku za karibuni
·        Kuanzishwa kwa kambi ya majangili katika Pori la Akiba Burigi ambapo vitendo vya ujangili vinaendeshwa. Majangili waliokuwa na silaha za moto walikimbia na kuacha nyuma nyani 30 waliokuwa wamewaua baada ya kukurupushwa na askari wa wanyamapori.
·        Kuongezeka wimbi la uvamizi na ufugaji wa mifugo ndani ya mapori ya akiba na hifadhi za misitu iliyopo magharibi mwa nchi yetu, hasa Burigi-Biharamulo-Kimisi, malagarasi-Moyowosi, Rukwa Lukwati, Luwanda, Ugalla, Ibanda-Rumanyika, Minziro na Katavi.

Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuwakumbusha wananchi kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 pamoja na Sheria zinazosimamia maeneo ya Hifadhi za Taifa na Misitu kuwa hairuhusiwi wananchi kuingia katika maeneo haya bila kibali ikiwa ni pamoja na uingizaji wa mifugo kwa ajili malisho. Aidha, bado vitendo vya ujangili haviruhusiwi chini ya sheria hizi. Kifungu cha 15 ni marufuku mtu yeyote kuingia kwenye pori la akiba bila kibali.  Aidha, Sheria hiyo inakataza kuwa na silaha yoyote ndani ya Pori la Akiba bila kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori [kifungu cha 17]; kuwinda, kuua, kukamata au kujeruhi mnyama [Kifungu cha 19] na kuchunga ng’ombe ndani ya Pori la Akiba [Kifungu cha 21].
Ikumbukwe kuwa matukio yaliyotokea bungeni Dodoma, hayajatengua Sheria yoyote ya Wanyamapori au Misitu.  Hamna maamuzi yoyote ya Bunge yaliyohalalisha ukiukwaji wa Sheria za Uhifadhi. Hivyo, wananchi wanatakiwa kutii na kufuata Sheria hizo kama zilivyo. Tahadhari inatolewa kuwa Serikali haitasita kumchukulia hatua kali yeyote atakayekiuka Sheria ya Wanyamapori kwa makusudi. Tunawaomba wananchi wasikubali kudanganywa na mtu yeyote yule kuvunja Sheria za nchi.

Aidha, nachukua nafasi hii kuwaagiza watumishi wote wa Wizara ya Maliasili na Utalii wahakikishe kuwa wanaendelea kutekeleza majukumu yao ya ulinzi wa maeneo ya Hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba na Misitu ya Hifadhi bila kutetereka. Sanjari na hilo wasisite kuchukua hatua stahiki dhidi ya mhalifu yeyote mradi tu wanazingatia Sheria, Kanuni na taratibu.  Utekelezaji huu wa sheria ufanyike bila kuathiri haki za msingi za binadamu.

Serikali ina maadili na miiko inayotawala utendaji kazi wa watumishi wake wote wakiwemo wale wa maliasili. Wizara ya Maliasili itaendelea kuwakumbusha watumishi wake juu ya maadili na miiko hii kupitia mafunzo ya mara kwa mara na mbinu nyingine. Aidha, Wizara itaendelea kuboresha miongozo inayohusu maadili na miiko hii ili iweze kuendana na wakati.

Mwisho, Serikali inasisitiza kuwa, kwa kutumia vyombo vyake, itaendelea kutekeleza majukumu yake na kusimamia ipasavyo Sheria ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayeshiriki moja kwa moja au kusaidia vitendo vya ujangili ili kunusuru rasilimali za Taifa. Jukumu la uhifadhi wa maliasili zetu liko pale pale, ni letu na lazima litekelezwe kwa manufaa ya kizazi hiki na vizazi vijavyo.

Imetolewa na:

Mh. Lazaro Nyalandu, MB.
NAIBU WAZIRI, MALIASILI NA UTALII
Desemba 29, 2013.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MHE. LAZARO NYALANDU (KUSHOTO) AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI (HAWAPO PICHANI) ALIPOKUWA AKIZUNGUMZIA MSIMAMO WA SERIKALI JUU YA MATUKIO YA UJANGILI NCHINI. KULIA NI KAIMU MKURUGENZI WA IDARA YA WANYAMAPORI PROFESA JAPHARY KIDEGHESHO.


Tuesday, December 17, 2013

MWEKEZAJI MZAWA AANZISHA HIFADHI MPYA NCHINI, NI YA WANYAMA ADIMU KAMA FARU WEUPE

Bonde la Laroi litakalotumika kwa ajili ya uhifadhi wa Faru weupe na wanyama wengine adimu waliopotea nchini ambapo kampuni ya uwekezaji ya HUGO itawaingia kutoka nchi za nje ikiwemo Afrika Kusini na Botswana

waandishi wa habari wakimhoji mjumbe wa Serikali ya kijiji cha Laroi Kitesho Kaya kuhusu makubaliano iliyofikiana kati ya Serikali ya kijiji hicho na Kampuni ya Hugo Investment 

waandishi wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Serikali ya kijiji cha Laroi 

Mkurugenzi wa Tanzaniasasa semmy kiondo wa kwanza kulia, David Rwenyagira aliyevaa tisheti nyeupe na Claud Gwandu wa kwanza kushoto wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Serikali ya kijiji cha Laroi pembezoni mwa hifadhi ya bonde la Laroi

Mwandishi wa habari Mkongwe, Claud Gwandu (kushoto) akiandika jambo, wengine kutoka kulia kwenda kushoto ni Semmy Kiondo, Mjumbe wa serikali ya kijiji cha Laroi Kitesho Kaya na aliyevaa shati jeupe ni Seif Mangwangi 

moja ya madarasa yatakayohamishwa 

moja ya darasa shule ya msingi Olemedeye  litakalohamishwa katika eneo la hifadhi ya bonde Laroi ambapo kampuni ya uwekezaji ya Hugo imeahidi kujenga majengo mengine mapya 

Waandishi wa habari katika picha ya pamoja, kutoka kushoto ni David Rwenyagira, Claud Gwandu, John Mhala, Shaban Mdoe, Semmy Kiondo na Raymond Nyamwihula wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya bonde la laroi litakalotumika kwa ajili ya uhifadhi wa wanyama adimu ikiwemo Faru

Mwandishi wa habari wa Sahara Media, Raymond Nyamwihula akiruka juu kwa furaha baada ya kuona bonde la LAROI litakalotumika kwa ajili ya uhifadhi wa Faru weupe na wanyama wengine adimu nchini

waandishi wa habari waliofika katika bonde la Laroi katika kata ya Mateves wilaya ya Arumeru litakalotumika kwa ajili ya uhifadhi wa Faru Weupe na wanyama adimu kutoka kushoto ni Claud Gwandu, Seif Mangwangi, John Mhala, Shaban Mdoe, Semmy Kiondo na Raymond Nyamwihula

Waandishi wa habari waliojumuika katika ziara ya kutembele bonde la Laroi litakalotumika kwa hifadhi ya wanyama adimu ikiwemo Faru weupe wakipata mlo wa mchana 

Waandishi wa habari waliofanya ziara ya kutembelea eneo la hifadhi katika bonde la Laroi wakipata mlo wa mchana, kutoka kushoto ni Semmy Kiondo( mmoja wa wamiliki wa blogu hii), John Mhala, Claud Gwandu na Shaban Mdoe


WAANDISHI WA HABARI WAFANYA ZIARA KIWANDA CHA NGUO A TO Z

Mtendaji Mkuu wa A TO Z Anuj Shah akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotembelea kiwandani kwake 

baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika meza moja wakisubiri kupata chakula baada ya kumaliza ziara ya kutembelea kiwanda cha A TO Z

Msaidizi wa masuala ya utawala wa mtendaji mkuu wa kiwanda cha A TO Z Abeid George akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Texas nje kidogo ya jiji la Arusha mara baada ya waandishi hao kutembelea kiwanda cha A TO Z

Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu (kushoto), akitoa hotuba yake kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha katika hoteli ya Texas mara baada ya kumalizika kwa ziara ya kikazi kutembelea kiwanda cha A TO Z

Msaidizi wa mtendaji Mkuu wa kiwanda cha A TO Z George Abeid akifurahia jambo 

Wasaidizi wa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha A TO Z kuhusu masuala ya utawala wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa ziara ya waandishi wa habari kutembelea kiwanda hicho 


waandishi wa habari wakiwa kwenye gari kuelekea katika kiwanda cha A TO Z 

and
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja na mtendaji mkuu wa kiwanda cha A TO Z Katikati ndugu Anuj Shah aliyevaa miwani pembeni yake kushoto ni ndugu Binesh ambae pia ni Mmoja wa wakurugenzi wa kiwanda hicho 
waandishi wa habari wakiwa ndani ya Chandarua, kulia ni Angelo Mwoleka na anaefuatia katikati ni David Rwenyagira

waandishi wa habari wakitembelea kiwanda cha A TO Z wa kwanza kulia ni queen Lema, David Rwenyagira, Zulfa Mussa, Mack Nkwame na Kulwa Mayombi
NA SEIF MANGWANGI,ARUSHA

IMEELEZWA kuwa tatizo la ajira nchini litaisha endapo watanzania watabadilika na kupenda kununua bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya nchini ikiwemo nguo na kuacha kuvaa mitumba.

Hayo yameelezwa juzi na mkurugenzi mtendaji wa kiwanda  cha A to Z Anuj Shah alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wanachama wa chama cha waandishi wa habari Arusha waliotembelea kiwanda hicho.

Shah alisema Tanzania imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa ajira jambo ambalo limekuwa likichangiwa na watanzania wenyewe kwa kupenda kununua bidhaa za nje na hivyo kutoa ajira kwa watu wa nje.

"Ukinunua bidhaa za nje ya nchi maana yake unatoa ajira kwa watu wa nje na unakosesha watanzania wa ndani, hapa atoz tunazalisha bidhaa bora na imara na tunazisafirisha nje ya nchi na baadae mnaletewa mitumba, kama mkinunua bidhaa za ndani mtasaidia watanzania kupata ajira,"alisema Shah.

Alisema matarajio ya baadae ya kiwanda ni kuendelea kuongeza ajira zaidi kwa watanzania kutoka 8000 iliyonayo hivi sasa hadi kufikia 10,000 na kuisaidia serikali katika harakati zake zake za kutokomeza tatizo hilo.

Akizungumzia mafanikio ya kiwanda Shah alisema kiwanda hicho kinatarajia kupanuka na kuongeza wigo wa usambazaji wa bidhaa zake nje ya nchi mara baada ya viwanda vyake viwili kumalizika ujenzi wake ambapo bidhaa za zaidi ya dola bil79 zitakuwa zikiuzwa.

Hata hivyo alisema matarajio hayo yatafanikiwa endapo atapata msaada wa kutosha kutoka serikalini pamoja na watanzania kwa kuanza kununua bidhaa za ndani na kuacha kununua mitumba kutoka nje ya nchi.

"Ukiangalia nchi kama bangladesh wamekuwa wakiuza bidhaa zenye thamani ya zaidi ya dola bil70 kwa mwaka lakini ni sababu wanapata msaasa kutoka serikalini na watu binafsi, kwanini tanzania tushindwe?, tuna nguvu kazi kubwa lakini hatuitumii,"alisema.

Alisema msaada mkubwa anaotarajia kupata serikalini ni pamoja na kutathmini viwango vya bei za umeme viwandani na kuzishusha ili kuwapunguzia gharama za bidhaa wanazozalisha


Tuesday, November 26, 2013

biashara ya mafuta ya alizeti yashamiri stendi ya mabasi singida

Wafanyabiashara ndogondogo wa mafuta ya alizeti washamiri stendi ya mabasi singida. Hapa wakionekaba wakiuza mafita kwa abiria wa basi la igembe nsabo kama walivyonaswa na mpiga pivha wetu leo


Sunday, November 24, 2013

TMF YAKUTANISHA WAANDISHI WATEULE WA KUFANYA HABARI ZA UCHUNGUZI DODOMA HOTEL


Mhariri wa gazeti la jamboleo Ebenezer mende akizungumza na mmoja wa washiriki wa mafunzo ya waandishi wa habari za uchunguzi yanayotaiiwa kuanza hivi karibuni

Thursday, November 21, 2013

RC Arusha aagiza OCD kumtia mbaroni diwani kata ya olasiti

Mkuu wa mkoa wa arusha magesa mulongo akitoa agizo kwa mkuu wa wilaya akhakikishe diwani wa kata ya olasiti ismail katamboi anakamatwa kwa kuzuia mradi wa maji usipite ktk kata yake

Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya vest construction ltd samwel Lugemalila akimweleza mkuu wa mkoa maendeleo ya mradi huo wa maji wa km15 na changamoto ambazo amekuwa akikabiliana nazo

Fundi mkuu wa mradi wa maji paul tahiya kulia akieleza namna alivyopigwa na diwani katamboi na kupelekwa polisi, wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa kampuni inayojenga bomba hilo ya vest co.ltd samweli lugemalila

Sehemu ya mtaro unaotarajiwa kurandazwa mabomba kupeleka maji kijiji cha lukudivinyi kisongo wilayani arumeru

Tuesday, November 19, 2013

NYALANDU AJITOSA KUINUA VIPAJI VYA WANARIADHA SINGIDA, PIA NI KWAAJILI YA KUHAMASISHA KUPINGA UJANGILI

wanariadha wakiwa njiani kuelekea kumalizia mbio hizo 

Mkurugenzi wa Afrika Wildlife Fund, Pratik Patel akagana na mshindi wa kwanza katika mbio za nusu marathoni Paul Itambo baada ya kumkabidhi zawadi zake 

Mwanariadha, Fabiola William akimalizia mbio za Nusu Marathoni za Singida Marathoni na kuibuka mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake na kujinyakulia kitita cha Tsh300,000 na medali. mbio hizo ziliandaliwa na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu kwa lengo la kunyanyua vipaji vya vijana sanjari na kupambana na ujangili wa Tembo (PICHA NA SEIF MANGWANGI)


                                                                                                                                                             
Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo Paul Itambo akimaliza mbio za km21 
                                                                                                                                                                                                                          
Mmoja wa washiriki wa mbio za Singida Nusu Marathoni Philemon Tengu akikimbia bila kuwa na vifaa maalum vya kukimbilia ikiwemo viatu jana katika mbio hizo zilizoanzia katika kijiji cha mitula darajani na kumalizikia katika viwanja vya shule ya msingi Ntunduu. Mbio hizo ziliandaliwa na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyaladu zikiwa na lengo la kukuza vipaji vya wanariadha vijana na kupambana na ujangili wa tembo. (PICHA NA SEIF MANGWANGI)    NA SEIF MANGWANGI, SINGIDA
 
ZAIDI ya wakimbiaji 400 kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Singida juzi walishiriki mbio za kwanza za nusu marathoni Mkoani humo zikiwa na lengo kuu l

a kunyanyua vipaji vya wakimbiaji vijana sanjari na kuhamasisha vijana kwenye mapambano dhidi ya ujangili wa tembo nchini.
 
Katika mbio hizo zilizoandaliwa na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kwa upande wa wanaume,  mkimbiaji, Paul Itambo aliibuka kidedea kwa kukimbia kwa saa 1:10 na kuzawadiwa fedha Taslimu Tsh300,000, huku kwa upande wa wanawake Fabiola William aliishinda kwa kutumia saa1:53 na kuzawadiwa Tsh300,000.
 
Mbio hizo zilizoanzia katika kijiji cha Mitula Darajani na kuishia katika shule ya msingi Ntunduu, Singida Vijijini, Samuel Ikungi aliibuka mshindi wa tatu katika mashindano hayo na Emmanuel Samson alishinda nafasi ya tatu huku kwa upande wa wanawake, Winfrida Hassan aliibuka kidedea katika  nafasi ya pili na Zakhia Abdallah alishika nafasi ya tatu.
 
Kwa upande wa wanaume, mbio za kilometa tano Gabriel Galado aliibuka mshindi,  akifuatiwa na Deo Lazaro nafasi ya pili na Jonas John aliibuka nafasi ya tatu huku kwa wanawake Neema Kisunda aliibuka mshindi katika mbio hizo za kilometa tano akifuatiwa na Pascalia Sylvester.
 
Katika mbio za kilometa mbili na nusu upande wa wanawake, Julitha Anthony aliibuka mshindi akifuatiwa na Editha Gabriel na Margret Benado, huku upande wa wanaume Petro Pascal aliibuka mshindi akifuatiwa na Baraka Sebastian nafasi ya pili na Haji Swalehe alishika nafasi ya tatu.
 
Akizungumza kwa Niabu ya Naibu Waziri, Nyalandu, Mkurugenzi wa shirika la Afrika Wildlife Trust(AWT), ambae ni mwanzilishi wa matembezi ya kupinga ujangili wa tembo nchini katika matembezi aliyoyafanya kutoka Arusha hadi Dar es salaam, Pratic Patel aliwataka wazazi kuhamasisha vijana kushiriki kwenye mchezo wa riadha ili kuitagnaza Tanzania.
 
Pratik alisema Mkoa wa Singida umekuwa kinara wa mbio mbalimbli nchini hivyo ni wakati wa wazazi na wadau mbalimbali kuwekeza katika mchezo huo mkoani humo ili waweze kushiriki michuano mikubwa duniani na kuitangaza Tanzania kwa kuleta ushindi katika mbio watakazo shiriki.
 
“Riadha ni mchezo ambao utawapatia ajira vijana wengi hasa hapa Singida, ni wakati sasa kwa wazazi na wafadhili wengine kote nchini kujitokeza kudhamini riadha ili vijana watakaopatikana waweze kushiriki michuano mikubwa ulaya na kuiletea sifa Tanzania,”alisema.
 
Pratik alisema Tanzania imekuwa katika tishio la kupotea kwa wanyamapori maarufu ikiwemo Tembo hivyo vijana wanapaswa kuwa mabalozi wazuri wa kupingana na ujangili huo kwa kuwataja watu wanaohusika ili vyombo vya sheria viweze kuwachukulia hatua za kisheria.
Ends…

Monday, November 18, 2013

WABUNGE EALA WAMPONGEZA RAIS KIKWETE KUHUSU JUMUIYA HIYO

Waandishi wa habari wakiwasikiliza wabunge wa bunge la afrika mashariki walipokuwa wakimpongeza rais kikwete kwa msimamo alioonyesha kuhusu jumuiya hiyo

Kushoto katibu wa wabunge wa Eala shyrose bhanji kushoto na mbunge mwenzake adam kimbisa wakizungumza na waandishi wa habari

MAHAKAMA ZA KIMATAIFA ZATAKIWA KUSHITAKI WAHALIFU MAHAKAMA YA AFRIKA

Na seif mangwangi, AICC, ARUSHA

MAHAKAMA za mataifa mbalimbali barani afrika  zimeshauriwa  kushirikiana na mahakama ya haki za binadamu barani afrika (AFCHPR)  yenye makao yake jijini Arusha,  kutafisiri na kuelewa ulinzi wa   haki za binadamu ambazo zimekuwa zikikiukwa katika mataifa mbalimbali.. 

Rai hiyo imetolewa leo na waziri mkuu, mizengo Pinda,,alipokuwa akifungua kongamano la kwanzala majaji  linalojadili kuwepo msingi imara wa kuteteanakulinda  la  haki za binadamu kutokana na ukiukwajiunaofanywa katika mataifa mbalimbali. 

Amesema kuwa kongamano hilolinaloshirikisha majaji ambao ni wakuu wa vyombo vya kutoa haki ndani ya nchi, mahakamaza kikanda ,mahakama ya afrika  na nje kuangaliajinsi wanavyoweza kushirikiana pamoja katika kuangalia swala zima la ulinzi nautetezi wa haki za binadamu.

 Pinda, amesema kuwa Tanzania iko msitari wa mbelekutekeleza na kulinda haki za binadamu na imeridhia mikata mbalimbali naitifaki(Protocal) mbalimbali ili kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa .

Amesema kuwa eneo ambalo halijapea  nafasi kubwa  ni wakati gain kunakuwepo na ukiukwaji  wa haki za binadamu ,mashirika au mtu mmoja mmoja  anaenda mahakamani kudai haki hizo  pindi zinapokiukwa.

Pinda amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 7 zilizoridhia kulindwa kwa haki za binadamu kati ya 26 barani afrika zilizosainimkataba wa kuanzishwa kwa mahakama ya afrika ambayo imetoa uhuru kwa mshirika yasiyokuwa ya kiserikali  kwenda mahakamani kudai  haki pale zinapokwa . 

Kwa upande wake Jaji mkuu Mohamed Othman  Chande, amesema kuwa kongamano hilo ni la kwanza  tangia kuanzishwa kwa mahakama ya afrika.

alisema katika kongamano hilo majaji mbalimbali majaji wamekutanishwa ikiwemo wa mahakama za kikanda na mahakama ya afrika na za kimataifa  na kwamba msingi mkubwa ukiwa ni kujadili namna ya majaji wanavyoweza kushirikiana  kutafisiri masharti ya haki za bindamu. 

Jaji, Chande amesema haki za binadamu zimekuwa zikilindwa katika katiba za mataifa mbalimbali  na kila mahakama ya nchi husika imekuwa ikizitafisiri  haki za binadamu kulingana na mazingira yake .

Amesema kuwa  kuna maamuzi ya kikanda kwa kila nchi , kimataifa ,ambapo kila mtu ana haki ya kuishi na haki hiyo ipo katika mikataba ambayo imeridhiwa na nchi 26 barani afrika ambapo Tanzania katika kutekeleza hilo imekubali mtu yeyote, kikundi chochote kwenda mahakamani kudai haki za binadamu pindi zikikiukwa.

 Awali rais wa mahakama ya afrika, Sophia Akufo, amesema ni lazima haki za jamii na watoto zilindwe.

Akasisitiza  kuwa ni muhimu kuzingatiwa kwa haki za binadamu na katiba za mataifa mbalimbali na zilindwe ili kudumisha utawala bora na wa kidemokrasia unaozingatia  sheria 

Amesema kuwa kongamano hilo linatoa mwelekeo na mtizamo  wa siku zijazo wa kuboresha utawala wa sheria na demokrasia ,uchumi na siasa nzuri zinazolinda haki za binadamu kulingana na mikataba na maazimio na matamko mbalimbali ya kimataifa kuhusu haki za binadamu.

Friday, November 15, 2013

MASHINDANO YA ARUSHA GOLF OPEN CHINI YA UDHAMINI WA LODHIA GROUP OF COMPANY YAMALIZIKA

Mwenyekiti wa arusha golf mustafali kushoto akimkabidhi zawadi mwenyekiti arusha gymkhana dkt freezby baada ya kuibuka mmoja wa washindi kwenye mashindano ya arusha open

Mwenykiti wa kampuni za Lodhia Harun Lodhia katikati akiwa na Mwenyekiti wa Golf Arusha Mustafali kushoto katika michuano hyo iliyomalizika hivi karibuni Arusha 

Harun Lodhia akipiga mpira katika mashindano hayo 

Harun Lodhia akiingiza mpira kwenye shimo

Mwenyekiti wa kampuni za Lodhia, Harun Lodhia akipiga mpira wa Golf kuingiza ndani ya shimo katika mashindano hayo ambayo aliibuka mshindi wa nne 


Mwenyekiti wa Golf Arusha Mustafal akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo na kutaja washindiMwenyekiti wa kampuni za Lodhia duniani, na mdhamini wa mashindano ya Golf Open Arusha 2013, Harun Lodhia akizungumza kabla ya kumkabidhi mshindi wa kwanza zawadi yake katika mashindano hayo yaliyofanyika viwanja vya Gymkhan Arusha 

Mwenyekiti wa Kampuni za Lodhia duniani, Harun Lodhia akimkabidhi mshindi wa kwanza ambae pia ni mwenyekiti wa GOlf Arusha Mustafali Kikombe

Mwenyekiti wa Makampuni ya Lodhia Harun Lodhia akimkabidhi Mwenyekiti wa Golf Arusha Mustafal zawadi ya mshindi wa kwanza katika mashindano hayo 

Mwenyekiti wa GOLF Arusha Mustafal akifurahia zawadi ya seti ya televisheni aina ya Sumsung kwa kuibuka mshindi katika mashindano hayo

Jimmy akipokea zawadi kutoka kwa JATN

NA SEIF MANGWANGI, GHMKHANA ARUSHA

MASHINDANO ya wazi ya mchezo wa Gofu kanda ya Arusha (Arusha Open Golf), yamemalizika jana jijini hapa kwa mchezaji Muzaffar Yusufali kuibuka mshindi wa kwanza wa jumla kati ya wachezaji 78 waliojitokeza kwenye mashindano hayo yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Gykhana jijini hapa.

Katika mashindano hayo yaliyofanyika kwa siku mbili na kudhaminiwa na  kampuni ya Lodhia (Lodhia Group of Campanies), Muzaffar alizawadiwa seti ya luninga aina ya Sumsang nchi32, nafasi ya pili ilishikwa na Francis Julius na kuzawadiwa jiko la kupikia, na nafasi ya tatu ilishikwa na Piniel Uliwa na kuzawadiwa seti ya Radio.

Nafasi ya nne ilishikiliwa na Mwenyekiti wa makampuni ya Lodhia (Lodhia Group of Campanies), ambae pia ni mdhamini wa mashindano hayo, Haroun Lodhia na kukabidhiwa Microwave, lakini hata hivyo zawadi hiyo aliitoa kwa mshindi wa tano kutoka timu ya TPC, Frank Roman.

Kwa mujibu wa Rais wa Gold Tanzania, Paul Matinez, Jimmy Mollel aliibuka kidedea kwenye kundi la washindi waliocheza bila kutoa (Gross winner) aliyezawadiwa seti ya radio , akifuatiwa na Issack Wanyeche
aliyezawadiwa Microwave.

“Mshindi kundi la wanawake (Lady Winner), alikuwa ni Madina Iddi aliyepewa Dish, na mshindi kundi la vijana wadogo(Junior) aliibuka James Samweli wa timu ya TPC Moshi na kuzawadiwa Dish, huku kundi la
wachezaji wakongwe (Senior winner), aliibuka kidedea Harbar Janshadar ambae pia alizawadiwa Dish,”alisema Martinez.

 Akizungumzia mashindano hayo Matinez ambae pia ni diwani wa kata ya Moshono, alisema mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka yalikuwa yafanyike Aprili mwaka huu lakini kutokana na ukosefu wa udhamini yalishindwa kufanyika.

Alisema baada ya kuona hivyo, walimtafuta mdhamini kampuni ya Lodhia kwa kushirikiana na kampuni ya  kimataifa ya usanifu wa madini  ya Diamond International yenye ofisi zake jijini hapa kwa pamoja
walikubali kutoa ufadhili wao.

Kwa upande wake mdhamini wa mashindano hayo Mwenyekiti wa makampuni ya Lodhia, Haroun Lodhia alisema kampuni yake kwa kushirikiana na Diamond International imeamua kusaidia mchezo wa Golf nchini ili kusaidia na Serikali kuutangaza mchezo huo kimataifa.