Saturday, March 9, 2013

JK AHUDHURIA MKUTANO WA VYAMA VYA UKOMBOZI AFRIKA KUSINI

R ais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa Freeedom Park mjini Pretoria Afrika ya Kusini kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyioshiriki katika harakati za ukombozi Kusini Mwa Afrika.

Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini(Katikati) akiongea na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Viongozi wa vyama vilivyokuwa mstari mbele katika harakati za ukombozi Kusini wa Afrika leo mchana.Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa FreedomPark,Jijini Pretoria Afrika ya Kusini. Kushoto ni Rais Jakaya Kikwete mbaye pia ni Mwenyekiti wa CCM na kulia ni Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye ni kiongozi wa ZANU PF(picha na Freddy Maro)

Rais Dkt.Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini ambaye pia ni kiongozi wa ANC(Watatu kushoto),Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye pia ni kiongozi wa ZANU PF(Wapili kushoto) pamoja na Waziri Mkuu wa Namibia aliyeiwakilisha SWAPO, muda mfupi kabla ya kuanza mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Freedom Park,jijini Pretoria nchini Afrika ya Kusini kwa mwaliko wa chama tawala cha Afrika ya Kusini ANC

No comments: