Thursday, March 21, 2013

UTALII WA NDANI- WAANDISHI WA HABARI WAKIWA NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA MANYARA KATIKA ZIARA YA SIKU MOJA BAADA YA KUMALIZA SEMINA YA SIKU MOJA KUHUSU UANDISHI WA HABARI ZA UTALII NA UTAMBULISHO WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA UTALII TANZANIA

Waandishi wa habari waliohudhuria semina kuhusu uandishi wa habari za utalii na maliasili nchini wakiwa katika picha ya pamoja

Peter Saramba wa Mwananchi mbele kulia akiongozana na Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za utalii na maliasili Doto John kushoto

Waandishi wa habari wakiingia ukumbini, katika hoteli ya Twiga iliyopo mto wa mbu mara baada ya kupiga picha ya pamoja, wa kwanza kushoto ni mwandishi Cynthia Mwilolezi wa Nipashe na anayefuata ni Julius Magodi ambae ni katibu mkuu wa chama cha waandishi wa habari za utalii na maliasini nchini

Mkurugenzi wa miradi wa shirika la Frankfurt zoological society na aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa TANAPA, Gerald Bigurube akihojiwa na waandishi wa habari wa TV mbalimbali nchini katika mji wa Mto wa mbu mara tu baada ya kumaliza kutoa mada yake katika semina ya waandishi wa habari na utambulisho wa chama cha waandishi wa habari za utalii na maliasili nchini

Mkurugenzi wa blogu hii, mwandishi wa habari mkongwe nchini Seif Mangwangi akinawa miguu kwa maji ya moto yanayopatikana katika hifadhi ya Taifa ya Manyara, kwa mujibu wa mhifadhi wa hifadhi hiyo Julie Lyimo, maji hayo hutibu fangasi na ngozi, wa mbele aliyenyanyua kifua ni Daniel Sabuni wa gazeti la Mwananchi, aliyeshika kiuno, Ramadhan Siwayombe wa Tanzania Daima

No comments: