Friday, April 26, 2013

BREAKING NEWS: MBUNGE LEMA AKAMATWA USIKU WA MANANE, ALALA SERO

Taarifa zilizotufikia hivi punde, Mbunge wa jimbo  la Arusha mjini, Godbles Lema(CHADEMA), amekamatwa na makachero wa jeshi la Polisi usiku wa kuamkia leo na kulazwa sero. Mbunge huyo anatuhumiwa kuhamasisha vurugu katika chuo cha uhasibu IAA zilizopelekea Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo kupopolewa mawe na wanachuo alipokwenda kuwasihi waache vurugu wakati uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi mwenzao ukiendelea kufanywa na wapelelezi wa jeshi la Polisi
HABARI ZAIDI ENDELEA KUFUATILIA HAPA!!!!!!!!
Makachero wa jeshi la Polisi wakiwa wamewakamata wanachuo wawili katika vurugu hizo

Baadhi ya wanafunzi waliohisiwa kufanya vurugu chuoni IAA wakiwa chini ya ulinzi ndani ya gari la Polisi

Gari la Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema likivutwa kupelekwa polisi baada ya yeye kutuhumiwa kuchochea vurugu katika chuo cha uhasibu jijini hapa na baadae kutoroka kabla ya kukamatwa leo

Askari wa FFU wakiwa tayari kukabiliana na vurugu za wanafunzi wa chuo cha uhasibu njiro

Askari wa FFU wakiwa wamemweka chini ya ulinzi mmoja wa wanafunzi wa chuo cha uhasibu njiro ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akituhumiwa kushiriki kwenye vurugu hizo

No comments: