Tuesday, April 23, 2013

KLABU YA WAANDISHI WA HABARI ARUSHA WAPANGA KUFANYA UCHAGUZI MKUU JUNI MOSI MWAKA HUU


WAKIFUATILIA: waandishi wa habari wanachama wa APC wakifuatilia kwa makini mkutano wa dharura ulioitishwa na chama hicho, kushoto ni Daniel Sabuni, Cynthia Mwilolezi na Janeth Mushi
ARUSHA
NA MWANDISHI WETU TANZANIASASA

Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha(APC) kitafanya mkutano wake wa mwaka ambao utawachangua viongozi wapya kushika nyazifa mbalimbali za uongozi wa chama hicho.

Akizungumza mapema leo kwenye kikao cha dharula kilichokuwa na lengo ya kupanga siku ya uchaguzi ambayo imekubaliwa kuwa ni Juni Mosi,mwaka huu,Mwenyekiti wa APC,Claud Gwandu alisema ameita kikao hicho ili kuomba ridhaa ya wananchama kupanga tarehe ya mkutano mkuu na uchaguzi kutokana na kukabiliwa na maandalizi ya siku ya vyombo vya habari itakayofanyika katika ngazi ya Kanda kwenye jiji la Arusha na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 200.

Alisema kikatiba uchaguzi ulitakiwa kufanyika mwezi Mei lakini kutokana na kuwa APC ndio wenyeji wa  siku ya vyombo vya habari imeonekana ni busara kusogeza mbele siku ya mkutano mkuu ambayo itaenda sanjari na kufanyika uchaguzi wa kuwapata viongozi wa APC.

Kikao hicho kimewapitisha wajumbe watano watakaosimamia  uchaguzi huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na kila mwanachama kuamini ana uwezo wa kuongoza akishirikiana na wanachama wenzake.

Katibu wa APC,Eliya Mbonea alisema mchakato wa kuandaa fomu zitakazotumwa kwa wanachama utafanywa na kamati ya uchaguzi ambayo wajumbe wake ni waandishi wakongwe,Willam Lobulu,Danford Mpumilwa,Mch Amos Sekajingo,Zephania Ubwani na Kulwa Mayombi.

Baadhi ya wanachama waliozungumza na Blog hii hawakupenda kutaja nafasi watakazowania kuwa ni mapema mno kutangaza na ni moja ya mbinu za kisayansi kusaka ushindi.

Uongozi unaomaliza muda wake unajivunia mafanikio mbalimbali yaliyopatikana ikiwa ni pamoja na kuwa na ofisi ya kudumu,mafunzo ya mara kwa mara,vitendea kazi na baadhi ya wanachama kulipa ada kwa wakati.
MAJADILIANO: Mratibu wa APC, Seif Mangwangi wa pili kutoka kulia, Katibu wa APC Eliya Mbonea, mwanachama Richard Konga na Bertha Ismail wa kwanza kulia wakijadili jambo

Makamu Mwenyekiti wa APC, Charles Ngereza pamoja na Anthony Masai wakionyeshana jambo kwenye komputa

wanachama wakiendelea na kazi wakati mkutano ulipokuwa ukiendelea, aiyesimama nyuma ni Mustafa Leu, Veronica mheta na Cynthia Mwilolezi

Mwanachama wa APC, Veronica Mheta akiuliza swali katika mkutano huo

Katibu mkuu wa APC Eliya Mbonea akisoma agenda za mkutano huo, kulia kwake ni Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu

MAAKULI: waandishi wa habari wakipata chai katika mkutano huo, wa kwanza kushoto, MC Kassim Kiko, Edward Selasini, Abraham Gwandu, Magesa Magesa, Cynthia Mwilolezi na Richard Konga

Viongozi wa juu wa APC, Charles Ngereza kushoto, Claud Gwandu katikati (Mwenyekiti) na Eliya Mbonea (Katibu Mkuu) wakiteta jambo katika mkutano huo

Mwenyekiti wa APC akijibu hoja

Waandishi wa habari Cynthia Mwilolezi na Janeth Mushi katika picha ya pamoja

Mwandishi Mkongwe na mjumbe wa kamati ya utendaji David Frank akiperuzi gazeti la Mwananchi

No comments: