Thursday, April 25, 2013

MKEMIA MKUU WA SERIKALI ATOA SOMO KUHUSU DNA KWA MAAFISA UPELELEZI WA MIKOA YA ARUSHA, MANYARA, KILIMANJARO NA SINGIDA

Afisa upelelezi katika ofisi ya RCO jiji la Arusha, Tausi Abdallah akiwa amepokea cheti chake, nyuma ni afisa mwingine wa Polisi
Mkemia Mkuu wa Serikali Samwel Manyele akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo ya DNA Afisa Upelelezi wa jeshi la Polisi Arusha, Tausi Abdallah jana jijini hapa
Na Mwandishi Wetu, ARUSHA

UKOSEFU wa maabara ya wakala wa Mkemia mkuu wa Serikali mikoani
kumekuwa kukisababisha usumbufu kwa wadau wa huduma hiyo kusafirisha
sampuni hadi Jijini Dar es salaam, kungojea majibu kwa muda mrefu na
gharama kubwa ya kusafirisha sampuli hizo.

Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Afisa Tawala wa Mkoa wa Arusha
Eveline Mtamisa alipokuwa akifungua warsha ya siku mbili kwa wadau wa
huduma hiyo kutoka Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida.

Alisema kutokamilika kwa maabara ya mkemia mkuu jijini Arusha
itakayokuwa ikihuduma wadau wa kanda ya kaskazini kunapunguza ufanisi
na kupunguza matumaini ya wadau wa huduma hiyo kupata huduma kwa
wakati za zenye ubora wanaoutarajia.

“Naomba tatizo hili liundiwe mkakati ili maabara hii ianze kutumika na
kuondoa matatizo ya kusafirisha sampuni kwenda Dar es salaam,
kumbukeni mkoa wa Arusha una umuhimu wa pekee kitaifa na kimataifa,
ofisi nyingi za Kimataifa ziko hapa,”alisema.

Alisema Jumuiya za Kimataifa zilizopo jijini Arusha zinahitaji huduma
ya wakala wa Mkemia wa Serikali kwa ukaribu na kwa ufanisi ili Jumuiya
hizo ziridhike kuwepo kwa ufanisi wa hali ya juu wa huduma hiyo
nchini.

Mtamsa aliwataka wadau wa huduma hiyo kutoka vyombo vya usalama kuwa
waadilifu katika kutekeleza majukumu yao na kuondoa kero ya wao
kupokea rushwa ambayo imekuwa ikielekezwa kwao kila mara.

Kwa upande wake Mkemia Mkuu wa Serikali Samweli Manyele alisema ofisi
yake imejipanga kuhamasisha wadau mbalimbali nchuini kutumia huduma
hiyo ili kuboresha utekelezaji wa huduma zao bila shaka.

Washiriki wa mafunzo kuhusu vinasaba wakimsikiliza kwa makini Mkemia Mkuu wa Serikali Samweli Manyele alipokuwa akifunga mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza Aprili 23 hadi 24, Mwaka huu

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali jijini Arusha wakimhoji Mkemia Mkuu wa Serikali, kuhusu mkutano uliokuwa ukiendelea katika hoteli ya Naura spring jijini Arusha

Washiriki wakisikiliza kwa makini

Washiriki wakisiliza kwa makini hotuba ya mkemia mkuu Samweli Manyele

Washiriki wa mafunzo kuhusu shughuli mbalimbali ikiwemo namna ya uchukuaji wa sampuni za vinasaba DNA kutoka idara ya upelelezi ya jeshi la polisi jijini Arusha, katika picha ya pamoja.  wa pili kutoka kulia ni Rashida Nchimbi ( Mwandishi wa jeshi la Polisi jijini Arusha), na wanne kutoka kulia ni Tausi Abdallah anayefanya kazi ofisi ya RCO Mkoa wa Arusha 






No comments: