Monday, April 29, 2013

PADRI ADAIWA KUFUMANIWA NA MKE WA MTU, ANAJULIKANA KWA JINA LA MAMA P.....

Padri Urbanus akihamaki baada ya kuvamiwa ndani ya chumba chake ndani ya parokia na kupigwa picha akiwa anavunja amri ya saba na mke wa mtu

hapa Padri akiomba msamaha asidhuriwe  baada ya kufumaniwa akijifaidia mke wa mtu ndani ya Parokia

Baada ya picha kupigwa hapa wakaruhusiwa kuvaa nguo,  Mama P anaonekana akivaa sidiria aka kificha manyonyo, na Padri akivaa boxer yake

wakiwa hawaelewi cha kufanya


KANISA Katoliki Jimbo la Moshi limeingia katika kashfa nzito baada ya padri wake, Father Urbanus Ngowi wa moja ya parokia zake kudaiwa kufumaniwa na mwanamke anayesemekana ni mke wa mtu, Ijumaa Wikienda lina sakata zima.
Sakata la fumanizi hilo linadaiwa kutokea Jumatatu ya wiki iliyopita chumbani kwa padri huyo, Marangu Wilaya ya Moshi Vijijini ambako Father Ngowi inasemekana alikutwa ‘laivu’ akiwa na mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.
Pamoja na kunaswa huko, vyanzo havijaeleza humo chumbani wawili hao walikuwa wakifanya nini!
Habari zinadai siku ya tukio, mwanamke huyo aliingia nyumbani kwa padri huyo ambapo baadhi ya ndugu wa mumewe walikuwa wakimfuatilia baada ya madai yaliyokuwepo kwamba ana ukaribu wenye maswali mengi na mtumishi huyo wa Mungu.
“Unajua siku nyingi ilivuma kwamba Mama P na Father Ngowi wana ukaribu wenye maswali mengi, mume wake alifuatilia na kubaini ni kweli lakini akashindwa kuutenganisha ukaribu wao,” kilidai chanzo.
Chanzo kikaendelea kudai kwamba baada ya kuona mkewe amejikita kwa mtumishi wa Mungu, mumewe (jina tunalo) alinyoosha mikono juu na kumwachia Mungu.
Chanzo: Sasa siku hiyo baada ya ndugu wa mume kumfuatilia mpaka anaingia kwa Father Ngowi, wakaona ni bora watafute mpigapicha ili kupata picha za tukio ambazo zitakuwa ushahidi siku za mbele.
“Walipompata wakazama ndani, sekeseke likaanzia hapo. Walimkuta mwanamke huyo na mtumishi wa Mungu wapo kitandani.”
AWEKWA KITIMOTO
Habari zinadai kwamba kufuatia tukio hilo, tayari Kanisa Katoliki limemweka kitimoto padri huyo ambaye alikuwa akihudumu katika Parokia ya Korongoni, Moshi Vijijini kabla ya kuhamishwa na kupelekwa Parokia ya Makomu, Marangu ambako inadaiwa ameshushwa cheo.
Inadaiwa kuwa baada ya tukio hilo, Father Ngowi alikana kukutwa na mke wa mtu chumbani kwake lakini alipobanwa sana na mabosi wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Moshi, alikiri na kudai ibilisi alimpitia na kuomba kanisa limsamehe na kutompa adhabu kali ambayo itamuathiri kisaikolojia.
Hili ni tukio kubwa na la aina yake kuwahi kulikumba Kanisa Katoliki nchini kwa padri wake kudaiwa kukutwa na mke wa mtu chumbani kwake!
SIKU ZA NYUMA
Kuna madai kwamba mwaka jana (2012), Father Ngowi, mbele ya waumini wake alisoma barua yenye kukana shutuma zote zilizoelekezwa kwake kwamba amekuwa na ukaribu wenye maswali mengi na wake za watu.
Taarifa zilidai kuwa padri huyo aliweka wazi akisema si kweli kwamba amekuwa na ukaribu unaotajwa, akawataka waumini wake wapuuze tuhuma hizo alizosema zina mwelekeo wa kuchafua sifa yake na taswira ya Kanisa Katoliki kwa jumla.
Hayo ni madai ya vyanzo vyetu ambavyo viliambatanisha na picha mbalimbali za tukio hilo lenye kushtua waumini sambamba na namba za simu za padri huyo kwa ajili ya mawasiliano ili kujiridhisha.
IJUMAA WIKIENDA NA FATHER NGOWI SASA
Baada ya kujazwa madai hayo, kama ilivyo desturi ya Magazeti ya Global Publishers likiwemo hili (Ijumaa Wikienda), lilimsaka Father Ngowi kwa udi na uvumba ambapo Ijumaa iliyopita nyakati za mchana lilifanikiwa kuzungumza naye lakini kabla ya kufanya hivyo, kifaa cha kunasia sauti kiliwekwa sawa na mambo yalikuwa hivi:
Wikienda: Haloo, naongea na Father Ngowi wa Parokia ya Korongoni, Marangu, Moshi?
Father Ngowi: Naam ni mimi, nani mwenzangu?
Wikienda: Naitwa…(mhariri anataja jina), napiga simu kutoka Magazeti ya Global Publishers.
Father Ngowi: Uko wapi?
Wikienda: Makao Makuu ya Global Publishers, Dar es Salaam.
Father Ngowi: Eeh…unasemaje?
Wikienda: Kuna madai ya wewe kukutwa na mke wa mtu chumbani. Je, unaweza kunielezea kama ni kweli na tukio lilikuwaje?
Father Ngowi: Siyo mimi.
Wikienda: Wewe siyo Father Urbanus Ngowi?
Father Ngowi: Nimekwambia siyo mimi, hao ni matapeli wanataka pesa ndiyo wametengeneza hizo picha.
Wikienda: Kwa hiyo unataka kuniambia hizi picha ni za kutengeneza?
Father Ngowi: Nimekwambia hao ni matapeli wanataka pesa.
Wikienda: Ulishaziona picha zenyewe?
Father Ngowi: Sijui.
NGOMA YATUPWA KWA MKUU WA JIMBO
Wikienda: Mbona tayari tukio hilo linadaiwa limeshafika kwenye ngazi ya jimbo, Moshi kwa Father Paul Uria?
Father Ngowi: Muulize yeye ndiye mkubwa wangu.
Wikienda: Basi nisaidie namba yake ya simu ya mkononi.
Baada ya takribani dakika 10, Father Ngowi alituma namba ya simu ya Father Uria na mambo yakawa hivi:
Wikienda (huku kinasa sauti kikiendelea kufanya kazi): Haloo…naitwa …(mhariri anajitambulisha) kutoka Magazeti ya Global Publishers, Dar es Salaam, naongea na Mkuu wa Jimbo Kanisa Katoliki, Moshi, Father Uria?
Father Uria (kwa sauti yenye unyenyekevu): Ndiyo.
Wikienda: Una taarifa za mtumishi wako, Father Ngowi kunaswa na mke wa mtu chumbani?
Father Uria: Kwanza mimi si mkuu wa jimbo, ni mwakilishi wa mkuu wa jimbo. Sipo mjini kwa sasa nipo Kilema huku vijijini kwenye huduma lakini nilikuta ‘missed calls’ zake jana (Alhamisi) kwani ilikuwa tukutane kwa sababu alishanijulisha kuwa kuna tukio kama hilo unaloniambia wewe.
NGOMA YAWA NZITO, YATUPWA LEO JUMATATU
“Kweli tulikuwa tukae jana lakini ikashindikana, leo (Ijumaa) ni sikukuu (Muungano), kesho (Jumamosi) na keshokutwa (Jumapili) ni wikiendi. Kwa hiyo tutakaa Jumatatu (leo) hivyo nipigie saa 10:00 jioni siku hiyo ili nikupe maagizo tutakayofikia na mengine.
Wikienda: Lakini Father Ngowi alikueleza tukio lilikuwaje?
Father Uria: Nimekwambia tukikaa ndiyo tutajua kilichotokea. Wewe nipigie hiyo saa 10 nikupe kitakachojiri.
Wikienda: Shukrani Father Uria kwa ushirikiano.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS

1 comment:

HOT WATER BLOGSPOT.COM said...

heee kumbe maparoko wanayajua hayo mambo..nimecheki Fr anaonekana hana hata mpira...anakamua kavukavu,daaa!! lakini msiwalaumu hawa ni watu na taasisi yao ya mishahara si huyo tu wapo kiao wazinzi na wazinifu