Tuesday, April 23, 2013

RC ARUSHA AZINDUA ZOEZI LA CHANJO

Viongozi mbalimbali wa Halmashauri wakisalimia
ARUSHA
NA MWANDISHI WETU TANZANIASASA

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo amewataka wazazi kutumia wiki ya chanjo kuwapeleka watoto kupewa matone dhidi ya magonjwa mbalimbali ukiwemp wa Polio.
 
Ametoa kauli hiyo leo wakati wa uzinduzi wa chanjo watoto walio chini ya umri wa miaka mitano mkoa wa Arusha katika Kijiji cha Mbuyuni Kata ya Oljoro,wilayani Arumeru
 
Amewataka viongozi wa vijiji kuweka sheria ndigondogo zitakazowabana wananchi ambao watakaidi kuwapeleka watoto kupata chanjo hiyo muhimu inayogharimiwa na serikali kwa wananchi wake.
Mulongo amesema kutokana na chanjo hizo kutolewa baadhi ya magonjwa yametoweka kabisa na zilizokuwa Wodi za magonjwa hayo katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru zinatumika kwa mambo mengine.
 
Awali Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha,Frida Mokiti alisema mwitikio wa chanjo kwa mkoa wa Arusha unaridhisha kutokana na takwimu za mwaka jana kuwa miongoni mwa mikoa minne iliyofanya vizuri kitaifa huku wilaya ya Ngorongoro ikivuka asilimia 100.
 
Amesema utoaji wa chanjo hizo ni mkakati wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuhakikisha nchi inafikia lengo namba nnela millennia la kupunguza vifo vya watoto kwa theluthi mbili sanjari na kuzitaka halmashauri zote kufanikisha zoezi hilo kwa kiwango cha asilimia 95 kwa kila chanjo.

Kauli mbiu ya wiki ya chanjo kwa mwaka huu ni "Okoa Maisha.Kinga Ulemavu.Toa Chanjo
RC Magesa Mulongo akihutubia watu waliofika kwenye uzinduzi wa chanjo hiyo

Kina Mama wakisubiri watoto wao kupewa chanjo

Mganga Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Arusha,Thobias Mkina akisalimia wananchi,Mkuu wa Mkoa(kushoto) na Diwani wa Kata ya Oljoro,Sanare Miparali

RC Mages Mulongo akihutubia wananchi waliohudhuria ufunguzi wa chanjo

RC Magesa Mulongo akitoa chanjo

Mkuu wa Mkoa Magesa Mulongo akifanya zoezi la kutoa chanjo kwa mmoja wa watoto waliohudhuria ufunguzi wa chanjo hiyo jijini Arusha

Mkuu wa mkoa akitembelea mabanda ya maonesho na kupata maelezo


Mtaalamu akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa

Viongozi mbalimbali kutoka kushoto ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha,Dk.Frida Mokiti,Katibu Tawala wa mkoa,Mama Itanisa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Nyirembe Munasa

Oljoro safiiiii

Chanjo oyeeeeee

Oljoro safiiiiiiii?

Mtaalamu akimweleza Mkuu wa mkoa jambo kuhusu mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria kwa kutumia Vyandarua(katikati)Mganga Mkuu wa wilaya ya Arusha,Thobias Mkina

Akina mama wakiwa na watoto wao wakielekea kupata chanjo

Akina mama wakiondoka kwa furaha baada ya watoto wao kupata chanjo ya Polio

Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha akizungumza kwenye uzinduzi wa chanjo ya Polio

Mtaalamu akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa

No comments: