Friday, May 17, 2013

MWENYEKITI WA CHADEMA NA KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI, MBUNGE WA JIMBO LA HAI FREEMAN MBOWE AGAWA VIFAA VYA MICHEZO JIMBONI KWAKE

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe akimkabidhi nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya KIA Sports, Danstun Ngambile, zawadi ya jezi na mipira kwa ajili ya timu hiyo karibuni. Katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la chama hicho wilayani Hai, Dorice Cornel. Kiongozi huyo yuko katika ziara ya wiki mbili jimboni kwake kuzungumza na wananchi wa jimbo hilo.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe akiwakabidhi viongozi wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Mtakuja FC ya Mtakuja, Yusuf Idd (kushoto) na Rasud Juma (katikati) zawadi ya jezi na mipira kwa ajili ya timu hiyo hivi karibuni. Katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana, Dorice Cornel na Katibu Mwenezi wa chama hicho wilayani Hai, Simon Mnyampanda. Kiongozi huyo yuko katika ziara ya wiki mbili jimboni kwake kuzungumza na wananchi wake.

No comments: