Friday, May 3, 2013

PICHA MBALIMBALI MAADHIMISHO YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI YALIYOFANYIKA JIJINI ARUSHA, 3-4/MAY 2013

Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt Richard Sezibera akimkabidhi mjane wa marehemu Daudi Mwangosi aliyeuwawa huko Iringa na askari Polisi, hundi ya Tsh milioni 5 iliyotolewa na uongozi wa umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini UTPC ili aweze kuanzisha biashara yoyote atakayoipenda, kushoto ni mjane huyo Itika Mwakapeja, mbele mtoto wake Morie na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan

Mgeni Rasmi katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt.Richard Sezibera akiwa amembeba mtoto Morie ambae ni mtoto wa hayati Daudi Mwangosi aliyeuwawa kwa bomu na askari polisi mapema mwaka jana, kushoto ni mjane wa Daudi Mwangosi,  Itika Mwakapeja

Mrisho mpoto jukwaani

Mwanamuziki Mrisho Mpoto akighani mashairi yake katika wimbo maalum alioutunga kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari yaliyofanyika jijini Arusha kitaifa huku viongozi mbalimbali wakimsikiliza kwa makini

Wanamuziki wa bendi ya Mrisho Mpoto wakiimba kwa hisia na kutokwa machozi huku wakieleza matatizo ambayo waandishi wa habari wamekuwa wakikabiliana nayo nchini

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akiwatuza wanamuziki wa bendi ya Mrisho Mpoto

Mgeni Rasmi Dkt. Richard Sezibera akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari waandamizi pamoja na mabalozi waliowakilisha nchi zao katika maadhimisho hayo

No comments: