Tuesday, May 7, 2013

RAIA WANNE WA SAUDI ARABIA WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA MLIPUKO WA MABOMU ARUSHA.

 
 
mmoja wa majeruhi wa mabomu akiwa kalazwa katika hospitali ya mtakatifu Elizabeth jana akiendelea kupata matibabu
Polisi nchini Tanzania inawashikilia watu wa nane kwa madai ya kuhusika na mlipuko wa siku ya jumapili katika kanisa Katoliki la Olasit viungani mwa mji wa Arusha. Miongoni mwa washukiwa ambao wako mikononi mwa polisi ni raia wanne wa Saudi Arabia, na wengine wanne ni raia wa Tanzania.
 
Uchunguzi wa tanzaniasasa umebaini kuwa hadi jana idadi ya watu waliofari dunia kufuatia mlipuko huo ni wawili na wala sio watatu kama ilivyoripotiwa hapo awali. Polisi mjini Arusha vile vile wamethibitisha kuwa waliokufa wakati wa tukio hilo la kigaidi ni watu wawili.

Kwa wakati huu polisi wanachunguza ni kulipuzi aina gani kilitumika wakati wa shambulizi hilo.
 
Katika tukio hilo hakuna hasara yoyote iliyopatikana zaidi ya majeruhi walioumizwa katika mlipuko huo na vifo vya watu wawili..

Mlipuko huo uliotokea majira ya saa tano asubuhi katika kanisa katoliki la Olasiti nje kidogo ya mji wa Arusha nchini Tanzania na wengine kadhaa kujeruhiwa huku balozi wa papa na watawa waliokuwa katika shughuli hiyo maalumu ya uzinduzi wa parokia mpya ya mtakatifu Yosefu mfanyakazi wakinusurika pia.

No comments: