Thursday, May 16, 2013

TAKUKURU YASHINDWA KUWAPANDISHA KIZIMBANI WATUMISHI 10 WA MANISPAA YA ARUSHA KWA KUJIPATIA MAMILIONI YA FEDHA KUPITIA MISHAHARA HEWA


Aliyekuwa Afisa Elimu wa Manispaa ya Arusha (Sasa Jiji), Fatma Laizer akiingia katika viwanja vya mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha akisubiri kupandishwa mahakamani akituhumiwa kujipatia mamilioni ya fedha kupitia mishahara ya watumishi hewa pindi akiwa Afisa elimu.


Mmoja wa watumishi wa idara ya Afsa wakati ikiitwa Manispaa ya Arusha(sasa jiji), ambae jina lake halikupatikana akiingia kwenye viwanja vya mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha akisubiri kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kujipatia mamilioni ya fedha kupitia mishahara hewa ya watumishi. kushoto ni Afisa mwingine wa Manispaa hiyo 


Mmoja wa Maofisa wa Manispaa ya Arusha akiteremka kutoka kwenye gari la TAKUKURU kuelekea kwenye viwanja vya mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha akisubiri kusomewa mashitaka kuhusu kujipatia mamilioni ya fedha kupitia mishahara ya watumishi hewa. hata hivyo walishindwa kupandishwa kizimbani leo kufuatia hati iliyowasilishwa mahakamani hapo kuonekana kuwa na makosa ya kisheria

Ofisa wa takukuru akimsubiri mmoja wa watuhumiwa wa kujipatia mamilioni ya fedha kupitia mishahara ya watumishi hewa akiwa mtumishi katika manispaa ya Arusha baada ya kumfikisha mahakamani hapo


Mmoja wa watuhumiwa akiingia mahakamani hapo baada ya kuteremka kutoka kwenye gari la Takukuru


No comments: