Friday, June 28, 2013

ASKOFU MKUU INTERNATIONAL EVANGELISM AKEMEA WANASIASA WANAOPINGA SERIKALI ILIYOPO MADARAKANI



Askofu Issangya akihubiria

Na Mwandishi Wetu, Tanzaniasasablog

ASKOFU mkuu wa kanisa la International Evangelism Center (IEC), Sakila Eliud Issangya amewataka wanasiasa wanaopinga Serikali iliyoko madarakani kuacha mara moja kwa kuwa imechaguliwa kisheria.

Akihutubia maelfu ya waumini wa kanisa hilo jana katika maadhimisho ya
miaka 30 ya kuanzishwa kwa chuo cha Biblia chini ya kanisa hilo
Issangya alisema katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na vuguvugu
la vijana na wanasiasa kutoheshimu mamlaka iliyopo nchini.

Alisema kutii mamlaka iliyopo sio ombi ni suala la lazima kwa kuwa
imechaguliwa kihalali na wananchi hivyo endapo wapo wanaofikiri haifai
wasubiri muda ukifika watumie haki yao ya kupiga kura na kuchagua
viongozi wanaowataka wao.

“Biblia inasema tuheshimu mamlaka zetu, kutiii mamlaka iliyopo sio
ombi maana usipoheshimu na wewe hutoheshimiwa hivyo serikali iliyopo
ni lazima uiheshimu kwani ni sawa na Baba na Mama yako, ukitaka
kutawala huwezi kutawala Baba na Mama yako labda usubiri mpaka
wafe,”alisema Issangya.

Alisema kuwa vuguvugu la kutoheshimu mamlaka iliyopo madarakani
imekuwa ikichangiwa kwa sehemu kubwa na vijana ambao mawazo yao
yamekuwa na moto ambao unatakiwa kutulizwa na wazee kwa kuwafunza
masuala ya uongozi ili wawe viongozi bora.

Askofu Issangya akihubiria

Askofu Issangya akihubiria maelfu ya waumini wa kanisa hilo

Askofu Issangya akitambulisha watoto wake na hapa anamtambulisha Alaine mmoja wa watoto wake ambae anatarajia kufunga ndoa mapema mwezi ujao

Mke wa Askofu Issangya akisalimia waumini

Askofu Mkuu Eliud Issangya akiwa amekabidhiwa kesi ya birthday ya miaka 30 kuanzishwa kwa chuo cha biblia


Mchungaji Mansah akigawa vitabu vyenye historia ya miaka 30 ya kuanzishwa kwa chuo hicho

Waumini wakisikiliza kwa makini

Mmoja wa wanzilishi na mfadhili wa chuo hicho shirley Bedsole akiimba wimbo katika jubilee hiyo

wachungaji wa kanisa hilo kutoka barani Afrika wakiingia kanisani kwa maandamano

kwaya ya kanisa la International Evangelism Sakila ikitumbuiza

No comments: