Tuesday, June 4, 2013

BHARTI AIRTEL YASAIDIA KUONDOA UMASKINI KUPITIA MRADI WA MILLENIUM VILLAGE


Meneja Huduma za Jamii wa Aitel Tanzanaia- Hawa Bayumi akizungumza na wananchi waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya mradi wa Milleniaum  jijini Dar es salaam leo . Mradi huu unalenga katika
kuboresha huduma za afya na elimu vijijini kupitia technolojia ya
mawasiliano

Meneja Huduma za Jamii wa Aitel Tanzanaia- Hawa Bayumi akikabidhi SIM
card 240 za mtandao huo kwa Meneja Mkuu wa Mradi wa Millenium Village
ulioko Mkoani Tabora- Dr Gerson Nyadzi. Mradi huu unalenga katika
kuboresha huduma za afya na elimu vijijini kupitia technolojia ya
mawasiliano. Kulia ni afisa mauzo wa Airtel kanda ya ziwa Charles
Elisante, na Meneja wa Airtel money kanda ya ziwa Violet Gyumi. Hafla
ya makabidhiano ilifanyika mkoani Tabora


Bharti Airtel yasaidia kuondoa umaskini  kupitia mradi wa Millenium Village

*         Mradi huo kutoa  elimu kwa wafanyakazi wa afya kwa kupitia
huduma za mawasiliano

*         Yawawezesha wafanyakazi 240 kuwasiliana kwa gharama nafuu za pekee.

*         Airtel unasaidiana na  mradi huu wa millennium village
katika nchi 6 za Afrika


Dar es Salaam Juni 04 2013: Kampuni ya Bharti ("Airtel") inayoongoza
kwa kutoa huduma za mawasiliano inayoendesha shughuli zake katika
ndani ya nchi 20 barani Afrika na Asia, leo imethihirisha thamira yake
ya kufikia malengo ya Millenium kwa kushirikiana na kampuni ya
Erickson katika mradi maalum ujulikanao kama Millenum village
inayoendeshwa katika nchi 6 za Afrika ikiweko Tanzania.
Mradi huo umeundwa na taasisi ya Earth Institute kwa dhamira ya
kutimiza baadhi ya malengo ya Milenia kwa kuelekeza ufumbuzi wa
kiubunifu zaidi katika maeneo ya vijijini huku ikishirikiana kwa
ukaribu zaidi na kampuni ya simu za mkononi Airtel barani Afrika
Airtel imesaidia mradi wa millennium village katika mkoa wa Tabora kwa
kutoa huduma za mawasiliano zitakazowawezesha watu kupata elimu kuhusu
maswala ya afya kwa urahisi. Airtel imetoa namba ya dharura
itakayopigwa bila kutozwa gharama yoyote na kuwawezesha watoa huduma
za afya  na wagonjwa kuwasiliana kiurahisi zaidi.
Mradi wa millennium Vilage unasaidiwa na Airtel katika nchi 6 ambazo
Airtel inafanya biashara zake. Nchini Tanzania mradi wa millinium
village umeanzishwa katika eneo la Mbola mkoani Tabora na kusambaa
katika maeneo mengi na kufikia  zaidi ya vijiji 20 vilivyopo katika
eneo lenye mita za mraba 700msq likiwa na wakazi 30,0000 waishio
katika wilaya ya Uyui Tabora.
Mpaka sasa mradi huu umekuwa na mafanikio makubwa, zaidi ya watu
500,000 katika nchi 11 zilizoko kusini mwa jagwa la sahara Afrika
wamefaidika ambapo hadi kufikia mwisho wa mwaka 2011 asiliimia 90 ya
vijiji vilikuwa vimesha unganishwa na mtandao wa simu
Vile vile ndani ya mradi huu kuna kipengele cha Connect to Learn,
chenye ushirikiano baina ya  Earth Institute Chuo kikuu cha Columbia ,
Ericsson and Bharti Airtel Africa, ulioanzishwa  katika shule zilizopo
ndani ya mradi wa millennium village  na kuwafikia walimu na wanafunzi
zaidi ya 5,000 katika nchi za Ghana, Tanzania, Uganda  na Kenya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Bwana Sunil Colaso
alisema" Airtel  ina dhamira ya kugusa maisha ya watu si tu kwa kutoa
huduma za mawasiliano zenye gharama nafuu lakini pia kuwazifikia
jamii  za  chini zenye uhitaji wa technologia katika kuendeleza na
kukuza maisha yao, ambayo ndio lengo lililotufanya kushirikiana na
Earth Institute pamoja na  Erickson kusaidia mradi huu wa millennium
village.
Ushirikiano huu unatupelekea kufikia malengo ya mradi wa millennium
village ya kushughulikia changamoto za umasikini katika maeneo mengi
ikiwemo Kilimo, elimu, afya, miundo mbinu, usawa katika jinsia na
kukua kwa  Biashara. Tunafurahi kuwa sehemu ya mabadiliko na tunaahidi
kuisaidia jamii nchini Tanzania.

Akiongea wakati wa halfa ya kupanua mradi wa millennium village katika
kijiji cha Mbola mkoani Tabora, Meneja Huduma Jamii wa Airtel bi Hawa
Bayumi alisema" tunafurahi kuendelea kutimiza dhamira yetu ya kutoa
huduma za mawasiliano zenye gharama nafuu katika  vijiji mbalimbali
Tanzania . leo tunaonyesha kwa vitendo dhamira yetu na  kuwapatia
wafanyakazi 240 huduma za mawasiliano ili kuuendesha  mradi huu wa
millennium village kirahisi.  Airtel pia imetoa namba ya dharura
ambayo itaboresha upatikanaji wa huduma za afya ikiwemo huduma za
dharura na elimu ya afya katika kijiji cha Mbola"

"Huduma ya mawasiliano tuliyoitoa kwa wafanyakazi 240 ni pamoja na
kupigiana simu kwa gharama nafuu zaidi (CUG), ujumbe mfupi wa bure
pamoja na huduma ya internet ilikuwezesha mawasiliano kati yao na
jamii" aliongeza Bayumi

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha huduma kwa jamii katika nchi za
Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara Bi Margaret Kositany,
alisema" ni imani yetu kwamba kwa kuboresha mawasiliano kutawezesha
kuleta ufanisi katika huduma zetu za afya na kufanya mawasiliano ya
karibu kati ya wauguzi na wagonjwa kuwa ya rahisi, kutoa elimu kwa
jamii  kupita mitandao  na kuongeza uelewa wa elimu kwa njia ya
mtandao kwa watoto wa shule."
Mbali na  mradi wa  Millennium Villages , Airtel Tanzania iko mstari
wa mbele katika kusaidia shule za secondari nchini kwa kuwapati nyenzo
za kufundishia ikiwemo vitabu. Tangu kuanzishwa kwa  mradi wa  'Airtel
Shule Yetu'  zaidi ya shule 900 nchini zimefaidika na kupata vitabu
kutoka Airtel.
Mwisho

No comments: