Monday, June 10, 2013

KIONGOZI WA MWENGE AWAMWAGIA SIFA WAKAZI ARUMERU








 Na Mwandishi wetu, Tanzaniasasa

KIONGOZI wa mbio za mwenge wa Uhuru Juma Ali Simai amesifu ushirikiano baina ya wananchi,wadau wa maendeleo na viongozi wa serikali wilayani Arumeru katika kutimiza kwa vitendo dhana nzima ya ulinzi shirikishi na polisi jamii uliowezesha ujenzi wa kituo cha polisi katika kata ya Mlangarini.
 

Kiongozi huyo ametoa pongezi hizo alipokua akizungumza katika uzinduzi  wa kituo hicho cha polisi chenye hadhi ya daraja C kilichojengwa kwa michango ya wananchi,diwani wa kata hiyo Mathias Manga pamoja na benki ya uwekezaji Tanzania (TIB).
 

Ujenzi huo wa kituo cha polisi katika kijiji cha Chekereni umeenda sambamba na ujenzi wa nyumba za wpolisi zenye uwezo wa kuchukua familia mbili kwa wakati mmoja ujenzi ambao ulianza mnamo mwaka 2008.

Uwepo wa kituo hicho cha polisi utawezesha upatikanaji wa huduma za kipolisi katika kata ya Mlangarini,Moshono,Nduruma pamoja na maeneo jirani ya jiji la Arusha yenye jumla ya wananchi zaidi ya 19,580 ambazo hapo awali walikua wakikosa huduma  za kipolisi.


Alisema ushirikiano huo wa ujenzi wa kituo hicho cha polisi na nyumba za watumishi ni kielelezo tosha kuwa sera na madhumuni ya mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema yametimia kwakua wananchi wa wilaya hiyo wameuelewa vizuri ujmbe huo.


Alisema kufanyka kwa kazi hiyo na hatimaye kuwepo kwa kituo hicho kumewawezesha wananchi wa kata hiyo na zile za jirani kujihakikishia ulinzi na usalama wakati wote tofauti na ilivyokua hapo awali ambapo
maeneo hayo yalikua yakikabiliwa na matukio ya uhalifu mara kwa mara.


Alisema ujenzi huo umegharimu kiasi cha shiolingi milioni 240 fedha ambazo zimetokana na michango ya wafadhili mbalimbali wakiwemo wa kilimo cha maua cha Arusha Blooms waliotoa shilingi 110,wamiliki wa
mashamba makubwa wilayani humo waliotoa shilingi 85,benki ya TIB iliyotoa shilingi milioni 30.

No comments: