Monday, June 3, 2013

PARTY YA USIKU KATIKA HOTELI YA PALACE BAADA YA KUZINDUA KWA NDEGE YA AIR UGANDA, LUCY ISMAIL NDIE ALIYEKUWA AKIIONGOZA


Mrembo Lucy Ismail, Meneja  Masoko wa Air Uganda nchini akikaribisha wageni katika hafla ya pekee ya uzinduzi wa ndege ya Air Uganda katika kiwanja cha KIA katika hoteli ya Palace jijini Arusha 

Meneja Masoko wa Air Uganda Jeniffer Musiime (mwenye koti jeupe),  akizungumza na wadau pamoja na wafanyabiashara waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa ndege hiyo katika hoteli ya Palace jijini ArushaWadau mbalimbali wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi


Exaud Mwanga akichagua mshindi wa tiketi ya bure katikati ni MC katika shughuli hiyo Lucy Ismail


Mrembo Lucy Ismail akisoma mshindi wa tiketi ya kusafiri na ndege ya Air Uganda bure mbele ya wageni waliohudhuria hafla hiyo, kulia ni mgeni rasmi Exaud Mwanga ambe ndie aliyechagua mshindi hafla hiyo.

Mfanyakazi wa TANESCO Arusha aliibuka mshindi wa kwanza wa tiketi ya bure kusafiri na Air Uganda

Mfanyakazi wa EAC aliibuka mshindi wa tatu wa tiketi za kwanza katika party hiyo

Mgeni Rasmi akimwakilisha mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo, Afisa tawala msaidizi Exaud Mwanga akimpa mkono mshindi wa pili wa tiketi ya ndege

BURUDANI: Burudani haikuwa nyuma kwenye  uzinduzi wa ndege ya Air Uganda , pichani mrembo Lucy Ismail akiburudika pamoja na wafanyakazi na wadau waliohudhuria hafla hiyo

Meneja Masoko mwenye gauni jekundu  wa Air uganda nchini Lucy Ismail akisakata rumba katika party hiyo, mwenye gauni la blue ni ofisa atakayekuwa akihudumia wakazi wa jiji la Arusha Jasmin

No comments: