Friday, June 7, 2013

TRAFIKI AGONGWA AFARIKI KWENYE MSAFARA WA MAKAMU WA RAIS DKT BILAL, WENGINE WAWILI, DEREVA DALADALA MKAZI WA MOSHONO WALAZWA HOI HOSPITALI YA SELIANI

Na Seif Mangwangi,Arusha

ASKARI wa barabarani aliyetajwa kwa jina la Augustino mwenye cheo cha
Koplo wa Polisi amegongwa na gari na kufariki dunia papo hapo
alipokuwa akiongoza msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt Gharib Bilal.

Katika ajali hiyo iliyotokea jana katika eneo la barabara ya kanisani
uzunguni  karibu na hoteli ya kibo palace pia askari watatu wa
barabarani pamoja na dereva mmoja wa daladala wamejeruhiwa vibaya
katika ajali hiyo na kulazwa katika hospitali ya Seliani Mkoani hapa.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,
Liberatus Sabas aliwataja majeruhi katika ajali hiyo kuwa ni Koplo
Gadiel na Koplo Ismail ambao pamoja na marehemu walikuwa wakiongoza
magari katika eneo hilo .

Alisema majeruhi mwingine katika ajali hiyo ni dereva wa daladala
Abdul Salum mkazi wa Moshono jijini Arusha ambae

Kamanda Sabas alisema askari hao pamoja na dereva huyo waligongwa na
gari namba T 992 BQD toyota Gaia iliyokuwa ikiendeshwa na Michael
Emanuel Sarakikya ( 31), ambae ni mkazi wa Nkoaranga wilayani Arumeru.

Alisema dereva huyo ambae alitaka kukimbia baada ya ajali hiyo
alikamatwa na askari wengine waliokuwa katika eneo hilo na kufikishwa
polisi kwa mahojiano zaidi kabla hajafikishwa mahakamani.

Mashuhuda katika ajali hiyo walisema kuwa ajali hiyo ilitokea saa 7.00
mchana ambapo dereva huyo wa gari dogo aliingilia msafara wa Makamu wa
Rais Dkt Bilal na kuwagonga askari hao waliokuwa katikati ya barabara.

No comments: