Thursday, August 22, 2013

BREAKING NEWS, NDEGE NDOGO YA TANZANIAIR YAHOFIWA KUANGUKA NDANI YA ZIWA MANYARA, ABIRI WOTE WAZIMA

Ndege ya kampuni ya tanzanair iliyokuwa ikitokea bukoba kuelekea zanzibar,imeanguka hivi punde katika ziwa manyara.mpaka muda huu bado inaelea majini,abiria wote sita pamoja na pilot wa saba bado wamo ndani ya ndege.taarfa za hivi karibuni zinasema kuna bot
i imetoka serena kwenda kuwaokoa. miongoni mwa abiria waliokuwepo ndani ya ndege hiyo ndogo ni pamoja na wakili Ishengoma.

Tuesday, August 20, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT.GHARIB BILAL AZINDUA KONGAMANO LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA MABUNGE DUNIANI KATIKA OFISI ZA JUMUIYA HIYO , NYUMA YA JENGO LA MIKUTANO LA AICC JIJINI ARUSHA

Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akihutubia  wakati wa akifungua kongamano la afrika mashariki katika kuadhimisha siku ya mabunge duniani kuhusu makazi, katikati ni waziri wa Ardhi na Makazi Professa Anna Tibaijuka

Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akipanda mti wa kumbukumbu nje ya ofisi mpya za Jumuiya ya Afrika Mashariki

Wageni mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi wa kongamano hilo , kushoto ni Afisa Usalama wa Mkoa wa Arusha

Makamu wa Rais Dkt.Gharib Bilal akikata utepe kuzindua maonyesho yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuazimisha siku ya mabunge duniani

Viongozi wa Mkoa wa Arusha Mkuu wa Mkoa huo Magesa Mulongo wa kwanza kushoto, Meya Gaudence Lyimo wakisikiliza hotuba ya Makamu wa Rais wakati wa ufunguzi wa kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuazimisha siku ya mabunge duniani, anayefuatia wanne kutoka kushoto ni John Mapinduzi, Mwandishi wa hotuba wa Makamu wa Rais.

Viongozi mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Makamu wa Rais Dkt, Bilal

Makamu wa Rais Dkt. Bilal akikagua moja ya bidhaa zinazozalishwa na wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika maonyesho yaliyoandaliwa kwenye kongamano hilo

Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kusoma hotuba yake ya ufunguzi wa kongamano hilo

Makamu wa Rais Dkt.Gharib Bilal akisalimiana na mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mshariki Shyrose Bhanji

Monday, August 19, 2013

SIKU MDAU NEEMA CHALAMILA ALIPOFUNGA SAFARI YA KUTEMBELEA HIFADHI YA NGORONGORO KUJIONEA WANYAMAPORI WA KILA AINA NDANI YA BONDE HILO

Neema Chalamila akiangalia kwa kutumia kifaa maalum cha kujaribu kuona wanyama walioko mbali na eneo alilosimama katika mamalaka ya hifadhi ya Ngorongoro

Neema Chalamila kulia pamoja na washkaji zake

Neema Chalamila akiwa katika picha ya pozi katika mti ambao pia ni moja ya vivutio katika bonde la hifadhi ya Ngorongoro

Mdau Neema Chalamila akiwa amepozi juu ya boneti ya gari waliyosafiria

TANAPA PASSING OUT PARADE OF THE SECOND PHASE OF RAPID RESPONSE TEAM TRAINING IN RUAHA NP

TWENTY-TWO PARK RANGERS PASS-OUT IN THE SECOND PHASE OF THE RAPID RESPONSE TEAM TRAINING

Director General of TANAPA Allan Kijazi has said that TANAPA will work closely with various stakeholders in the country in ensuring that poaching crisis is eliminated. Kijazi said this during the pass out parade of the second phase of the Rapid Response Team training in Ruaha National Park over the weekend.

Kijazi said TANAPA has established a Rapid Response Team with a focus of prompt dealing with poaching incidences in the parks. He said that RRT is a specialized team of well-trained and specialized personnel on law enforcement with high level of discipline, motivation and morale who will react to criminal situations in the parks immediately they are reported. “The team is expected to be proactive with proper planning for crisis, threat assessment and establish counter actions,” said Kijazi.

The six weeks training involved 29 park rangers but only 22 managed to make it to the end and they were trained and assessed in operational proficiency pertaining to tactical techniques. The course was based on availing technical and tactical skills pertaining to protection of resources in the parks. The rangers were also taught to adhere to punctuality and effectiveness as key issues on maintaining their discipline.

Other areas of interest, which were imparted to the rangers, include stripping and assembling of firearms; safety precautions while using firearms, firing exercises and section battle drills.
Having been empowered with the skills, RRT rangers will then be ready to perform their day-to-day duties of dealing with poachers in an effective and efficient manner. 

The rangers were observed and given chances to demonstrate their skills shall be applied in their place of work. Their responses to situational performance such as shooting drills were observed firmly. Strongly and on the spot rectifications were done in terms of instant teaching and group discussion set up.
TANAPA and the African Field Ranger Training Services of South Africa conducted the training jointly.

 Director General of TANAPA Allan Kijazi has said that TANAPA will work closely with various stakeholders in the country in ensuring that poaching crisis is eliminated. Kijazi said this during the pass out parade of the second phase of the Rapid Response Team training in Ruaha National Park over the weekend.
Mkurugenzi  Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na Askari waliohitimu mafunzo

Kijazi said TANAPA has established a Rapid Response Team with a focus of prompt dealing with poaching incidences in the parks. He said that RRT is a specialized team of well-trained and specialized personnel on law enforcement with high level of discipline, motivation and morale who will react to criminal situations in the parks immediately they are reported. “The team is expected to be proactive with proper planning for crisis, threat assessment and establish counter actions,” said Kijazi.

The six weeks training involved 29 park rangers but only 22 managed to make it to the end and they were trained and assessed in operational proficiency pertaining to tactical techniques. The course was based on availing technical and tactical skills pertaining to protection of resources in the parks. The rangers were also taught to adhere to punctuality and effectiveness as key issues on maintaining their discipline.
Other areas of interest, which were imparted to the rangers, include stripping and assembling of firearms; safety precautions while using firearms, firing exercises and section battle drills.
 
Director General of TANAPA Allan Kijazi addressing Park Rangers who passed out the second phase of RRT training in Ruaha National Park
 
Having been empowered with the skills, RRT rangers will then be ready to perform their day-to-day duties of dealing with poachers in an effective and efficient manner.
The rangers were observed and given chances to demonstrate their skills shall be applied in their place of work. Their responses to situational performance such as shooting drills were observed firmly. Strongly and on the spot rectifications were done in terms of instant teaching and group discussion set up.

TANAPA and the African Field Ranger Training Services of South Africa conducted the training jointly.

Director General of TANAPA Allan Kijazi inspecting a parade of the park rangers who attended the second phase of RRT training in Ruaha National Park.

Martin Loibooki who is the Director of Resources Conservation (right) with Commander Venance Tossi.

Rapid Response Team taking their oath of allegiance before the guest of honor during their pass out parade in Ruaha National Park

RRT demonstrates on how to approach poachers in the field

RRT demonstrates on the exchange of fire to poachers

TANAPA's Director of Resources Conservation and Ecological Monitoring Martin Loibooki give out welcoming remarks to Director General Allan Kijazi

Trainers Genes Shayo and Martin Mthembu showing guest of honor how the target was hit by the RRT

Wardens from TANAPA watching attentively progress of the event. They are from left Dr. Christopher Timbuka, John Shemkunde, Mtango Mtahiko and Godwell Meing'ataki

Saturday, August 17, 2013

NHC YAINGIA MKATABA WA UJENZI WA NYUMBA ZA WAFANYAKAZI NA HALMASHAURI YA MONDULI

NA MWANDISHI WETU, TANZANIASASA

 SHIRIKA la nyumba la Taifa (NHC), limeingia mkataba wa bilioni 5 na  Halmashauri ya wilaya ya Monduli kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za  wafanyakazi wa Halmashauri hiyo kwa lengo la kuwaondolea adha ya

mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akimsikiliza mkuu wa Wilaya ya Monduli Jowika Kasunga akitoa maelezo kuhusu eneo ambalo litajengwa nyumba za wafanyakazi wa Halmashauri ya Monduli na shirika la nyumba la Taifa NHC, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi msaidizi ujenzi wa NHC mhandisi Benedict Kilimba, kulia kwa mkuu wa Mkoa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli aliyevaa miwani ni Meneja wa NHC Arusha, James Kisarika
 ukosefu wa makazi  wafanyakazi wanaopangiwa kufanyakazi katika  halmashauri hiyo.

 Akitoa taarifa ya ujenzi wa nyumba hizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Magesa Mulongo, jana wilayani Monduli , Kaimu Mkurugenzi wa ujenzi wa  shirika la nyumba la Taifa, Mhandisi Benedict Kilimba alisema shirika  la nyumba limeshatenga shilingi bilioni  5 kwa ajili ya ujenzi huo  ambao unatarajiwa kuanza mapema Oktoba mwaka huu.

 Alisema Halmashauri ya Monduli imetenga maeneo mawili ikiwemo la ekari  1.8 na eneo lingine lenye ukubwa wa ekari tatu ambapo kwa pamoja  zitajengwa nyumba za ghorofa moja moja zitakazo kuwa na uwezo wa  kukaliwa na familia 40.

 “ Pia halmashauri imetupatia eneo lingine lenye ukubwa wa ekari 11  ambazo pia tutajenga nyumba ambazo tutaziuza kwa wananchi wa Monduli  na maeneo ya jirani na zitakazobakia tutazipangisha kwa wale
 watakaohitaji huduma hiyo,”alisema Kilimba.

 Aidha alisema shirika hilo liko kwenye mikakati ya kuanza ujenzi wa  miji mwili ya kisasa (satellite Town), jijini Arusha katika eneo la  Matevez na Usa river wilayani Arumeru ambayo itakuwa na huduma zote za
 kijamii ikiwemo soko la kisasa.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akimsikiliza mhandisi Morgan Nyoni wa kitendo cha ubunifu wa shirika la nyumba la taifa NHC kuhusu michoro ya majengo yatakayojengwa katika Halmashauri ya Monduli

 “Shirika limeshapata maeneo mawili jijini Arusha ambayo tunatarajia  kuanza ujenzi wa miji ya kisasa ‘satelite town’, katika eneo la  Matevez shirika limeshapata eneo la ukubwa wa ekari 500 ambapo
 zitajengwa nyumba zaidi ya 7000 na katika mji wa Usa-river shirika  limepata eneo la ukubwa wa ekari 3000 na tunatarajia kujenga nyumba  zaidi ya 3000,”alisema.

 Alisema katika wilaya ya Longido, shirika hilo litajenga nyumba 58  ambapo ujenzi unatarajiwa kuanza Septemba 15 mwaka huu na kwamba  wilayani Karatu shirika hilo limepewa ekari 200.

 Akizungumzia ujenzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alitoa  wito kwa wakazi wa miji ambapo ujenzi wa nyumba hizo unatarajiwa  kujengwa kuonyesha ushirikiano kwa shirika hilo kwa lengo la
 kufanikisha miradi hiyo kukamilika kwa wakati.

 Pia alitoa wito kwa watendaji wa Halmashauri ambazo bado hazijatenga  maeneo ya ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika hilo  kutenga maeneo hayo haraka ili kuwaondolewa wakazi wa maeneo hayo
 ikiwemo wafanyakazi usumbufu wa ukosefu wa nyumba za kupanga.

Wednesday, August 14, 2013

UMATI MKUBWA WAJITOKEZA KUMZIKA BILIONEA WA TANZANITE, SERIKALI YAAHIDI KUWASAKA WALIOUA, AZIKWA BILA KUTOLEWA RISASI



NA MWANDISHI WETU, MIRERANI

SERIKALI imesema mpaka kufikia wiki ijayo, mtandao  wa mauaji ya kinyama ya mfanyabiashara bilionea wa Tanzanite, Erasto Msuya (43), aliyeuliwa kwa kupigwa risasi lukuki mwilini, eneo la KIA wakati wa
mauziano ya madini,  utawekwa hadharani na kufikishwa Mahakamani.

Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa mulongo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara na kamati ya ulinzi na usalama wa Mikoa  mitatu ya Kilimanjaro, Manyara na Arusha, wakati alipokuwa akitoa rambirambi yake kwenye mazishi ya kifahari ya mfanyabiashara huyo  yaliofanyika kijiji cha Kairo Mererani, Mkoani Manyara.

Alisema kuwa tayari kama serikali kwa kushirikiana na kamati za ulinzi  na usalama wa mikoa hiyo mitatu, mpaka kufikia wiki ijayo watakuwa  wamekamilisha kupata mtandao wote wa majuaji hayo ya kinyama na kuweka  hadharani ili kila mtu afahamu.

“Mtandao huu tunahakikisha hadi wiki ijayo tutaweka hadharani na hawa  watu watafikishwa mahakamani, na kwa kuwa tunafanya kazi kwa pamoja  kazi imekuwa rahisi kwetu “alisema Mulongo.

Katika Mazishi hayo ambayo yamehudhuriwa na maelfu ya wananchi kutoka  Mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na viunga vyake walijitokeza  kumzika mfanyabiashara huyo, huku eneo la msiba kukiwa na vyoo vya  kisasa vyenye uwezo wa kuvinyanyua na kuondoka navyo.

Pamoja na hilo jeneza la bilionea huyo limekuw agunzo kutokana na kufunguliwa kwa Remote na kufungwa kwake pia, huku magari ya kubeba wagonjwa ya hadhi yakiwepo eneo hilo,pamoja na vikosi vya ulinzi na
usalama wa askari wa KK Guard Security vikitanda eneo la msiba.

Naye Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, akitoa rambirambi kwa niaba ya serikali , alisema kuwa Rais amesikitishwa na msiba huo na ametuma pole kwa ndugu jamaa na marafiki.

“Rais amesikitishwa sana na msiba huu na ametoa pole kw andugu, jamaa  na marafiki wa  marehemu,”alisema Masele.

Kwa upande wake Askofu wa Dayosisi ya Meru wa Kanisa la Kiinjili la  Kilutheri Tanzania (KKKT), Paulo Akyoo, ambaye aliongoza ibada ya  marehemu, alikemea watu wanaotoa roho z awenzao ili wapate utajiri.

Alisema kuwa watu waliofanya kitendo cha mauaji hayo ya kinyama na  mengine, wataendelea kuteswa na roho ya mauti na dhambi hiyo itasambaa  katika mioyo yao,”alisema.

“Mungu ndiyo mwenye uwezo wa kuchukua uhai wa mtu na siyo binadamu mwingine yoyote, hii ni dhambi kubwa sana,”alisema Askofu Akyoo.

Alisema kwa dunia ya sasa wapo watu wengi wamepta utajiri kwa kufanya kafala kwa kuua watoto na watu mbalimbali,  ili kuendeleza migodi yao,  hivyo tabia hiyo siyo nzuri na haimpendezi mungu.

Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina mmoja wa ndugu wa marehemu, alisema kuwa marehemu alipigwa risasi 21, huku risasi  mbli alipigwa katika paji la uso, ambapo moja ilishindikana kutolewa kwa sababu ya
kuhofia kuharibu sura ya marehemu na amezikwa nayo.

Marehemu huyo ameacha mke na watoto wanne ambao nia Esta Msuya, Glory  Msuya, Simon Msuya ambaye yuko nchini Australia na Stephen Msuya.
 Pia katika uhai wake alikuwa akimiliki  Hoteli ya kifahari  ijulikanayo kwa jina la SG Resolt, migodi mitatu ambayo miwili kati ya hiyo ya baba yake na malizzingine lukuki.

Mfanyabiashara huyo aliuwawa kinyama kwa kupigwa risasi Agosti 7 mwaka  huu, majira ya saasita mchana huko eneo la KIA, kwenye miti aina ya  Mijohoro, katika barabara ya Moshi Arusha, wakati alipoitwa na
wafanyabiashara wenzake wa madini ili kumuuzia madini ya Tanzanite.

Monday, August 12, 2013

TAHARUKI MSIBA WA BILIONEA MSUYA: NDUGU NA MAJIRANI WAZIMIA, WAPEWA HUDUMA YA KWANZA

BABA WA MAREHEMU MZEE ELISARIA AKIAGA MWILI WA MWANAE JANA
Na MWANDISHI WETU,  ARUSHA

ZOEZI la kuaga mwili wa marehemu, mfanyabiashara wa madini ya
Tanzanite Erasto Msuya (43), jana nusura liingie dosari baada ya
baadhi ya waombolezaji kupoteza fahamu na kuacha taharuki kubwa
miongoni mwao.

Miongoni mwa waliopoteza fahamu na kulazimika kupewa huduma  ya kwanza  kupitia gari la wagonjwa la kampuni ya ulinzi ya KK Security ya jijini
Arusha ni pamoja na mdogo wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Atu Msuya  ambae anaelezwa kuwa karibu na marehemu wakati wa uhai wake.

Wengine waliozimia na kupatiwa huduma ya kwanza ni wanawake watatu  ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja lakini hata hivyo  baada ya kuwekezwa hewa ya oxygen walizinduka.

MKE WA MAREHEMU MIRIAM MSUYA AKIMBUSU MAREHEMU
Kwa mujibu wa  kaka wa Marehemu Israel Msuya, mwili wa mfanyabiashara  huyo Erasto Msuya (43), aliyeuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya kumi na  watu wasiojulikana unatarajiwa kuzikwa leo alasiri nyumbani kwa wazazi  wake Kairo, Mirerani wilayani Simanjiro,Manyara.

Maombolezo na mazishi ya mfanyabiashara huyo aliyekuwa akimiliki mali  kadhaa kipindi cha uhai wake yalipangwa kugharimu zaidi ya shilingi  milioni 100, huku jeneza na gari maalum ya kubeba mwili yakiagizwa  kutoka jijini Nairobi, Kenya.

Gharama ya jeneza pamoja kukodisha gari ilikadiriwa kuwa shilingi  milioni nane huku kiasi kinachosalia kikipangwa kugharamia vyakula na  vinywaji tangu siku ya kwanza ya msiba hadi mazishi ya leo.

Msuya anayemiliki hoteli ya kitalii ya SG Resort jijini Arusha pamoja  na mali kadhaa yakiwemo nyumba za kuishi, biashara na magari ya  kifahari ikiwemo aina Range Rover New Model iliyotengenezwa mwaka huu  wa 2013, alipigwa risasi eneo la Mjohoroni, katikati ya Uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro na mji wa Bomang’ombe.

Katika uhai wake, Msuya alikuwa akijihusisha na uchimbaji na biashara  ya madini ya Tanzanite akimiliki migodi katika vitalu ‘B’ na ‘D’ huko  Mirerani.

Licha ya kuacha gumzo, kifo cha mfanyabiashara huyo kimezua  sintofahamu miongoni mwa wafanyabiashara wenzake, huku wengi wakihoji  sababu za kuuawa kwa kumiminiwa risasi nyingi kiasi hicho ambapo  baadhi wanahusisha tukio hilo na visasi vya kibiashara na uhasama miongoni mwa wafanyabiashara hao.



MKE WA MAREHEMU, MIRIAM MSUYA AKILIA KWA UCHUNGU


MKE WA MAREHEMU MIRIAM MSUYA PAMOJA NA MWANAE PEKEE WA KIUME WAKIANGALIA MWILI WA MAREHEMU KWA UCHUNGU

MKE WA MAREHEMU MIRIAM AKIUCHUNGUZA KWA UCHUNGU MWILI WA MUMEWE

DADA WA MAREHEMU AKILIA KWA UCHUNGU NA BAADAE KUPOTEZA FAHAMU




DADA WA MAREHEMU

PICHA MBALIMBALI WAKAZI WA ARUSHA WAKIAGA MWILI WA BILIONEA ERASTO MSUYA ALIYEPIGWA RISASI NA WATU WASIOJULIKANA, AGOSTI 7 MWAKA HUU