Wednesday, August 14, 2013

UMATI MKUBWA WAJITOKEZA KUMZIKA BILIONEA WA TANZANITE, SERIKALI YAAHIDI KUWASAKA WALIOUA, AZIKWA BILA KUTOLEWA RISASI



NA MWANDISHI WETU, MIRERANI

SERIKALI imesema mpaka kufikia wiki ijayo, mtandao  wa mauaji ya kinyama ya mfanyabiashara bilionea wa Tanzanite, Erasto Msuya (43), aliyeuliwa kwa kupigwa risasi lukuki mwilini, eneo la KIA wakati wa
mauziano ya madini,  utawekwa hadharani na kufikishwa Mahakamani.

Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa mulongo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara na kamati ya ulinzi na usalama wa Mikoa  mitatu ya Kilimanjaro, Manyara na Arusha, wakati alipokuwa akitoa rambirambi yake kwenye mazishi ya kifahari ya mfanyabiashara huyo  yaliofanyika kijiji cha Kairo Mererani, Mkoani Manyara.

Alisema kuwa tayari kama serikali kwa kushirikiana na kamati za ulinzi  na usalama wa mikoa hiyo mitatu, mpaka kufikia wiki ijayo watakuwa  wamekamilisha kupata mtandao wote wa majuaji hayo ya kinyama na kuweka  hadharani ili kila mtu afahamu.

“Mtandao huu tunahakikisha hadi wiki ijayo tutaweka hadharani na hawa  watu watafikishwa mahakamani, na kwa kuwa tunafanya kazi kwa pamoja  kazi imekuwa rahisi kwetu “alisema Mulongo.

Katika Mazishi hayo ambayo yamehudhuriwa na maelfu ya wananchi kutoka  Mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na viunga vyake walijitokeza  kumzika mfanyabiashara huyo, huku eneo la msiba kukiwa na vyoo vya  kisasa vyenye uwezo wa kuvinyanyua na kuondoka navyo.

Pamoja na hilo jeneza la bilionea huyo limekuw agunzo kutokana na kufunguliwa kwa Remote na kufungwa kwake pia, huku magari ya kubeba wagonjwa ya hadhi yakiwepo eneo hilo,pamoja na vikosi vya ulinzi na
usalama wa askari wa KK Guard Security vikitanda eneo la msiba.

Naye Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, akitoa rambirambi kwa niaba ya serikali , alisema kuwa Rais amesikitishwa na msiba huo na ametuma pole kwa ndugu jamaa na marafiki.

“Rais amesikitishwa sana na msiba huu na ametoa pole kw andugu, jamaa  na marafiki wa  marehemu,”alisema Masele.

Kwa upande wake Askofu wa Dayosisi ya Meru wa Kanisa la Kiinjili la  Kilutheri Tanzania (KKKT), Paulo Akyoo, ambaye aliongoza ibada ya  marehemu, alikemea watu wanaotoa roho z awenzao ili wapate utajiri.

Alisema kuwa watu waliofanya kitendo cha mauaji hayo ya kinyama na  mengine, wataendelea kuteswa na roho ya mauti na dhambi hiyo itasambaa  katika mioyo yao,”alisema.

“Mungu ndiyo mwenye uwezo wa kuchukua uhai wa mtu na siyo binadamu mwingine yoyote, hii ni dhambi kubwa sana,”alisema Askofu Akyoo.

Alisema kwa dunia ya sasa wapo watu wengi wamepta utajiri kwa kufanya kafala kwa kuua watoto na watu mbalimbali,  ili kuendeleza migodi yao,  hivyo tabia hiyo siyo nzuri na haimpendezi mungu.

Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina mmoja wa ndugu wa marehemu, alisema kuwa marehemu alipigwa risasi 21, huku risasi  mbli alipigwa katika paji la uso, ambapo moja ilishindikana kutolewa kwa sababu ya
kuhofia kuharibu sura ya marehemu na amezikwa nayo.

Marehemu huyo ameacha mke na watoto wanne ambao nia Esta Msuya, Glory  Msuya, Simon Msuya ambaye yuko nchini Australia na Stephen Msuya.
 Pia katika uhai wake alikuwa akimiliki  Hoteli ya kifahari  ijulikanayo kwa jina la SG Resolt, migodi mitatu ambayo miwili kati ya hiyo ya baba yake na malizzingine lukuki.

Mfanyabiashara huyo aliuwawa kinyama kwa kupigwa risasi Agosti 7 mwaka  huu, majira ya saasita mchana huko eneo la KIA, kwenye miti aina ya  Mijohoro, katika barabara ya Moshi Arusha, wakati alipoitwa na
wafanyabiashara wenzake wa madini ili kumuuzia madini ya Tanzanite.

No comments: