Friday, September 27, 2013

WAANDISHI WA HABARI ZAIDI YA 40 KUTOKA NCHI ZA KENYA, UGANDA NA TANZANIA WALIOKUWA WAKIHUDHURIA KONGAMANO LA MESHA NCHINI KENYA WANUSURIKA KATIKA AJALI YA MOTO BAADA YA HOTELI WALIYOFIKIA KUUNGUA

Mmiliki wa mtandao huu, Seif Mangwangi kulia akiwa na mwandishi wa habari wa Raia Mwema Paul Sarwat nje ya jengo la hoteli ya Galexon jijini Nairobi muda mfupi baada ya kukimbia ndani ya vyumba kufuatia jengo hilo kuanza kuwaka moto, hata hivyo kampuni ya ulinzi ya G4S ya jijini Nairobi ilifika baada ya zaidi ya saa moja kupita tangu moto huo ulipoanza kuwaka na kufanikiwa kuzima moto huo

Wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya G4S wakijiandaa kuanza kuzima moto uliokuwa ukiunguza hoteli ya Galexon jijini Nairobi usiku wa kuamkia leo 

Katibu Mkuu wa chama cha waandishi wa habari za Sayansi, Kilimo, Afya na mazingira nchini Kenya, Aghan Daniel katikakati(mwenye shati jeupe),  akizungumza na waandishi wa habari walionusurika katika ajali ya hoteli ya Galexon kuungua moto jijini Nairobi usiku wa kuamkia leo. waandishi hao walihamishiwa hoteli ya Delta iliyoko katikati ya jiji la Nairobi

Thursday, September 26, 2013

KENYA YAFANIKIWA KUTEKELEZA MALENGO YA MILENIUM, YATOKOMEZA UGONJWA WA KIFUA KIKUU






 



































NA SEIF MANGWANGI, NAIROBI

SERIKALI ya Kenya imesema kuwa imefanikiwa kutekeleza malengo ya millennia katika sekta ya afya kwa kutokomeza maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu uliokuwa miongoni mwa magonjwa makuu yaliyokuwa yakiua maelfu ya wananchi wa Kenya.

Akizungumza katika hotuba yake ya ufunguzi wa kongamano la chama cha waandishi wa habari za sayansi, kilimo na afya nchini Kenya (MESHA), Mkurugenzi wa idara ya Afya nchini Kenya,  Dkt Shahnaz Sharrif alisema jitihada za kutokomeza ugonjwa huo ni matokeo mazuri ya utendaji wa
watafiti nchini Kenya.

Alisema katika utekelezaji wa malengo ya dunia ya millennia namba sita, wizara ya afya imekuwa ikipambana na magonjwa sugu ambayo yamekuwa yakisababisha vifo vya wakenya wengi na kufanikiwa kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu.

Dkt.Sharrif alisema mapambano ya ugonjwa huo yamechangiwa na sekta mbalimbali ikiwemo waandishi wa habari za sayansi, afya na mazingira ambao wamekuwa wamekuwa wakiandika taarifa  tofauti kuhusu madhara na namna ambavyo ugonjwa huo umekuwa ukiambukiza.
“Pia Serikali imekuwa katika mapambano ya kutokomeza magonjwa mengine sugu kama Malaria na Ukimwi ambayo yamekuwa yakiua sehemu kubwa ya wakenya, hata hivyo mapambano haya bado yanahitaji jitihada za pamoja,”alisema.
Dkt.Sharrif alisema katika kuboresha sekta ya afya nchini Kenya, nchi hiyo imeanza utekelezaji wa matakwa ya katiba ya nchi hiyo yanayoiagiza Serikali kuteremsha majukumu ya kupanga shughuli za maendeleo katika ngazi za chini.
Aliwataka waandishi wa habari nchini Kenya kuendelea kutoa elimu sahihi kwa wananchi kuhusiana na upelekwaji wa madaraka hayo ngazi za chini ambapo wananchi watapata nafasi ya kuamua shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Kongamano hilo la siku tatu lililoenda sanjari na mkutano mkuu wa chama cha waandishi wa habari za sayansi,kilimo na afya nchini Kenya (MESHA),  limekutanisha watafiti kutoka katika taasisi mbalimbali za sayansi, kilimo, afya na waandishi wa habari kutoka nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.
Ends…

Wednesday, September 18, 2013

KLABU YA WAANDISHI WA HABARI ARUSHA YATOA TUZO KWA TANAPA KWA KUTAMBUA MSAADA INAOPATA KUTOKA KATIKA SHIRIKA HILO

Katibu waw APC Semmy Kiondo akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi, fulana yenye nembo ya klabu hiyo 

Katibu Mkuu wa APC akimsaidia mkurugenzi mkuu wa TANAPA Allan Kijazi kuweka fulani ndani ya mfuko

Mwenyekiti wa APC, Claud Gwandu akimkabidhi tuzo ya heshima mkurugenzi wa TANAPA Allan Kijazi kwa kutambua mchango wa shirika hilo kwa APC 

Katibu Mkuu wa APC Semmy Kiondo akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijana mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kumkabidhi tuzo kwa kutambua mchango wa shirika hilo kwa APC 

Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi, akisalimiana na mjumbe wa kamati ya utendaji Janeth Mushi. katikati ni mwekahazina wa APC Pamela Mollel

WAZIRI MAGHEMBE AINUSURU POLISI ARUSHA KUKATIWA MAJI KWA DENI LA MIL300

Wafanyakazi wa Mamlaka ya maji Arusha (AUWSA) wakimsikiliza waziri maghembe 

Mkurugenzi wa AUWSA Injinia Ruth Koya akiwasilisha taarifa ya AUWSA mbele ya waziri wa maji Jumanne Maghembe 

Waziri wa Maji Jumanne Maghembe akizungumza na wafanyakazi pamoja na bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya maji Arusha AUWSA 

Waziri wa maji Jumanne Maghembe akizindua bodi ya mamaka ya maji jiji la Arusha (AUWSA)

Waziri wa Maji Jumanne Maghembe akimkabidhi nyaraka za mamlaka ya AUWSA Mwenyekiti mpya Felix Mrema 

Waziri wa maji Jumanne Maghembe akimkabidhi mwenyekiti wa bodi ya AUWSA Felix Mrema zawadi 

Makamu Mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya maji ya AUWSA Anold Kileo akipokea zawadi ya utendaji bora wa bodi iliyopita kutoka kwa waziri wa maji Jumanne Maghembe

NA MWANDISHI WETU, TANZANIASASA
WAZIRI wa maji Professa Jumanne Maghembe juzi alilazimika kuingilia kati na kuiagiza Mamlaka ya maji jiji la Arusha (AUWSA), kusitiza zoezi la kuwakatia maji wadaiwa sugu taasisi za Serikali ikiwemo jeshi
la Polisi Arusha linalodaiwa deni la maji milioni 308.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya wakurugenzi wa mamlaka hiyo, Waziri Maghembe aliiagiza mamlaka hiyo kumwachia jukumu la kuzungumza na viongozi wa mamlaka za Serikali zinazodaiwa na mamlaka hiyo.

Waziri Maghembe alisema Mamlaka za maji nchini zinakabiliwa na changamoto kubwa ya upotevu wa mapato ikiwemo kupotea kwa maji kwa asilimia 38 ya maji yote yanayozalishwa na mamlaka hizo  na
kusababisha upotevu wa bilioni2 kwa kila mwezi.

 “Nawaomba hili suala la Mamlaka za Serikali kudaiwa mniachie nipambane nalo kwanza msiwakatie maji mpaka nitakapoonana nao, lakini pia hakikisheni mnapambana na changamoto zingine kama vile kuongeza
ukusanyaji wa mapato hadi kufikia asilimia 100 kutoka asilimia 93 mliyokuwa nayo hivi sasa,”alisema.

Waziri Maghembe pia aliiagiza bodi ya mamlaka hiyo kushirikiana na mamlaka za Mkoa na Wilaya za Arusha kutafuta vyanzo vipya vya maji na kuvihifadhi ili kusaidia upatikanaji wa maji kwa miaka ijayo wakati
vyanzo vilivyopo hivi sasa vitakapokauka.

“ Utafiti unaonyesha eneo la viwanja vya burka hadi Ngaramtoni ndio kuna maji mengi chini lakini badala ya kuchukua viwanja na kuvitunza kwa ajili ya baadae nyie mmeuza viwanja watu wanajenga maghorofa, hii
sio sahihi kabisa, bodi nawaagiza mtafute viwanja katika eneo hilo kwa ajili ya vizazi viavyo pindi maji yatakapopungua hapo baadae katika maeneo ambayo mnatumia hivi sasa,”alisema.

Awali Mwenyekiti wa bodi ya mamlaka hiyo mbunge wa zamani wa jimbo la Arusha, Felix Mrema aliigiza menejimenti na  wafanyakazi wa mamlaka hiyo kufanyakazi kwa malengo ili kujiongezea mapato na wao kupata maslahi mazuri.

“  Endapo mtakusanya mapato ya kutosha na kutokomeza tatizo la upotevu wa maji ambalo ni zaidi ya bilioni mbili hivi sasa basi  na nyie mtapata mshahara mzuri kwa kuwa fedha itakuwepo, na kwa taarifa yenu sisi tunalipata mshahara kutokana na makusanyo tunayoyafanya, hivyo
fanyeni kasi kwa kazi ili mapato yaongezeke,”alisema Mrema.

Awali katika taarifa yake, Mkurugenzi wa mamalaka hiyo Injinia Ruth Koya alisema AUWSA kwa kushirikiana na wizara ya Maji imetenga bajeti ya bilioni 1.98 kwa mwaka wa fedha 2013/14 kuongeza usambazaji wa maji kwa kuchimba visima virefu na ujenzi wa tenki katika maeneo ya Sokoni1, Moshono, Olasiti, na Esami.

UKARIMU WA WATANZANIA KWA WAGENI NI TATIZO KWA WAJASIRIAMALI - MKURUGENZI MPINGO SUMMIT


Mkurugenzi wa Global Skills Bakiri Angalia akifungua mafunzo ya wajasiriamali katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa AICC jijini Arusha hivi karibuni 

Kaimu Katibu Mkuu wizara ya habari na utamaduni Elisante,  akitoa mada katika mkutao huo 

Kutoka kushoto Mkurugenzi wa REPOA Professa Wangwe,  Mkurugenzi wa Kidot Love, Jocket Mwegelo, Mkurugenzi wa Global Skill na waandaaji wa mkutano wa MPIGO SUMMIT Bakili Angalia, Mkuu wa chuo cha MS-TCDC Dkt Kaare na MC maarufu nchini Taji Liundi wakimsikiliza kaimu Katibu Mkuu wizara ya Habari na utamaduni (hayupo pichani), Dkt Elisante alipokuwa akiwasilisha mada katika mkutano huo.


IMEELEZWA kuwa kutokuwa makini wafanyabiashara wa kitanzania na ukarimu wao dhidi ya wageni wanaokuja nchini kwa lengo la kuwekeza katika sekta mbalimbali ni hatari kwa maslahi ya nchi jambo linaloweza kusababisha kuporomoka kwa uchumi wa nchi.

Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Mkurugenzi wa kampuni ya Global Skill and education ya jijini Arusha, Bakiri Angalia katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa wajasiriamali na wafanyabiashara
unaofanyika jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC.

Angalia alisema viongozi wa nchi nyingi duniani wamekuwa wakiwaeleza wananchi wa nchi zao kuwekeza nchini kufuatia watanzania kuwa wakarimu katika Nyanja mbalimbali jambo ambalo ni hatari kwa uchumi wa nchi kufuatia wageni hao kutumia mwanya wa watanzania kutokuwa makini kufaidi tunu ya taifa.

Alisema uwekezaji ni jambo zuri ambalo kila kiongozi katika nchi analifurahia lakini hata hivyo wenyeji wanatakiwa kuwa makini  na uwekezaji huo kama ambavyo imekuwa ikifanyika katika nchi zingine
ikiwemo Kenya na Uganda.

“ Katika hotuba ya mmoja wa mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini alishawahi kusema kuwa kuwekeza Tanzania ni vizuri sana kwa kuwa watanzania ni wakarimu tofauti na nchi zingine kama za Kenya na Uganda, mimi binafsi nilisikitishwa sana na kauli hii kwa kuwa watanzania hatuko makini tunaweza kujikuta tunaumizwa kwa uwekezaji huo,”alisema.

Akiwakilisha mada katika mkutano huo, Mkuu wa chuo cha maendeleo cha MS-TCDC, Dkt.Suma Kaare alitoa wito kwa watafiti na wakufunzi katika vyuo vikuu mbalimbali nchini kufanya utafiti katika biashara za ndani ili kupata jibu la kutofanikiwa kwa wafanyabiashara hao.

“ Ukiwa shuleni utapata uzoefu kutoka biashara za wafanyabiashara wakubwa nje ya nchi lakini ni wakati sasa kwa wakufunzi na watafiti nchini kufanya utafiti wao kwa wafanyabiashara wa nchini ili kujua
tatizo ambalo limekuwa likisababisha kuanguka kwa biashara zao na kuwa somo kwa wafanyabiashara wengine,”alisema Dkt.Kaare.

Aliwataka wafanyabiashara kujifunza kwa wafanyabiashara wengine namana ambavyo wamefanya na kufanikiwa ili kuboresha biashara zao na kuvifanya kuwa endelevu.

Sunday, September 15, 2013

MAMIA WAJITOKEZA KUPOKEA WALIOANDAMANA KUPINGA UJANGILI NA PEMBE ZA NDOVU NCHINI



Na Mwandishi Wetu, TANZANIASASA
MAMIA ya wakazi wa jiji la Arusha, juzi walijitokeza katika uwanja mdogo wa ndege Arusha kuwapokea watu walioandamana kwa kutembea kwa miguu kutoka Arusha hadi jijini Dar es Salaa kupinga vitendo vya ujangili na biashara ya pembe za ndovu.
Maandamano hayo yaliyozinduliwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo Agosti 24, mwaka huu na kupokelewa jijini Dar es Salaam Septemba 12, mwaka huu na Naibu waziri wa Utalii na Maliasili, Lazaro Nyalandu, yaliandaliwa na kuongozwa na Mtanzania mwenye asili ya Asia, Pratik Patel kupitia Taasisi ya African Wildlife Trust ya jijini Arusha.
Pamoja na Patel, muandamanaji mwingine aliyeanzia safari yake kutoka Arusha katika eneo la jengo la Mkuu wa mkoa hadi Dar es Salaam ni raia wa Marekani, Maraya Cornel.
Akizungumza mara baada ya mapokezi hayo, Patel aliwataka Watanzania wote kushiriki vita dhidi ya ujangili na biashara ya pembe za ndovu kwani jukumu la ulinzi wa marasilimali za taifa linahusu raia wote bila kujali tofauti zao kiuchumi, kisiasa na kimaeneo (kikabila).
“Taasisi kama Shirika la hifadhi za taifa (TANAPA) na Mamlaka ya bonde la Ngorongoro (NCAA) na mamlaka zingine za serikali zimepewa tu dhamana ya kusimamia na kuongoza shughuli za uhifadhi. Lakini ukweli ni kwamba sote tuna wajibu wa kulinda rasilimali zetu kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo,” alisema Patel
Kwa upande wake, mmoja wa waongoza watalii aliyehudhuria mapokezi hayo, Engbeth Quorro aliwaomba viongozi serikalini na wale wa kisiasa kuwa na dhamira safi katika usimamizi wa maliasili na rasilimali za taifa.
“Wote wenye dhamira mbaya na rasilimali zetu wadhibitiwe mara moja bila kujali nyadhifa zao hata itakapobainika kuwa miongoni mwao wamo viongozi wa serikali au wanasiasa wenye ushawishi,” alisema Quorro
Awali akizindua maandamano hayo wiki tatu zilizopita, Mkuu wa Arusha, Mulongo alisema ni wajibu wa kila Mtanzania kushiriki vita dhidi ya ujangili kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kuwatia mbaroni wanaojihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo.
“Wahifadhi, wasimamizi na watekelezaji wa sheria za uhifadhi watimize wajibu na majukumu yao kwani wasipofanya hivyo hawatabaki salama katika msako dhidi ya majangili unaoendelea,” alisema Mulongo
Kaimu Mkuu wa Kikosi cha kupambana na ujangili Kanda ya Kaskazini, Michael Melakiti alisema kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita pekee, watuhumiwa 64 wametiwa mbaroni kwa makosa ya kujihusisha na ujangali katika kanda hiyo ambapo 51 kati yao walipigwa faini ya Sh. 10.6 milioni.
Melakiti alisema kipindi hicho kinachoanzia Juni mwaka jana hadi Juni mwaka huu, watuhumiwa 11 walifikishwa mahakamani na kesi zao ziko katika hatua mbalimbali huku mmoja akipewa onyo kwa maandishi.
Alisema katika kipindi hicho, jumla ya Tembo 29 waliuawa na nyara zake kuchukuliwa na majangili. Tembo hao waliuawa katika wilaya za Ngorongoro, Rombo, Monduli, Longido na Simanjiro.
Licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa, sekta ya utalii nchini inachangia asilimia 17 ya pato la taifa.
Mwisho.

Tuesday, September 10, 2013

TANAPA YAAHIDI USHIRIKIANO ENDELEVU NA APC, NI BAADA YA KAMATI YA UTENDAJI KUMTEMBELEA MKURUGENZI MKUU OFISINI KWAKE

Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi

Wajumbe wa kamati ya utendaji wakiwa ofisini kwa mkurugenzi mkuu wa TANAPA,

Katibu msaidizi wa APC, Mustafa leu (hayupo pichani), akijitambulisha kwa mkurugenzi wa TANAPA Mbele aliyevaa miwani

Kutoka kulia David Frank, Mustafa Leu, Semmy Kiondo na Pascal Shelutete wakiwa ofisini kwa mkurugenzi Mkuu wa TANAPA

Mwenyekiti wa APC, Claud Gwandu akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa kamati ya utendaji walipomtembelea Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi anayesikiliza ofisini kwake jana

Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete kushoto, Semmy Kiondo (Katibu Mkuu wa APC), na Mustafa Leu (Katibu Msaidizi), wakimsilikiza mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi (hayupo pichani).

Katibu Msaidizi wa APC, Semmy Kiondo akichangia jambo katika ziara hiyo ofisini kwa mkurugenzi mkuu wa TANAPA

Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akichukua dondoo katika mkutano huo mfupi

Makamu Mwenyekiti wa APC, Charles Ngereza akisaini kitabu cha wageni

Mjumbe wa kamati ya utendaji Janeth Mushi akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa TANAPA (hayuko pichani)


Mkurugenzi wa TANAPA, Allan Kijazi akizungumza katika kikao hicho kifupi, nakuahidi kuendelea kushirikiana na APC katika shughuli zake

Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi

Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi akiagana na Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu

Katibu Mkuu wa APC, Semmy Kiondo akiagana na Mkurugenzi wa TANAPA Allan Kijazi

Mkurugenzi wa TANAPA Allan Kijazi akiagana na wajumbe

KAMATI YA UTENDAJI YA APC YAPIGWA MSASA MAFUNZO YA UONGOZI NA NAMNA YA KUANZISHA SACCOS ILI KUSAIDIA WANACHAMA WAKE

Wajumbe wa kamati ya utendaji wakiwa kwenye mafunzo ya namna ya kuanzisha saccos nje kidogo ya mji wa Arusha hivi karibuni wa kwanza kushoto ni Claud Gwandu (Mwenyekiti), David Frank, Charles Ngereza, Janeth Mushi , Pamela Mollel, Swai(Afisa ushirika Mkoa wa Arusha), Mustafa Leu na Semmy Kiondo




Mwezeshaji wa mafunzo ya uongozi, Bill Mushi katikati mbele, akitoa maelezo muhimu ya namna ambavyo viongozi wanapaswa kuongoza katika mafunzo ya siku moja kwa kamati ya utendaji yaliyofanyika hivi karibuni nje kidogo ya mji wa Arusha

Mwezeshaji Bill Mushi akisisitiza jambo

wajumbe wakimsikiliza kwa makini mwezeshaji Bw.Bill Mushi

WAANDISHI WA HABARI ARUSHA WAHIMIZWA KUANDIKA HABARI ZA MAKALA

Washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za Makala wakimsikiliza kwa makini mwezeshaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Arusha, kutoka kulia mbele ni Janeth Mushi, Cynthia Mwilolezi na Abraham Gwandu

Washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za makala wakimsikiliza kwa makini mwezeshaji Evaristi Mwitumba(hayuko pichani), wa kwanza kulia ni Raymond Nyamwihula.


Washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za makala kutoka kushoto Claud Gwandu, Mohamed Isimbula na Angelo Mwoleka wakimsikiliza kwa makini mwezeshaji alipokuwa akifundisha somo hilo

Washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za Makala wakionekana kwa wingi katika picha



Washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za Makala wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa hoteli ya Olasiti Garden nje kidogo ya jiji la Arusha