Monday, November 18, 2013

MAHAKAMA ZA KIMATAIFA ZATAKIWA KUSHITAKI WAHALIFU MAHAKAMA YA AFRIKA

Na seif mangwangi, AICC, ARUSHA

MAHAKAMA za mataifa mbalimbali barani afrika  zimeshauriwa  kushirikiana na mahakama ya haki za binadamu barani afrika (AFCHPR)  yenye makao yake jijini Arusha,  kutafisiri na kuelewa ulinzi wa   haki za binadamu ambazo zimekuwa zikikiukwa katika mataifa mbalimbali.. 

Rai hiyo imetolewa leo na waziri mkuu, mizengo Pinda,,alipokuwa akifungua kongamano la kwanzala majaji  linalojadili kuwepo msingi imara wa kuteteanakulinda  la  haki za binadamu kutokana na ukiukwajiunaofanywa katika mataifa mbalimbali. 

Amesema kuwa kongamano hilolinaloshirikisha majaji ambao ni wakuu wa vyombo vya kutoa haki ndani ya nchi, mahakamaza kikanda ,mahakama ya afrika  na nje kuangaliajinsi wanavyoweza kushirikiana pamoja katika kuangalia swala zima la ulinzi nautetezi wa haki za binadamu.

 Pinda, amesema kuwa Tanzania iko msitari wa mbelekutekeleza na kulinda haki za binadamu na imeridhia mikata mbalimbali naitifaki(Protocal) mbalimbali ili kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa .

Amesema kuwa eneo ambalo halijapea  nafasi kubwa  ni wakati gain kunakuwepo na ukiukwaji  wa haki za binadamu ,mashirika au mtu mmoja mmoja  anaenda mahakamani kudai haki hizo  pindi zinapokiukwa.

Pinda amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 7 zilizoridhia kulindwa kwa haki za binadamu kati ya 26 barani afrika zilizosainimkataba wa kuanzishwa kwa mahakama ya afrika ambayo imetoa uhuru kwa mshirika yasiyokuwa ya kiserikali  kwenda mahakamani kudai  haki pale zinapokwa . 

Kwa upande wake Jaji mkuu Mohamed Othman  Chande, amesema kuwa kongamano hilo ni la kwanza  tangia kuanzishwa kwa mahakama ya afrika.

alisema katika kongamano hilo majaji mbalimbali majaji wamekutanishwa ikiwemo wa mahakama za kikanda na mahakama ya afrika na za kimataifa  na kwamba msingi mkubwa ukiwa ni kujadili namna ya majaji wanavyoweza kushirikiana  kutafisiri masharti ya haki za bindamu. 

Jaji, Chande amesema haki za binadamu zimekuwa zikilindwa katika katiba za mataifa mbalimbali  na kila mahakama ya nchi husika imekuwa ikizitafisiri  haki za binadamu kulingana na mazingira yake .

Amesema kuwa  kuna maamuzi ya kikanda kwa kila nchi , kimataifa ,ambapo kila mtu ana haki ya kuishi na haki hiyo ipo katika mikataba ambayo imeridhiwa na nchi 26 barani afrika ambapo Tanzania katika kutekeleza hilo imekubali mtu yeyote, kikundi chochote kwenda mahakamani kudai haki za binadamu pindi zikikiukwa.

 Awali rais wa mahakama ya afrika, Sophia Akufo, amesema ni lazima haki za jamii na watoto zilindwe.

Akasisitiza  kuwa ni muhimu kuzingatiwa kwa haki za binadamu na katiba za mataifa mbalimbali na zilindwe ili kudumisha utawala bora na wa kidemokrasia unaozingatia  sheria 

Amesema kuwa kongamano hilo linatoa mwelekeo na mtizamo  wa siku zijazo wa kuboresha utawala wa sheria na demokrasia ,uchumi na siasa nzuri zinazolinda haki za binadamu kulingana na mikataba na maazimio na matamko mbalimbali ya kimataifa kuhusu haki za binadamu.

No comments: