Tuesday, November 19, 2013

NYALANDU AJITOSA KUINUA VIPAJI VYA WANARIADHA SINGIDA, PIA NI KWAAJILI YA KUHAMASISHA KUPINGA UJANGILI

wanariadha wakiwa njiani kuelekea kumalizia mbio hizo 

Mkurugenzi wa Afrika Wildlife Fund, Pratik Patel akagana na mshindi wa kwanza katika mbio za nusu marathoni Paul Itambo baada ya kumkabidhi zawadi zake 

Mwanariadha, Fabiola William akimalizia mbio za Nusu Marathoni za Singida Marathoni na kuibuka mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake na kujinyakulia kitita cha Tsh300,000 na medali. mbio hizo ziliandaliwa na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu kwa lengo la kunyanyua vipaji vya vijana sanjari na kupambana na ujangili wa Tembo (PICHA NA SEIF MANGWANGI)


                                                                                                                                                             
Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo Paul Itambo akimaliza mbio za km21 
                                                                                                                                                                                                                          
Mmoja wa washiriki wa mbio za Singida Nusu Marathoni Philemon Tengu akikimbia bila kuwa na vifaa maalum vya kukimbilia ikiwemo viatu jana katika mbio hizo zilizoanzia katika kijiji cha mitula darajani na kumalizikia katika viwanja vya shule ya msingi Ntunduu. Mbio hizo ziliandaliwa na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyaladu zikiwa na lengo la kukuza vipaji vya wanariadha vijana na kupambana na ujangili wa tembo. (PICHA NA SEIF MANGWANGI)    NA SEIF MANGWANGI, SINGIDA
 
ZAIDI ya wakimbiaji 400 kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Singida juzi walishiriki mbio za kwanza za nusu marathoni Mkoani humo zikiwa na lengo kuu l

a kunyanyua vipaji vya wakimbiaji vijana sanjari na kuhamasisha vijana kwenye mapambano dhidi ya ujangili wa tembo nchini.
 
Katika mbio hizo zilizoandaliwa na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kwa upande wa wanaume,  mkimbiaji, Paul Itambo aliibuka kidedea kwa kukimbia kwa saa 1:10 na kuzawadiwa fedha Taslimu Tsh300,000, huku kwa upande wa wanawake Fabiola William aliishinda kwa kutumia saa1:53 na kuzawadiwa Tsh300,000.
 
Mbio hizo zilizoanzia katika kijiji cha Mitula Darajani na kuishia katika shule ya msingi Ntunduu, Singida Vijijini, Samuel Ikungi aliibuka mshindi wa tatu katika mashindano hayo na Emmanuel Samson alishinda nafasi ya tatu huku kwa upande wa wanawake, Winfrida Hassan aliibuka kidedea katika  nafasi ya pili na Zakhia Abdallah alishika nafasi ya tatu.
 
Kwa upande wa wanaume, mbio za kilometa tano Gabriel Galado aliibuka mshindi,  akifuatiwa na Deo Lazaro nafasi ya pili na Jonas John aliibuka nafasi ya tatu huku kwa wanawake Neema Kisunda aliibuka mshindi katika mbio hizo za kilometa tano akifuatiwa na Pascalia Sylvester.
 
Katika mbio za kilometa mbili na nusu upande wa wanawake, Julitha Anthony aliibuka mshindi akifuatiwa na Editha Gabriel na Margret Benado, huku upande wa wanaume Petro Pascal aliibuka mshindi akifuatiwa na Baraka Sebastian nafasi ya pili na Haji Swalehe alishika nafasi ya tatu.
 
Akizungumza kwa Niabu ya Naibu Waziri, Nyalandu, Mkurugenzi wa shirika la Afrika Wildlife Trust(AWT), ambae ni mwanzilishi wa matembezi ya kupinga ujangili wa tembo nchini katika matembezi aliyoyafanya kutoka Arusha hadi Dar es salaam, Pratic Patel aliwataka wazazi kuhamasisha vijana kushiriki kwenye mchezo wa riadha ili kuitagnaza Tanzania.
 
Pratik alisema Mkoa wa Singida umekuwa kinara wa mbio mbalimbli nchini hivyo ni wakati wa wazazi na wadau mbalimbali kuwekeza katika mchezo huo mkoani humo ili waweze kushiriki michuano mikubwa duniani na kuitangaza Tanzania kwa kuleta ushindi katika mbio watakazo shiriki.
 
“Riadha ni mchezo ambao utawapatia ajira vijana wengi hasa hapa Singida, ni wakati sasa kwa wazazi na wafadhili wengine kote nchini kujitokeza kudhamini riadha ili vijana watakaopatikana waweze kushiriki michuano mikubwa ulaya na kuiletea sifa Tanzania,”alisema.
 
Pratik alisema Tanzania imekuwa katika tishio la kupotea kwa wanyamapori maarufu ikiwemo Tembo hivyo vijana wanapaswa kuwa mabalozi wazuri wa kupingana na ujangili huo kwa kuwataja watu wanaohusika ili vyombo vya sheria viweze kuwachukulia hatua za kisheria.
Ends…

No comments: