Wednesday, May 14, 2014

MACHIFU 120 WAKUTANA ARUSHA KESHO, NI KWENYE TAMASHA LA UTAMADUNI LA 'MTU KWAO'

Chifu wa Kasulu Kigoma, Isambe Gilbert Isambe


Chifu wa Kasulu mkoani Kigoma Isambe G. Isambe wa kwanza kushoto, Chifu wa Old Moshi, Gerald Madara katikati na Mkurugenzi wa Utamaduni Training Janeth Jonas kulia wakizungumza na waandishi wa habari jana

Chifu wa Kasulu mkoani Kigoma Isambe G. Isambe wa kwanza kushoto, Chifu wa Old Moshi, Gerald Madara

Chifu wa Kasulu, Kigoma Isambe G Isambe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo kuhusu tamasha la utamaduni linaloanza kesho jijini Arusha, kulia ni Mkurugenzi wa Utamaduni Training Ltd


Na Seif Mangwangi, Arusha

TAMASHA kubwa la utamaduni linalokutanisha zaidi ya machifu 120 wa kabila mbalimbali nchini, linaanza leo katika uwanja wa mpira wa miguu wa Shekh Amri Abeid jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana  jijini hapa, Mkurugenzi  wa kampuni ya  Utamaduni Training, Janeth Jonas alisema tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza nchini likiwa na lengo la kuenzi utamaduni wa Mtanzania kwa vizazi vilivyopo.

Chifu wa Kasulu Kigoma Isambe G Isambe akiwa katika vazi la kitamaduni la jamii yake
Alisema katika tamasha hilo la siku tano linalotambulika kwa jina la ‘MTU KWAO’, washiriki zaidi ya 10,000 wanatarajiwa kushiriki ambapo shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwemo kuonyesha mavazi, ngoma za asili za makabila hayo na elimu ya tamaduni zao.
Janeth alisema wasanii mbalimbali watakuwepo kutumbuiza katika tamasha hilo ikiwemo Mrisho Mpoto, Jambo Squard, Dogo Janja, Wema Sepetu, Roma Mkatoliki,Weusi na  Daniel Sekuo kutokana nchini Kenya.

“Mbali ya wasanii hawa pia kutakuwa na ngoma za asili kwa kila kabila ikiwemo ngoma ya Mtingo kutoka Moshi, Hadzabe, Maasai, Datoga n.k, lakini pia kutakuwa na tamaduni mbalimbali zitakazoonyeshwa,”alisema.

Alisema siku ya mwisho ya kilele cha Tamasha hilo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti ambae pia ni Chifu katika jamii yake anatarajiwa kuwa mgeni rasmi ambapo shughuli mbalimbali pia zitafanyika.

Kwa upande wake chifu kutoka wilaya ya Kasulu,  Mkoa wa Kigoma, Isambe Isambi alisema Tamasha hilo linafanyika ikiwa ni kukumbusha watanzania utamaduni wao ambapo miongoni mwa shughuli zitakazofanyika ni pamoja na kutoa elimu ya tamaduni ambazo zinaweza kuendelea kuenziwa na kuondoa ambazo zimepitwa na wakati.


Saturday, May 3, 2014

WAANDISHI WA HABARI WANA NAFASI KUBWA YA KUPAMBANA NA UJANGILI - SHELUTETE

MENEJA MAWASILIANO WA SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) PASCAL SHELUTETE AKITOA SALAMU ZA MKURUGENZI WA SHIRIKA HILO KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUANIANI, KATIKA UKUMBI WAMIKUTANO WA AICC, JIJINI ARUSHA LEO
VIONGOZI MBALIMBALI WAKIWA MEZA KUU WAKATI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI, WA PILI KUTOKA KULIA NI RAIS WA UTPC KENNY SIMBAYA, MKURUGENZI WA MISA-TANZANIA NA JAJI MSTAAFU MACK BOMANI

WASHIRIKI WAKIMSIKILIZA MWAKILISHI WA TANAPA ALIPOKUWA AKITOA SALAMU ZA SHIRIKA HILO 

WAANDISHI WAKIFUATILI SALAMU KUTOKA KWA WADAU MBALIMBALI IKIWEMO TANAPA 


WAANDISHI WAKOGWE WAKIONGOZWA NA EDA SANGA WA KWANZA KUSHOTO WAKIFUATIA HOTUBA ILIYOKUWA IKITOLEWA NA WAWAKILISHI WA MASHIRIKA YA TANAPA NA NCAA
MENEJA MAWASILIANO WA TANAPA, PASCAL SHELUTETE AKITOA SALAMU ZA TANAPA 
NA MWANDISHI WETU, ARUSHA

WAANDISHI wa habari wameelezwa kuwa na nafasi kubwa ya kuzuia matukio ya ujangili yanayoendelea kwa kasi nchini jambo ambalo linaweza kuathiri shughuli mbalimbali za maendeleo ya Taifa kutokana na pato linalopatikana kutokana na sekta hiyo.

Wito huo umetolewa leo jijini hapa na Mkurugenzi wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi katika salamu zake zilizowasilishwa kwa niaba yake na Meneja mawasiliano wa shirika hilo Pascal Shelutete katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani.

Shelutete alisema ujangili umekuwa ni jambo ambalo linapaswa kupingwa na kila mtanzania katika sekta aliyokuwepo badala ya kuiachia Tanapa kwa kuwa hifadhi za Taifa zimekuwa zikiliingizia Serikali mapato mengi ambayo yamekuwa yakitumika kwenye shughuli za maendeleo.

“Waandishi wa habari naombeni muungane na Tanapa na serikali kwa ujumla kupambana na vita dhidi ya ujangili, tunajua nguvu ambayo mmekuwa nayo kupitia kalamu zenu, hii ni vita mbaya kwa kuwa inahatarisha uhai wa nchi,”alisema Shelutete.

Alisema mchango wa waandishi wa habari unaotikana na uandishi mzuri kuhusu hifadhi za Taifa umekuwa ukionekana kutokana na wageni wengi kufika nchini kutembelea hifadhi hizo na kuiingizia Serikali mapato mengi

Shelutete alitoa wito kwa waandishi kuendelea kuandika taarifa mbalimbali za hifadhi za Taifa ili kuvutia zaidi wageni kuja nchini na kwamba shirika hilo litaendelea kushirikiana na waandishi wa habari.

Kwa upande wake, Meneja mawasiliano wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, Adam Akyoo alisema tunaposherehekea siku ya uhuru wa vyombo vya habari ni wakati wa kutathmini visa na mikasa ambayo waandishi wamekuwa wakikabiliana nayo.

Alitoa wito kwa mamlaka za Serikali kuheshimu tasnia ya uandishi wa habari kwa kutoa sheria nzuri na ambayo itaweza kueleza maudhuni mazuri ya tasnia hiyo nchini.

Ends… 

SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI YAFANYIKA KITAIFA ARUSHA KWA WADAU KUTOA HOJA MOTOMOTO

MTANGAZAJI WA KITUO CHA REDIO CHA RADIO 5 DAVID RWENYAGIRA AKISIKILIZA KWA MAKINI MADA ZILIZOKUWA ZIKIWASILISHWA, PEMBENI YAKE NI MWENYEKITI WA IRINGA PRESS CLUB, FRANK LEONARD

MKURUGENZI WA UTPC ABUBAKAR KARSAN AKISIKILIZA KWA MAKINI MADA MBALIMBALI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI, AICC ARUSHA 

MWAKILISHI WA ITV JIJINI MWANZA MABERE MAKUBI AKISILIZA USHUHUDA WA HABARI YA UCHUNGUZI KUTOKA KWA FREDRICK KATULANDA (HAYUPO PICHANI)MSANIFU KURASA WA GAZETI LA MWANANCHI, DANNY MWAIJENGA AKISIKILIZA KWA MAKINI


MWAKILISHI WA ITV MANYARA, CHARLES MASAYANYIKA AKISILIZA KWA MAKINI MADA ZILIZOKUWA ZIKIWASILISHWA

MTANGAZAJI MKONGWE NCHINI MASUD MASUD (KATIKATI) AKISILIZA KWA MAKINI

MKUFUNZI WA CHUO KIKUU CHA TUMAINI IRINGA, SAIMON BEREGE NA MWANAHABARI MKONGWE AKIWASILISHA MADA KATIKA MAADHIMISHO HAYO


MMOJA WA WAKURUGENZI WA KAMPUNI YA MWANANCHI COMMUNICATION, THEOPHIL MAKUNGA WA KWANZA KULIA AKIFUATILIA KWA MAKINI MJADALA ULIOKUWA UKIENDELEA KATIKA MAAZIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI ILIYOFANYIKA KITAIFA JIJINI ARUSHA

Saturday, April 12, 2014

MAFURIKO MAGARI NGORONGORO YAKWAMA

Dereva wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro akiwa juu ya mti baada ya gari alilokuwa anaendesha kusombwa na maji katika eneo la Melela wilayani Karatu juzi

Na Mwandishi Wetu, Karatu

Dereva wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) mkoani Arusha, Juma Moshi, amenusurika kufa maji baada ya gari alilokuwa akiliendesha kusombwa na mafuriko katika mto Malera uliopo nje kidogo ya mji wa Karatu kwa kupanda juu ya mti.

Juma alilazimika kutoka kwenye gari hilo aina ya Toyota Land Cruizer SU 36037 lililokuwa limesombwa na mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha kwa umbali wa mita zipatazo 70 kutoka barabarani,  alfajiri jana na kujiokoa kwa kupanda juu ya mti wakati akienda mjini Arusha kikazi.

Mkuu wa Idara ya Huduma ya Uhandisi wa NCAA, Isra Missana na wafanyakazi wengine wa mamlaka hiyo wakishirikiana na wakazi jirani wa eneo hilo, walimwokoa dereva huyo saa 12:30 asubuhi.

Nao mamia ya wasafiri waliokuwa wakitoka maeneo ya Karatu na watalii  Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwenda mjini Arusha, Dar es Salaam na maeneo mengine nchini jana walikwama kwa muda kuvuka Mto Kirurumo uliokuwa umefurika maji hadi kupita juu ya barabara huku ukiporomosha mawe makubwa kutoka milima ya Mbulumbulu.

Mto huo upo mpakani mwa Wilaya za Monduli na Karatu. Miongoni mwa abiria ni waliokuwa wasafiri kwa mabasi ya Dar Express na Sai Baba kwenda Dar es Salaam.

Pia mamia ya magari yaliyokuwa yakiwasafirisha watalii kutoka hifadhi za taifa yalikuwa miongoni mwa magari mengine mengi yaliyokwama katika eneo hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Felix Ntibenda, akizungumza katika eneo la tukio hilo alisema tatizo la mafuriko katika mto huo limekuwa likijirudia mara kwa mara na serikali inafanya utafiti wa kutafuta ufumbuzi wa kudumu.

BILIONEA WA KIMAREKANI HOWARD G. BUFFET AAHIDI MAKUBWA VITA DHIDI YA UJANGILI NCHINI

Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Pasiansi, kulia ni Bilionea wa Kimarekani Howard G Buffet

Waziri Nyalandu pamoja na Bilionea Buffet wakisalimiana na wafanyakazi wa chuo cha Pasiansi, Mwanza

Bilionea wa Kimarekani Howard G Buffet akipanda mti katika chuo cha  Wanyamapori cha Pasiansi


Bilionea wa Kimarekani Howard Buffet akisalimiana na mkuu wa idara ya mafunzo chuo cha Wanyamapori Pasiansi, Venance Tossi alipotembelea chuo hicho jana

Bilionea wa Kimarekani akipanda mti

Askari walioko kwenye mafunzo katika chuo cha Wanyamapori cha Pasiansi wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu

Waziri Nyalandu na Bilionea wa Kimarekani Buffet wakikagua gwaride la askari wanafunzi wa chuo cha wanyamapori cha Pasiansi

Tajiri duniani wa kimarekani Buffet pamoja na waziri Nyalandu wakiwa kwenye jukwaa ndani ya chuo cha wanyamapori cha Pasiansi ulipokuwa ukipigwa wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kukagua gwaride la askari wanafunzi chuoni hapo

Tuesday, April 1, 2014

WADAU WA VOLLEYBALL WATAKIWA KUANZISHA CHAMA ILI KUTAMBULIKA


Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela katikati akipiga mpira kuashiria ufunguzi wa uwanja wa wavu uliopo katika bustani ya Pentagoni Suye jijini Arusha, wa kwanza kushoto ni mratibu wa klabu hiyo

Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela akirusha juu mpira kupiga ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa uwanja wa mpira wa wavu ulioenda sanjari na bonanza la mpira huo ulioshirikisha timu kutoka kanda ya Kaskazini. wa sita mbele ni mmiliki wa bustani ya Pentagon Estomii Mallah 

wachezaji wa Mbulu wakijaribu kuzuia mashambulizi kutoka kwa wachezaji wa timu ya Hai

Wachezaji wa tiimu za Hai na Mbulu wakichuana vikali katika fainali baada ya mchezo wa wavu katika bustani ya pentagon, hata hivyo timu ya Hai iliibuka kidedea kwa seti tatu, huku mbulu ikiambulia patupu

Mmoja wa wachezaji wa timu ya Hai kutoka mkoani Kilimanjaro, katikati akiwa juu baada ya kupiga mpira kuelekeza mashambulizi upande wa timu ya Mbulu . Mashindano hayo yaliyoshirikisha timu 20, timu ya Hai iliibuka kidedea.

NA SEIF MANGWANGI

UONGOZI wa Taifa wa chama cha mpira wa wavu nchini(TAVA) umewataka wadau wa mchezo huo Mkoa wa Arusha kutafuta uongozi utakaosaidia kuwezesha uwepo wa klabu mbalimbali za mchezo huo jijini Arusha na ambao utakuwa ukiratibu shughuli mbalimbali za mchezo huo ndani na nje ya Arusha.

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa kamati ya makocha wa mchezo huo  na Kaimu Mwenyekiti wa TAVA Taifa Emanuel Majengo mbele ya mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela katika fainali za mchezo huo ulioambatana na ufunguzi wa uwanja wa mchezo huo katika bustani ya Pentagoni jijini hapa.

Majengo alisema kwa muda mrefu chama chake kimekuwa kikihaha kuushirikisha mkoa wa Arusha katika michuano mbalimbali ya mchezo huo kutokana na kukosekana kwa uongozi jambo ambalo linautia aibu mkoa mkubwa kama wa Arusha.

Alimshauri Mongela kusimamia jambo hilo ili kupatikane hata uongozi wa muda mfupi utakaowezesha mkoa huo kushiriki hata katika michezo ya Muungano na mingine mingi inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Katika uzinduzi huo timu 20 zilishiriki na kufikia hatua ya nusu fainali na fainali ambapo timu ya Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro iliibuka mshindi kwa kuifunga timu ya Mbulu mkoani Manyara kwa seti tatu kwa bila.

Katika hatua ya nusu fainali timu ya Mbulu iliitoa timu ya KCMC ya Moshi kwa kuifunga kwa seti tatu kwa bila wakati timu ya Hai iliingia fainali kwa kuibugiza timu ya Ngorongoro kwa seti nne kwa moja.

Akizungumza wakati wa shukurani mmiliki wa uwanja huo Estomii Mallah alisema lengo la kuanzisha kwa bonanza hilo haikuwa kumpaya mshindi wala vikombe bali ilikua ni kuwaunganisha wanafamili wa mchezo huo katika kanda ya kaskazini ili kukuza mchezo huo.

Alisema hata hivyo kumukuwa na mwamko mkubwa kwa wanafamilia wa mchezo huo hususani mashuleni na vyuoni hadi kufikia kujichanga na kuwezesha kujengwa kwa uwanja huo kupitia michango yao mbalimbali.

Awali mratibu wa bonanza hilo Willium Nkanga alieleza kuwa mchezo huo mkoani Arusha unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa vifaa,viwanja,vyama na viongozi wa michezo hiyo,wanamichezo,timu pamoja na wafadhili wa michezo hiyo.

Aidha alisema ujenzi wa uwanja huo mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 80 pekee hali ambayo bado inawahitaji kupata fedha kwaajili ya kukamilisha kwa kutegemea michango toka kwa wadau na wanafamilia wa mchezo huo.

Nae Mongela alipongeza hatua za mmiliki huyo kujitolea eneo la ujenzi wa uwanja huo pamoja na wanafamilia wa mchezo huo kwa kujitolea kuanzisha kwa juhudi za mchezo huo mkoani Arusha na kuahidi kwaunga mkono.

Aidha aliahidi kuundwa kwa uongozi wa muda na kuanzishwa kwa chama hicho haraka iwezekanavyo mkoani hapa kama njia ya kutafuta mwelekeo wa kuwepo kwa uongozi wa kudumu na timu za mchezo huo.

Alisema ni aibu kwa mkoa mkubwa kama Arusha kukosa chama,viongozi na hata timu zinazoweza kuuwakilisha mkoa katika michuano mbalimbali ya mchezo huo na kuagiza jiji la Arusha kwa kuanzia kuanzisha timu itakayoweza kushiriki michuano ya hivi karibuni.

Pia Mongela alikubali kuwa mlezi wa kilabu hiyo kama njia ya kukuza mchezo huo mkoani Arusha pamoja na kutoa kiasi cha shilingi 500,000 taslimu kama mchango wake katika kukamilisha ujenzi wa uwanja huo.


NCAA YAKABIDHIWA VITUO VYA MAMBO YA KALE VYA OLTUPAI NA LAITOLIE

John Kimaro (kushoto) akimkabidhi hati ya makabidhiano ya vituo vya Oltupai na Laitole kwa mhifadhi wa Ngorongoro Dkt.Fred Manongi kwa ajili ya kuvisimamia. Aliyesimama katikati na kupiga makofi ni meneja mawasiliano wa Mamlaka hiyo Adam Akyoo.

John Kimaro akisaini hati ya kukikabidhi vituo vya Laitole na Oltupai kwa uongozi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA)

Uongozi wa kituo cha mambo ya kale cha Oltupai pamoja na uongozi wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wakiwa katika picha ya pamoja 

TANAPA YAKAMATA MAJANGILI 6, NA MENO 53 YA TEMBOWaziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akizungumza na waandishi wa habari jana katika hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha 
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu (Hayupo Pichani)

Msemaji wa Shirika la Hifadhi za Taifa Pascal Shelutete akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akimkaribisha waziri Lazaro Nyalandu jana.


NA SEIF MANGWANGI, ARUSHA

KIKOSI kazi cha shirika la hifadhi ya wanyamapori (TANAPA) kwa kushirikiana na makachero wa jeshi la Polisi wilaya ya Manyoni mkoani Singida, wamefanikiwa kukamata majangili sita pamoja na  meno 53 ya tembo yenye jumla ya kilo 169.7 na silaha moja ya kivita aina ya SMG na magazine tatu.a

waandishi wa habari wakimsikiliza waziri Nyalandu kutoka kulia
ni Shechelela Kongola(TBC), Mwanaidi Mkwizu (ITV) na
Abraham Gwandu (RAI)
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Waziri wa utalii na Maliasili Lazaro Nyalandu alisema tukio hilo lilitokea juzi katika kijiji cha kiombo Wilaya ya manyoni ambapo tembo 26 wameuwawa na majangili katika maeneo ya hifadhi za Rungwa na Kizigo

Akizungumzia mazingira ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambao serikali inawasaka kwa udi na uvumba, Waziri Nyalandu alisema taarifa mbalimbali za kiintelejensia ndizo zilizofanikisha kukamatwa kwa watu hao pamoja na idadi hiyo ya meno.

'Majangili 6 wameshikiliwa chini ya ulinzi mkali katika kituo cha polisi cha Manyoni ambapo walikutwa na meno ya tembo 53,silaha ya kivita moja na magazine tatu, hawa ni watu hatari sana ambao Serikali imekuwa ikiwasaka kila kukicha,"alisema Nyalandu.

 Nyalandu alisisitiza kuwa pamoja na changamoto kubwa iliyopo dhidi ya ujangili, serikali imeazimia kuwasaka na kuwakamata majangili na washirika wao popote walipo na kwamba zoezi la kuwasaka ni la usiku na mchana

 Aidha alisema kuwa msako unaendelea kuwasaka wauaji wa tembo 26, huku akiwaomba wananchi wenye taarifa kuhusu uhalifu watoe ushirikiano wao kwa askari wa wanyamapori,jeshi la polisi na vyombo vya usalama


Nyalandu alitoa pongezi zake kwa mkurugenzi wa wanyamapori na kikosi chake dhidi ya ujangili kanda ya kati Manyoni na kikosi kazi maalum(Task force)kwa weledi na kujituma kwao ambapo imefanikisha kukamatwa majangili hao na meno ya tembo

TANAPA YAKANUSHA 'KATAVI' KUUZWA


Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal Shelutete akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha
                        TAARIFA KWA UMMA
Katika gazeti la Jamhuri Toleo Namba 129 Machi 25-31, 2014 kulikuwa na habari iliyoandikwa chini ya kichwa cha habari “Nyalandu ‘auza’ Hifadhi” ambapo maelezo ya habari hiyo yaliitaja Hifadhi ya
Taifa ya Katavi kuwa inatarajiwa kukabidhiwa kwa wawekezaji kutoka nchini Afrika Kusini ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe…. Lazaro Nyalandu.

Shirika la Hifadhi za Taifa linalosimamia Hifadhi ya Taifa ya Katavi pamoja na Hifadhi nyingine 15 nchi nzima linapenda kukanusha habari hiyo iliyoandikwa kwa lengo la kupotosha umma kama ifuatavyo.

Mosi, hakuna mpango wala uamuzi wowote uliopo au uliokwisha kufanywa wa kuingia Mkataba
wa Uendeshaji wa aina yoyote ile baina ya Shirika la Hifadhi za Taifa naMwekezaji yeyote kutoka nchini Afrika ya Kusini ikiwa ni pamoja na African Parks Network waliotajwa katika habari husika.

Pili, Sheria inayosimamia uanzishwaji wa maeneo ya Hifadhi za Taifa ikiwemo Katavi imelipa dhamana hii pekee shirika kusimamia maeneo haya kwa niaba ya Watanzania na ni kinyume cha sheria kukabidhi kwa wawekezaji kwa ajili ya usimamizi kama ilivyobainishwa katika habari hiyo.

Tatu, Shirika la Hifadhi za Taifa bado linao uwezo thabiti wa kusimamia uendeshaji wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi ili kuhakikisha rasilimali za wanyama na mimea zinaendelea kutunzwa kwa miaka mingi ijayo kama ambavyo imekuwa ikifanya tangu kuanzishwa kwa hifadhi hiyo mwaka 1974.

Aidha, kama ambavyo shirika limekuwa likipanga katika mipango yake ya maendeleo mwaka hadi mwaka, katika mwaka mpya wa fedha ujao shirika limepanga kuongeza idadi ya watalii katika Hifadhi za Kusini ikiwemo Katavi,Saadani,Mikumi na Ruaha.

 Mkakati huu utahusisha kuongeza ubora wa utoaji huduma ikiwa ni pamoja na malazi ili kukuza utalii wa ndani. Shirika litafungua ofisi Jijini Dar es Salaam na kuimarisha ofisi za Mwanza na Iringa ili watalii wapate taarifa za Hifadhi na kuweza kufanya
‘bookings’ kwa urahisi. Aidha, kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa masoko ya nje, Shirika sasa litaanzisha ‘Road shows’ mbalimbali kwa soko la ndani na nchi za jirani. Vilevile, Shirika litaongeza kujitangaza kupitia Mitandao ya Jamii, TV, majarida na tovuti ya Shirika itaboreshwa katika kuarifu wadau masuala mbalimbali yanayojiri kwenye Hifadhi zetu.

Tayari Shirika limeanzisha Kurugenzi mpya ya Utalii na Masoko kwa ajili ya kutekeleza mkakati huu wa kuzifanya hifadhi za ukanda wa kusini kuvutia watalii wengi zaidi.
Imetolewa  na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania
30.03.2014

Wednesday, March 26, 2014

MUAMKO JUU YA ULINZI SHIRIKISHI WASHIKA KASI ARUSHA TAARIFA ZAIDI ZA UHALIFU ZATOLEWA


Na Rashid NchimbiwaJeshi la PolisiArusha

Wananchi Mkoani hapa wameonekana kuwa na muamko zaidi wa Ulinzi Shirikishi baada ya kutoa taarifa mbili zilizofanikisha kukamata misokoto 1,038 ya madawa ya kulevya aina ya bangi pamoja na mirungi kilogramu 75.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisi kwake, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Gilles Muroto alisema kwamba katika matukio mawili yaliyofanikisha ukamataji wa madawa hayo taarifa zake zilitolewa na raia wema.

Kaimu Kamanda Muroto alisema kwamba, tukio la kwanza lilitokea tarehe 18.02.2014 muda wa saa 1:30 asubuhi maeneo ya Kituo Kikuu cha mabasi jijini hapa ambapo mtu mmoja aitwaye Charles Ogaga Ayunga (38) raia wa Kenya nani mkazi wa Taveta nchini humo, alikamatwa na misokoto 1,038 ya Madawa ya kulevya aina ya bangi iliyokuwa ndani ya boksi.

Akifafanua taarifa hiyo Kaimu Kamanda huyo alisema kwamba, siku ya tukio mtuhumiwa alikuwa anatokea maeneo ya Ngaramtoni akiwa kwenye Hiace na alipofika maeneo ya Kituo Kikuu cha Mabasi alishuka akiwa na boksi na kutaka kupanda basi linaloelekea Holili wilayani Rombo lakini kabla hajapandisha boksi hilo kwenye basi hilo watu walimshuku na kutoa taarifa katika kituo kikuu cha Polisi, ambapo askari waliokuwa doria maeneo ya karibu walikwenda katika maeneo hayo na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa misokoto hiyo.

Mara baada ya mahojiano mtuhumiwa alikiri kuumiliki madawa hayo ya kulevya aina ya bangi na kueleza kwamba alikuwa anasafirisha kupeleka nchini Kenya.

Wakati huo huo mtu mmoja aitwaye Philipo Santolin (25) Mkazi wa Holili wilayani Rombo alikamatwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi yenye uzito wa kilogramu 75 ambayo ilikuwa imehifadhiwa kwenye vifurushi tofauti tofauti 7.

Akifafanua tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Gilles Muroto alisema tukio hilo la ukamataji lilitokea tarehe 19/02/2014 muda wa saa 2:00 usiku maeneo ya Kaloleni jijini hapa.

Alisema siku ya tukio wananchi walitoa taarifa katika kituo kikuu cha Polisi kwamba, kuna mtu alikuwa anasafirisha madawa hayo katika gari aina ya Corolla lenye namba za usajili T 162 AYW toka mkoani Kilimanjaro kuja Arusha, ndipo askari walipoweka mtego maeneo ya Kwa Mrefu na mara baada ya gari hilo kusimamishwa halikusimama ndipo askari wa kaamua kulifuatilia ambapo walifanikiwa kulikamata maeneo ya Kaloleni mara baada ya gari hilo la mtuhumiwa kupasuka tairi la mbele.

Kaimu Kamanda Muroto alisema mpaka hivi sasa watuhumiwa wote wawili wanahojiwa na watafikishwa makamani mara baada ya upelelezi kukamilika.