Wednesday, May 14, 2014

MACHIFU 120 WAKUTANA ARUSHA KESHO, NI KWENYE TAMASHA LA UTAMADUNI LA 'MTU KWAO'

Chifu wa Kasulu Kigoma, Isambe Gilbert Isambe


Chifu wa Kasulu mkoani Kigoma Isambe G. Isambe wa kwanza kushoto, Chifu wa Old Moshi, Gerald Madara katikati na Mkurugenzi wa Utamaduni Training Janeth Jonas kulia wakizungumza na waandishi wa habari jana

Chifu wa Kasulu mkoani Kigoma Isambe G. Isambe wa kwanza kushoto, Chifu wa Old Moshi, Gerald Madara

Chifu wa Kasulu, Kigoma Isambe G Isambe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo kuhusu tamasha la utamaduni linaloanza kesho jijini Arusha, kulia ni Mkurugenzi wa Utamaduni Training Ltd


Na Seif Mangwangi, Arusha

TAMASHA kubwa la utamaduni linalokutanisha zaidi ya machifu 120 wa kabila mbalimbali nchini, linaanza leo katika uwanja wa mpira wa miguu wa Shekh Amri Abeid jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana  jijini hapa, Mkurugenzi  wa kampuni ya  Utamaduni Training, Janeth Jonas alisema tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza nchini likiwa na lengo la kuenzi utamaduni wa Mtanzania kwa vizazi vilivyopo.

Chifu wa Kasulu Kigoma Isambe G Isambe akiwa katika vazi la kitamaduni la jamii yake
Alisema katika tamasha hilo la siku tano linalotambulika kwa jina la ‘MTU KWAO’, washiriki zaidi ya 10,000 wanatarajiwa kushiriki ambapo shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwemo kuonyesha mavazi, ngoma za asili za makabila hayo na elimu ya tamaduni zao.
Janeth alisema wasanii mbalimbali watakuwepo kutumbuiza katika tamasha hilo ikiwemo Mrisho Mpoto, Jambo Squard, Dogo Janja, Wema Sepetu, Roma Mkatoliki,Weusi na  Daniel Sekuo kutokana nchini Kenya.

“Mbali ya wasanii hawa pia kutakuwa na ngoma za asili kwa kila kabila ikiwemo ngoma ya Mtingo kutoka Moshi, Hadzabe, Maasai, Datoga n.k, lakini pia kutakuwa na tamaduni mbalimbali zitakazoonyeshwa,”alisema.

Alisema siku ya mwisho ya kilele cha Tamasha hilo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti ambae pia ni Chifu katika jamii yake anatarajiwa kuwa mgeni rasmi ambapo shughuli mbalimbali pia zitafanyika.

Kwa upande wake chifu kutoka wilaya ya Kasulu,  Mkoa wa Kigoma, Isambe Isambi alisema Tamasha hilo linafanyika ikiwa ni kukumbusha watanzania utamaduni wao ambapo miongoni mwa shughuli zitakazofanyika ni pamoja na kutoa elimu ya tamaduni ambazo zinaweza kuendelea kuenziwa na kuondoa ambazo zimepitwa na wakati.


Saturday, May 3, 2014

WAANDISHI WA HABARI WANA NAFASI KUBWA YA KUPAMBANA NA UJANGILI - SHELUTETE

MENEJA MAWASILIANO WA SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) PASCAL SHELUTETE AKITOA SALAMU ZA MKURUGENZI WA SHIRIKA HILO KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUANIANI, KATIKA UKUMBI WAMIKUTANO WA AICC, JIJINI ARUSHA LEO
VIONGOZI MBALIMBALI WAKIWA MEZA KUU WAKATI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI, WA PILI KUTOKA KULIA NI RAIS WA UTPC KENNY SIMBAYA, MKURUGENZI WA MISA-TANZANIA NA JAJI MSTAAFU MACK BOMANI

WASHIRIKI WAKIMSIKILIZA MWAKILISHI WA TANAPA ALIPOKUWA AKITOA SALAMU ZA SHIRIKA HILO 

WAANDISHI WAKIFUATILI SALAMU KUTOKA KWA WADAU MBALIMBALI IKIWEMO TANAPA 


WAANDISHI WAKOGWE WAKIONGOZWA NA EDA SANGA WA KWANZA KUSHOTO WAKIFUATIA HOTUBA ILIYOKUWA IKITOLEWA NA WAWAKILISHI WA MASHIRIKA YA TANAPA NA NCAA
MENEJA MAWASILIANO WA TANAPA, PASCAL SHELUTETE AKITOA SALAMU ZA TANAPA 
NA MWANDISHI WETU, ARUSHA

WAANDISHI wa habari wameelezwa kuwa na nafasi kubwa ya kuzuia matukio ya ujangili yanayoendelea kwa kasi nchini jambo ambalo linaweza kuathiri shughuli mbalimbali za maendeleo ya Taifa kutokana na pato linalopatikana kutokana na sekta hiyo.

Wito huo umetolewa leo jijini hapa na Mkurugenzi wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi katika salamu zake zilizowasilishwa kwa niaba yake na Meneja mawasiliano wa shirika hilo Pascal Shelutete katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani.

Shelutete alisema ujangili umekuwa ni jambo ambalo linapaswa kupingwa na kila mtanzania katika sekta aliyokuwepo badala ya kuiachia Tanapa kwa kuwa hifadhi za Taifa zimekuwa zikiliingizia Serikali mapato mengi ambayo yamekuwa yakitumika kwenye shughuli za maendeleo.

“Waandishi wa habari naombeni muungane na Tanapa na serikali kwa ujumla kupambana na vita dhidi ya ujangili, tunajua nguvu ambayo mmekuwa nayo kupitia kalamu zenu, hii ni vita mbaya kwa kuwa inahatarisha uhai wa nchi,”alisema Shelutete.

Alisema mchango wa waandishi wa habari unaotikana na uandishi mzuri kuhusu hifadhi za Taifa umekuwa ukionekana kutokana na wageni wengi kufika nchini kutembelea hifadhi hizo na kuiingizia Serikali mapato mengi

Shelutete alitoa wito kwa waandishi kuendelea kuandika taarifa mbalimbali za hifadhi za Taifa ili kuvutia zaidi wageni kuja nchini na kwamba shirika hilo litaendelea kushirikiana na waandishi wa habari.

Kwa upande wake, Meneja mawasiliano wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, Adam Akyoo alisema tunaposherehekea siku ya uhuru wa vyombo vya habari ni wakati wa kutathmini visa na mikasa ambayo waandishi wamekuwa wakikabiliana nayo.

Alitoa wito kwa mamlaka za Serikali kuheshimu tasnia ya uandishi wa habari kwa kutoa sheria nzuri na ambayo itaweza kueleza maudhuni mazuri ya tasnia hiyo nchini.

Ends… 

SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI YAFANYIKA KITAIFA ARUSHA KWA WADAU KUTOA HOJA MOTOMOTO

MTANGAZAJI WA KITUO CHA REDIO CHA RADIO 5 DAVID RWENYAGIRA AKISIKILIZA KWA MAKINI MADA ZILIZOKUWA ZIKIWASILISHWA, PEMBENI YAKE NI MWENYEKITI WA IRINGA PRESS CLUB, FRANK LEONARD

MKURUGENZI WA UTPC ABUBAKAR KARSAN AKISIKILIZA KWA MAKINI MADA MBALIMBALI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI, AICC ARUSHA 

MWAKILISHI WA ITV JIJINI MWANZA MABERE MAKUBI AKISILIZA USHUHUDA WA HABARI YA UCHUNGUZI KUTOKA KWA FREDRICK KATULANDA (HAYUPO PICHANI)MSANIFU KURASA WA GAZETI LA MWANANCHI, DANNY MWAIJENGA AKISIKILIZA KWA MAKINI


MWAKILISHI WA ITV MANYARA, CHARLES MASAYANYIKA AKISILIZA KWA MAKINI MADA ZILIZOKUWA ZIKIWASILISHWA

MTANGAZAJI MKONGWE NCHINI MASUD MASUD (KATIKATI) AKISILIZA KWA MAKINI

MKUFUNZI WA CHUO KIKUU CHA TUMAINI IRINGA, SAIMON BEREGE NA MWANAHABARI MKONGWE AKIWASILISHA MADA KATIKA MAADHIMISHO HAYO


MMOJA WA WAKURUGENZI WA KAMPUNI YA MWANANCHI COMMUNICATION, THEOPHIL MAKUNGA WA KWANZA KULIA AKIFUATILIA KWA MAKINI MJADALA ULIOKUWA UKIENDELEA KATIKA MAAZIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI ILIYOFANYIKA KITAIFA JIJINI ARUSHA