Saturday, May 3, 2014

WAANDISHI WA HABARI WANA NAFASI KUBWA YA KUPAMBANA NA UJANGILI - SHELUTETE

MENEJA MAWASILIANO WA SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) PASCAL SHELUTETE AKITOA SALAMU ZA MKURUGENZI WA SHIRIKA HILO KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUANIANI, KATIKA UKUMBI WAMIKUTANO WA AICC, JIJINI ARUSHA LEO
VIONGOZI MBALIMBALI WAKIWA MEZA KUU WAKATI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI, WA PILI KUTOKA KULIA NI RAIS WA UTPC KENNY SIMBAYA, MKURUGENZI WA MISA-TANZANIA NA JAJI MSTAAFU MACK BOMANI

WASHIRIKI WAKIMSIKILIZA MWAKILISHI WA TANAPA ALIPOKUWA AKITOA SALAMU ZA SHIRIKA HILO 

WAANDISHI WAKIFUATILI SALAMU KUTOKA KWA WADAU MBALIMBALI IKIWEMO TANAPA 


WAANDISHI WAKOGWE WAKIONGOZWA NA EDA SANGA WA KWANZA KUSHOTO WAKIFUATIA HOTUBA ILIYOKUWA IKITOLEWA NA WAWAKILISHI WA MASHIRIKA YA TANAPA NA NCAA
MENEJA MAWASILIANO WA TANAPA, PASCAL SHELUTETE AKITOA SALAMU ZA TANAPA 
NA MWANDISHI WETU, ARUSHA

WAANDISHI wa habari wameelezwa kuwa na nafasi kubwa ya kuzuia matukio ya ujangili yanayoendelea kwa kasi nchini jambo ambalo linaweza kuathiri shughuli mbalimbali za maendeleo ya Taifa kutokana na pato linalopatikana kutokana na sekta hiyo.

Wito huo umetolewa leo jijini hapa na Mkurugenzi wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi katika salamu zake zilizowasilishwa kwa niaba yake na Meneja mawasiliano wa shirika hilo Pascal Shelutete katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani.

Shelutete alisema ujangili umekuwa ni jambo ambalo linapaswa kupingwa na kila mtanzania katika sekta aliyokuwepo badala ya kuiachia Tanapa kwa kuwa hifadhi za Taifa zimekuwa zikiliingizia Serikali mapato mengi ambayo yamekuwa yakitumika kwenye shughuli za maendeleo.

“Waandishi wa habari naombeni muungane na Tanapa na serikali kwa ujumla kupambana na vita dhidi ya ujangili, tunajua nguvu ambayo mmekuwa nayo kupitia kalamu zenu, hii ni vita mbaya kwa kuwa inahatarisha uhai wa nchi,”alisema Shelutete.

Alisema mchango wa waandishi wa habari unaotikana na uandishi mzuri kuhusu hifadhi za Taifa umekuwa ukionekana kutokana na wageni wengi kufika nchini kutembelea hifadhi hizo na kuiingizia Serikali mapato mengi

Shelutete alitoa wito kwa waandishi kuendelea kuandika taarifa mbalimbali za hifadhi za Taifa ili kuvutia zaidi wageni kuja nchini na kwamba shirika hilo litaendelea kushirikiana na waandishi wa habari.

Kwa upande wake, Meneja mawasiliano wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, Adam Akyoo alisema tunaposherehekea siku ya uhuru wa vyombo vya habari ni wakati wa kutathmini visa na mikasa ambayo waandishi wamekuwa wakikabiliana nayo.

Alitoa wito kwa mamlaka za Serikali kuheshimu tasnia ya uandishi wa habari kwa kutoa sheria nzuri na ambayo itaweza kueleza maudhuni mazuri ya tasnia hiyo nchini.

Ends… 

No comments: