Wednesday, March 4, 2015

OLOLOSOKWAN WAFURAHIA UJIO WA KIJIJI CHA DIGITALI, UNESCO WATOA MAFUNZO


DSC_0057
Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la IrikRAMAT linalomiliki Redio Loliondo FM, Bw. Yannick Ndoinyo akitoa maoni yake wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja iliyomalizika mwishoni mwa wiki wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya utekelezaji wa mradi kijiji cha Kidigitali (Unesco-Samsung Digital Village) cha Ololosokwan kilichopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Warsha hiyo ya wiki iliandaliwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)nchini.


DSC_0070
Picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo ya wiki moja iliyomaziki mwishoni mwa juma wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

DSC_0070
Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues akitoa maboresho ya kazi za vikundi vilivyokuwa vikijadili na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zilizopo katika kijiji cha Ololosokwan kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali.

DSC_0118
Mkurugenzi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisikiliza baadhi ya maboresho ya changamoto zilizojadiliwa na kikundi kazi cha sekta ya elimu na wadau mbalimbali wa elimu.

DSC_0064
Mkurugenzi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, akionesha kwa mifano baadhi ya bidhaa za nje zikivyokuwa na ubora kwenye vifungashio wakati wa warsha ya wiki moja inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha digitali (Unesco-Samsung digital village) kwa wakazi wa kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

DSC_0008
Kutoka kushoto ni Mathias Herman wa UNESCO, Mkurugenzi wa elimu ya msingi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Sarah Mlaki pamoja na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ololosokwan, Emmanuel Madeje.
DSC_0066
Pichani jii na chini ni wadau mbalimbali wa elimu, afya, Tehama na masuala ya utamaduni na uchumi waliohudhuria warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na UNESCO wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
DSC_0054
Afisa Miradi msaidizi kutoka UNESCO, Myoung Su Ko (kushoto) na Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Teresia Irafay wakinakili yanayojiri wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya uwapo wa kijiji cha kidigital (Unesco - Samsung digital village) katika kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

DSC_0051
Ofisa Ustawi wa jamii Ngorongoro, Beneth Bwikizo akitoa neno la shukrani kwa niaba ya ujumbe wa kijijini cha Ololosokwan uliohudhuria warsha hiyo ya wiki moja iliyomalizika mwishoni mwa juma wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
DSC_0018
Mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya afya kutoka UNESCO, Bw. Mathias Herman akiwasilisha mrejesho wa kikundi kazi chake wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali (Unesco-Samsung Digital Village) cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
DSC_0036
Mratibu wa shirika la IrikRAMAT  Foundation, Salangat Mako akitoa mrejesho wa suluhu za changamoto mbalimbali za kikundi cha uchumi na utamaduni wakati wa kuhitimisha warsha hiyo ya wiki moja.
DSC_0044
Mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya elimu kutoka UNESCO, Jennifer Kotta akitoa mrejesho wa kilichojadiliwa na kikundi chake.
DSC_0003
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya Tehama,  Al Amin Yusuph akiwasilisha mrejesho wa kazi ya kikundi chake wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha
Na Mwandishi Wetu
WAKAZI wa kijiji cha Ololosokwan wamesema kwamba ujio wa kijiji cha digitali katika kijiji chao ni neema kwao kwani kitawasaidia kukabiliana na changamoto kubwa za maisha zinazowakabili.
Kauli hiyo wameitoa mwishoni mwa wiki wakati wa kuhitimisha warsha ya siku saba ya kuangalia fursa na changamoto zitakazoambatana na mradi huo wa miaka mitatu unaodhaminiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO)  kwa kushirikiana na kampuni ya Ki-elektroniki ya Samsung.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake waliohudhuria warsha hiyo ambapo wataalamu mbalimbali wanaohusika na mradi huo walikutana kujadili changamoto na namna ya kukabiliana nazo, Salangat Mako, alisema kwamba tatizo la miundombinu, Afya na Elimu wanaamini litakabiliwa na mradi huo.
Alisema  kuna shida kubwa ya elimu kutokana na mazingira yaliyopo ambapo wanafunzi wanalazimika kutembea kilomita 14 kwenda na kurudi shule hali inayodhoofisha ari ya kujifunza.
Aidha alisema kwamba kuna changamoto katika zahanati yao yenye wauguzi wawili  huku hospitali ya wilaya ikiwa kiasi cha kilomita 50 hali inayowafanya watu wengi kutegemea mitishamba katika matibabu mbalimbali pamoja na wanawake kusaidiwa uzazi na wakunga wa jadi.
Alisema kuwepo kwa mradi huo kutasaidia wanafunzi kuweza kujisomea kwa kutumia mfumo wa mtandao wa intaneti na hivyo kuwa katika nafasi ya kuelimika vyema kutambua wajibu wao na fursa zilizopo  zinazowazunguka kwa kuwa hifadhini.
Aidha kuwepo kwa kiliniki ya mtandao kutaongeza ufanisi wa zahanati iliyopo pamoja na kuipa mkono katika tiba na kuondoa watu kutegemea tiba za asili.
Akizungumzia fursa za kiuchumi alisema ni matarajio yao kwamba kuwepo kwa kijiji hicho na utamaduni wake, kutawezesha kutumia vyema fursa za kitalii ili kukua kiuchumi kwa kujua mipango inayostahili katika kuendeleza utamaduni kwa jicho la kibiashara zaidi.
Naye Mganga mfawidhi wa zahanati ya Ololosokwan Obeid Laizer ambaye yupo katika kijiji hicho kwa miaka 15 amesema ana matumaini makubwa na mradi huo kwa kuwa mchanyato wake unaonekana kujali zaidi sosholojia za watu na afya zao hasa kwa kuwa na kliniki inayotembea na tiba kwa intaneti itakayomuwezesha kuwasiliana na madaktari wenzake ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya afya.
Alisema kwamba kijiji hicho kina magonjwa mengi japokuwa makubwa ni nyumonia, ukosefu wa damu, magonjwa ya zinaa, majereha ya wanyama kutokana na kuchunga mbugani na ugonjwa wa kuhara damu.
Alisema uwapo wa maabara utawasaidia kupata uhakika wa tiba kuliko sasa ambako wanafanya kwa kukisia zaidi.
Naye Ofisa Ustawi wa jamii Ngorongoro Beneth Bwikizo amesema kwamba mradi huo utaleta mabadiliko makubwa kwa wanakijiji hapo kutokana na shughuli nyingi za hapo kuhusanishwa na mradi huo.
Alisema mradi huo ambao unaangalia zaidi kukabili utamaduni unaokwamisha maendeleo kwa kutoa elimu na kuiunganisha na dunia nyingine kwa mawasiliano unaonekana utafanya maisha ya wakazi wa hapo kuboreka.
Alisema mradi huo wa kwanza nchini Tanzania na watatu bara la Afrika umempa hamasa kubwa baada ya kuona unaangalia changamoto zilizopo Ololosokwan ambazo ni za miundombinu katika elimu, afya na uchumi na kuzifanyia kazi.

No comments: