Saturday, March 7, 2015

UN YAZINDUA RIPOTI YA DAWA ZA KULEVYA DUNIANI

Uongozi wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) umezindua ripoti ya Kupambana na dawa za kulevyaa ya Umoja wa Mataaifa, Uzinduzi uliofanywa Machi 4, Jijini Dar es Salaam.
 
Wakizungumza mbele ya wandishi wa habari kwa upande wake, Afisa Habari wa Kituo Cha Habari wa Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo alibainisha ripoti hiyo imeweza kuchambua mambo mbalimbali dhidi ya dawa za kulevya na mikakati iliyofikiwa.
 
Ambapo alisema kuwa miongoni mwa mambo yaliyomo kwenye ripoti hiyo ni pamoja na kupungua kwa wimbi la kuingia kwa dawa za kulevyaa nchini hasa kupitia njia za bahari ya Hindi huku mji wa Mexico wa America, ukipunguza kwa asilimia kubwa matumizi ya dawa za kulevya.
 
Vuzo alibainisha kuwa, pia mikakati iliyofikiwa ambayo pia imo kwenye ripoti hiyo ni pamoja na mfumo wa kuwasaidia watumiaji wa dawa za kulevya wanaoacha kwa kuwapatia dawa maalum za kupunguza taratibu matumizi hayo.
DSCN9301
 Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya Taifa ya kudhibiti  Ukimwi (DCC), January Ntisi akionyesha ripoti hiyo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
 
‘Mipango ya kuwapatia wale wanaocha dawa maalum za kusaidia utumiaji wa madawa na pia dhidi ya kupambana na dawa maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi wa watumiaji” alisema Vuzo.
 
Aidha, alibainisha kuwa,  Afrika Kusini katika bara la Afrika ndio inayoongoza kwa kuwa na njia nyingi za usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya Cocaine na Heroine .


DSCN9317
Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya Taifa ya kudhibiti  Ukimwi (DCC), January Ntisi akifafanua jambo na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo.
DSCN9311
Baadhi ya waandishi wa habari na wadau wa kupambana utumiaji wa Madawa ya Kulevya waliohudhuria uzinduzi huo.

DSCN9299
Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Komputa wa Tume ya Taifa ya kudhibiti  Ukimwi (DCC), January Ntisi akizindua kitabu cha ripoti ya Bodi ya Kupambana na Dawa za Kulevya ya Umoja wa Mataifa, kwenye hafla ya uzinduzi uliofanyika Machi 4, MAELEZO, jijini Dar es salaam. Kushoto ni Afisa Mipango wa Umoja wa Mataifa, Immaculata Malyamkono-Nyoni na katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Kupambana na Watumiaji wa Madawa ya Kulevya,Very Kunambi.

DSCN9305
Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na uzinduzi wa ripoti ya Kupambana na dawa za kulevya ya Umoja wa Mataifa. Kulia ni mgeni rasmi Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya Taifa ya kudhibiti  Ukimwi (DCC), January Ntisi na kushoto ni Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama.


 

No comments: