Na
Rashid NchimbiwaJeshi la PolisiArusha
Wananchi Mkoani hapa
wameonekana kuwa na muamko zaidi wa Ulinzi Shirikishi baada ya kutoa taarifa mbili
zilizofanikisha kukamata misokoto 1,038 ya madawa ya kulevya aina ya bangi pamoja
na mirungi kilogramu 75.
Akizungumza na Waandishi
wa habari ofisi kwake, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi
wa Polisi (SSP) Gilles Muroto alisema kwamba katika matukio mawili yaliyofanikisha
ukamataji wa madawa hayo taarifa zake zilitolewa na raia wema.
Kaimu Kamanda Muroto
alisema kwamba, tukio la kwanza lilitokea tarehe 18.02.2014 muda wa saa 1:30
asubuhi maeneo ya Kituo Kikuu cha mabasi jijini hapa ambapo mtu mmoja aitwaye
Charles Ogaga Ayunga (38) raia wa Kenya nani mkazi wa Taveta nchini humo,
alikamatwa na misokoto 1,038 ya Madawa ya kulevya aina ya bangi iliyokuwa ndani
ya boksi.
Akifafanua taarifa hiyo
Kaimu Kamanda huyo alisema kwamba, siku ya tukio mtuhumiwa alikuwa anatokea maeneo
ya Ngaramtoni akiwa kwenye Hiace na alipofika maeneo ya Kituo Kikuu cha Mabasi alishuka
akiwa na boksi na kutaka kupanda basi linaloelekea Holili wilayani Rombo lakini
kabla hajapandisha boksi hilo kwenye basi hilo watu walimshuku na kutoa taarifa
katika kituo kikuu cha Polisi, ambapo askari waliokuwa doria maeneo ya karibu walikwenda
katika maeneo hayo na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa misokoto hiyo.
Mara baada ya mahojiano
mtuhumiwa alikiri kuumiliki madawa hayo ya kulevya aina ya bangi na kueleza kwamba
alikuwa anasafirisha kupeleka nchini Kenya.
Wakati
huo huo mtu mmoja aitwaye Philipo Santolin (25) Mkazi wa Holili
wilayani Rombo alikamatwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi yenye uzito wa kilogramu
75 ambayo ilikuwa imehifadhiwa kwenye vifurushi tofauti tofauti 7.
Akifafanua tukio hilo
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP)
Gilles Muroto alisema tukio hilo la ukamataji lilitokea tarehe 19/02/2014 muda wa
saa 2:00 usiku maeneo ya Kaloleni jijini hapa.
Alisema siku ya tukio
wananchi walitoa taarifa katika kituo kikuu cha Polisi kwamba, kuna mtu alikuwa
anasafirisha madawa hayo katika gari aina ya Corolla lenye namba za usajili T
162 AYW toka mkoani Kilimanjaro kuja Arusha, ndipo askari walipoweka mtego maeneo
ya Kwa Mrefu na mara baada ya gari hilo kusimamishwa halikusimama ndipo askari wa
kaamua kulifuatilia ambapo walifanikiwa kulikamata maeneo ya Kaloleni mara baada
ya gari hilo la mtuhumiwa kupasuka tairi la mbele.
Kaimu Kamanda Muroto
alisema mpaka hivi sasa watuhumiwa wote wawili wanahojiwa na watafikishwa makamani
mara baada ya upelelezi kukamilika.