watu wakitoa heshima za mwisho |
Mkurugenzi wa Kibo Palace Vincent Laswai akiteta jambo na mmoja wa waombolezaji |
Waombolezaji wakiwa na majonzi |
Jamal akifunga jeneza lililobeba mwili wa marehemu Babu Sambeke |
Jamal akifunga jeneza |
Mkurugenzi wa Hoteli ya Kibo Palace Vincent Laswai akitoa neno kabla ya kupakia mwili na kuusafirisha kwenda Moshi |
Waombolezaji wakiwa hawaamini kiilichotokea |
Waombolezaji |
Waombolezaji wakielekea kwenye magari kupanda kuelekea Moshi |
Mamia ya vigogo pamoja na watu mbalimbali
wafurika nyumbabi kwa marehemu Bilionea “Babu Sambeke”Ernest Sambeke eneo
la njiro jijini Arusha kuaga mwili wake unaotarajiwa kuzikwa kesho
nyumbani kwake eneo la Karanga mjini Moshi huku msiba huo ukiwa tofauti na
misiba mingine iliyozoekeaka hapa Nchini
Marehemu,Sambeke
alifariki hivi karibuni katika ajali ya ndege aliyokuwa akiiendesha na
pia mmiliki wa ndege hiyo ambapo ilianguka katika eneo la Kisongo na
kusababisha kifo chake Mkoani Arusha
Shughuli za kuaga mwili wa marehu
zilikamilika majira ya saa 8:45 mchana huku mwili huo ukipakiwa katika gari
maalumu la kifahari tayari kusafirishwa kuelekea nyumbani kwake Moshi kwaaajili
ya mazishi.
Taratibu
za kuaga mwili wa marehemu zilianza majira ya saa 5 asubuhi huku
wafanyabiashara wa madini pamoja wafanyabiashara wengine kutoka hapa Arusha na
Moshi walionekana kutawala msiba huo
Katika
zoezi hilo la kuaga mwili wa mareheu Padri Florentine Mallya ambaye ni mdogo wa
marehemu aliongoza misa ya kumuombea marehemu na baada ya kumaliza alitoa
fursa kwa watu mbalimbali kupita mbele ya jeneza kwaajili ya kuaga mwili
Ndani ya jeneza marehemu alivalishwa nguo
zake za kirubani huku ,baadhi ya wanajeshi kutoka jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ) walionekana jana katika zoezi la kuuaga mwili wa marehemu ambapo baadhi
yao walikuwa wamevalia sare za jeshi hilo
Hatahivyo,baadhi
ya watu walionekana katika hali ya kawaida huku watoto wakionekana
na nyuso za huzuni mda wote
Tofauti na misiba mingine nchini watu mbalimbali
walipata fursa ya kupata chakula na vinywaji mbalimbali kwa kujihudumia
vikiwemo vinywaji aina ya Bavaria ambapo watu waliohudhuria zoezi hilo
walionekana wakijihudumia zaidi vinywaji vya bavaria
Magari ya kifahari yalionekana kutawala msiba huo huku barabara ya njiro ikionekana kuwa na msongamano kubwa iliyosababishwa na zoezi hilo la uwagaji wa mwili
Marehemu aliacha watoto watatu ambao ni Sia,Jamal,Getruda
No comments:
Post a Comment