Monday, December 30, 2013

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATOA TAHADHARI KWA WAUAJI WA TEMBO


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII



TAARIFA KWA UMMA
Itakumbukwa kuwa Serikali iliamua kuanzisha “Operesheni Tokomeza Ujangili” kufuatia kukithiri kwa vitendo vya ujangili katika maeneo yote yaliyotengwa kisheria kama Mapori ya Akiba; Hifadhi za Taifa na Hifadhi za Misitu katika miaka ya karibuni. Hata hivyo, Serikali iliamua kusitisha operesheni hiyo kwa muda.

Kufuatia kusitishwa kwa Operesheni Tokomeza, matukio ya uvunjaji wa sheria za hifadhi kama vile uingizaji holela wa mifugo katika maeneo ya hifadhi; ujangili wa tembo pamoja na uvunaji wa miti katika hifadhi za misitu yanaonekana kushamiri. Aidha, kumekuwa na ongezeko la kuvamiwa watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na hata kuwasababisha madhara yakiwemo vifo na majeraha. Baadhi ya matukio hayo ni pamoja na:
·        Majangili kuua takriban tembo 60 katika Hifadhi/Mapori ya Selous, Rungwa, Burigi na Katavi na Ngorongoro. Hawa ni takriban tembo wawili kwa siku. Ikumbukwe kuwa wakati wa kipindi chote cha operesheni kilichodumu kwa mwezi mmoja ni tembo wawili tu waliokuwa wameuawa.  
·        Watumishi wa Pori la Akiba Mkungunero (Kondoa) waliokuwa doria kuvamiwa na kundi la watu wapatao 80 waliokuwa na mikuki na silaha nyingine za jadi  tarehe  24 Desemba, 2013.
·        Kuuawa kwa Askari mmoja wa wanyamapori aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Magengere (40) na mwingine, Bwana Yahaya Ramadhani (34), kujeruhiwa vibaya na Wafugaji walioingiza mifugo ndani ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Jumuiya (WMA) Ukutu (au JUKUMU) iliyoko Morogoro vijijini tarehe 6 Decemba, 2013.
·        Mtumishi mmoja wa wanyamapori, Sajidi Majidi, kujeruhiwa kwa kuchomwa mkuki kichwani na kuvunjwa mkono na wafugaji walioingiza ng’ombe katika Eneo la Ramsar la Kilombero tarehe 14 Novemba, 2013.
·        Kukamatwa kwa gari lililokuwa na mizoga 20 ya swala wilayani Simanjiro siku za karibuni
·        Kuanzishwa kwa kambi ya majangili katika Pori la Akiba Burigi ambapo vitendo vya ujangili vinaendeshwa. Majangili waliokuwa na silaha za moto walikimbia na kuacha nyuma nyani 30 waliokuwa wamewaua baada ya kukurupushwa na askari wa wanyamapori.
·        Kuongezeka wimbi la uvamizi na ufugaji wa mifugo ndani ya mapori ya akiba na hifadhi za misitu iliyopo magharibi mwa nchi yetu, hasa Burigi-Biharamulo-Kimisi, malagarasi-Moyowosi, Rukwa Lukwati, Luwanda, Ugalla, Ibanda-Rumanyika, Minziro na Katavi.

Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuwakumbusha wananchi kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 pamoja na Sheria zinazosimamia maeneo ya Hifadhi za Taifa na Misitu kuwa hairuhusiwi wananchi kuingia katika maeneo haya bila kibali ikiwa ni pamoja na uingizaji wa mifugo kwa ajili malisho. Aidha, bado vitendo vya ujangili haviruhusiwi chini ya sheria hizi. Kifungu cha 15 ni marufuku mtu yeyote kuingia kwenye pori la akiba bila kibali.  Aidha, Sheria hiyo inakataza kuwa na silaha yoyote ndani ya Pori la Akiba bila kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori [kifungu cha 17]; kuwinda, kuua, kukamata au kujeruhi mnyama [Kifungu cha 19] na kuchunga ng’ombe ndani ya Pori la Akiba [Kifungu cha 21].
Ikumbukwe kuwa matukio yaliyotokea bungeni Dodoma, hayajatengua Sheria yoyote ya Wanyamapori au Misitu.  Hamna maamuzi yoyote ya Bunge yaliyohalalisha ukiukwaji wa Sheria za Uhifadhi. Hivyo, wananchi wanatakiwa kutii na kufuata Sheria hizo kama zilivyo. Tahadhari inatolewa kuwa Serikali haitasita kumchukulia hatua kali yeyote atakayekiuka Sheria ya Wanyamapori kwa makusudi. Tunawaomba wananchi wasikubali kudanganywa na mtu yeyote yule kuvunja Sheria za nchi.

Aidha, nachukua nafasi hii kuwaagiza watumishi wote wa Wizara ya Maliasili na Utalii wahakikishe kuwa wanaendelea kutekeleza majukumu yao ya ulinzi wa maeneo ya Hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba na Misitu ya Hifadhi bila kutetereka. Sanjari na hilo wasisite kuchukua hatua stahiki dhidi ya mhalifu yeyote mradi tu wanazingatia Sheria, Kanuni na taratibu.  Utekelezaji huu wa sheria ufanyike bila kuathiri haki za msingi za binadamu.

Serikali ina maadili na miiko inayotawala utendaji kazi wa watumishi wake wote wakiwemo wale wa maliasili. Wizara ya Maliasili itaendelea kuwakumbusha watumishi wake juu ya maadili na miiko hii kupitia mafunzo ya mara kwa mara na mbinu nyingine. Aidha, Wizara itaendelea kuboresha miongozo inayohusu maadili na miiko hii ili iweze kuendana na wakati.

Mwisho, Serikali inasisitiza kuwa, kwa kutumia vyombo vyake, itaendelea kutekeleza majukumu yake na kusimamia ipasavyo Sheria ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayeshiriki moja kwa moja au kusaidia vitendo vya ujangili ili kunusuru rasilimali za Taifa. Jukumu la uhifadhi wa maliasili zetu liko pale pale, ni letu na lazima litekelezwe kwa manufaa ya kizazi hiki na vizazi vijavyo.

Imetolewa na:

Mh. Lazaro Nyalandu, MB.
NAIBU WAZIRI, MALIASILI NA UTALII
Desemba 29, 2013.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MHE. LAZARO NYALANDU (KUSHOTO) AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI (HAWAPO PICHANI) ALIPOKUWA AKIZUNGUMZIA MSIMAMO WA SERIKALI JUU YA MATUKIO YA UJANGILI NCHINI. KULIA NI KAIMU MKURUGENZI WA IDARA YA WANYAMAPORI PROFESA JAPHARY KIDEGHESHO.


Tuesday, December 17, 2013

MWEKEZAJI MZAWA AANZISHA HIFADHI MPYA NCHINI, NI YA WANYAMA ADIMU KAMA FARU WEUPE

Bonde la Laroi litakalotumika kwa ajili ya uhifadhi wa Faru weupe na wanyama wengine adimu waliopotea nchini ambapo kampuni ya uwekezaji ya HUGO itawaingia kutoka nchi za nje ikiwemo Afrika Kusini na Botswana

waandishi wa habari wakimhoji mjumbe wa Serikali ya kijiji cha Laroi Kitesho Kaya kuhusu makubaliano iliyofikiana kati ya Serikali ya kijiji hicho na Kampuni ya Hugo Investment 

waandishi wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Serikali ya kijiji cha Laroi 

Mkurugenzi wa Tanzaniasasa semmy kiondo wa kwanza kulia, David Rwenyagira aliyevaa tisheti nyeupe na Claud Gwandu wa kwanza kushoto wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Serikali ya kijiji cha Laroi pembezoni mwa hifadhi ya bonde la Laroi

Mwandishi wa habari Mkongwe, Claud Gwandu (kushoto) akiandika jambo, wengine kutoka kulia kwenda kushoto ni Semmy Kiondo, Mjumbe wa serikali ya kijiji cha Laroi Kitesho Kaya na aliyevaa shati jeupe ni Seif Mangwangi 

moja ya madarasa yatakayohamishwa 

moja ya darasa shule ya msingi Olemedeye  litakalohamishwa katika eneo la hifadhi ya bonde Laroi ambapo kampuni ya uwekezaji ya Hugo imeahidi kujenga majengo mengine mapya 

Waandishi wa habari katika picha ya pamoja, kutoka kushoto ni David Rwenyagira, Claud Gwandu, John Mhala, Shaban Mdoe, Semmy Kiondo na Raymond Nyamwihula wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya bonde la laroi litakalotumika kwa ajili ya uhifadhi wa wanyama adimu ikiwemo Faru

Mwandishi wa habari wa Sahara Media, Raymond Nyamwihula akiruka juu kwa furaha baada ya kuona bonde la LAROI litakalotumika kwa ajili ya uhifadhi wa Faru weupe na wanyama wengine adimu nchini

waandishi wa habari waliofika katika bonde la Laroi katika kata ya Mateves wilaya ya Arumeru litakalotumika kwa ajili ya uhifadhi wa Faru Weupe na wanyama adimu kutoka kushoto ni Claud Gwandu, Seif Mangwangi, John Mhala, Shaban Mdoe, Semmy Kiondo na Raymond Nyamwihula

Waandishi wa habari waliojumuika katika ziara ya kutembele bonde la Laroi litakalotumika kwa hifadhi ya wanyama adimu ikiwemo Faru weupe wakipata mlo wa mchana 

Waandishi wa habari waliofanya ziara ya kutembelea eneo la hifadhi katika bonde la Laroi wakipata mlo wa mchana, kutoka kushoto ni Semmy Kiondo( mmoja wa wamiliki wa blogu hii), John Mhala, Claud Gwandu na Shaban Mdoe


WAANDISHI WA HABARI WAFANYA ZIARA KIWANDA CHA NGUO A TO Z

Mtendaji Mkuu wa A TO Z Anuj Shah akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotembelea kiwandani kwake 

baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika meza moja wakisubiri kupata chakula baada ya kumaliza ziara ya kutembelea kiwanda cha A TO Z

Msaidizi wa masuala ya utawala wa mtendaji mkuu wa kiwanda cha A TO Z Abeid George akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Texas nje kidogo ya jiji la Arusha mara baada ya waandishi hao kutembelea kiwanda cha A TO Z

Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu (kushoto), akitoa hotuba yake kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha katika hoteli ya Texas mara baada ya kumalizika kwa ziara ya kikazi kutembelea kiwanda cha A TO Z

Msaidizi wa mtendaji Mkuu wa kiwanda cha A TO Z George Abeid akifurahia jambo 

Wasaidizi wa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha A TO Z kuhusu masuala ya utawala wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa ziara ya waandishi wa habari kutembelea kiwanda hicho 


waandishi wa habari wakiwa kwenye gari kuelekea katika kiwanda cha A TO Z 

and
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja na mtendaji mkuu wa kiwanda cha A TO Z Katikati ndugu Anuj Shah aliyevaa miwani pembeni yake kushoto ni ndugu Binesh ambae pia ni Mmoja wa wakurugenzi wa kiwanda hicho 
waandishi wa habari wakiwa ndani ya Chandarua, kulia ni Angelo Mwoleka na anaefuatia katikati ni David Rwenyagira

waandishi wa habari wakitembelea kiwanda cha A TO Z wa kwanza kulia ni queen Lema, David Rwenyagira, Zulfa Mussa, Mack Nkwame na Kulwa Mayombi
NA SEIF MANGWANGI,ARUSHA

IMEELEZWA kuwa tatizo la ajira nchini litaisha endapo watanzania watabadilika na kupenda kununua bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya nchini ikiwemo nguo na kuacha kuvaa mitumba.

Hayo yameelezwa juzi na mkurugenzi mtendaji wa kiwanda  cha A to Z Anuj Shah alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wanachama wa chama cha waandishi wa habari Arusha waliotembelea kiwanda hicho.

Shah alisema Tanzania imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa ajira jambo ambalo limekuwa likichangiwa na watanzania wenyewe kwa kupenda kununua bidhaa za nje na hivyo kutoa ajira kwa watu wa nje.

"Ukinunua bidhaa za nje ya nchi maana yake unatoa ajira kwa watu wa nje na unakosesha watanzania wa ndani, hapa atoz tunazalisha bidhaa bora na imara na tunazisafirisha nje ya nchi na baadae mnaletewa mitumba, kama mkinunua bidhaa za ndani mtasaidia watanzania kupata ajira,"alisema Shah.

Alisema matarajio ya baadae ya kiwanda ni kuendelea kuongeza ajira zaidi kwa watanzania kutoka 8000 iliyonayo hivi sasa hadi kufikia 10,000 na kuisaidia serikali katika harakati zake zake za kutokomeza tatizo hilo.

Akizungumzia mafanikio ya kiwanda Shah alisema kiwanda hicho kinatarajia kupanuka na kuongeza wigo wa usambazaji wa bidhaa zake nje ya nchi mara baada ya viwanda vyake viwili kumalizika ujenzi wake ambapo bidhaa za zaidi ya dola bil79 zitakuwa zikiuzwa.

Hata hivyo alisema matarajio hayo yatafanikiwa endapo atapata msaada wa kutosha kutoka serikalini pamoja na watanzania kwa kuanza kununua bidhaa za ndani na kuacha kununua mitumba kutoka nje ya nchi.

"Ukiangalia nchi kama bangladesh wamekuwa wakiuza bidhaa zenye thamani ya zaidi ya dola bil70 kwa mwaka lakini ni sababu wanapata msaasa kutoka serikalini na watu binafsi, kwanini tanzania tushindwe?, tuna nguvu kazi kubwa lakini hatuitumii,"alisema.

Alisema msaada mkubwa anaotarajia kupata serikalini ni pamoja na kutathmini viwango vya bei za umeme viwandani na kuzishusha ili kuwapunguzia gharama za bidhaa wanazozalisha