Mtendaji Mkuu wa A TO Z Anuj Shah akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotembelea kiwandani kwake |
baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika meza moja wakisubiri kupata chakula baada ya kumaliza ziara ya kutembelea kiwanda cha A TO Z |
Msaidizi wa mtendaji Mkuu wa kiwanda cha A TO Z George Abeid akifurahia jambo |
Wasaidizi wa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha A TO Z kuhusu masuala ya utawala wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa ziara ya waandishi wa habari kutembelea kiwanda hicho |
waandishi wa habari wakiwa kwenye gari kuelekea katika kiwanda cha A TO Z |
and
waandishi wa habari wakiwa ndani ya Chandarua, kulia ni Angelo Mwoleka na anaefuatia katikati ni David Rwenyagira |
waandishi wa habari wakitembelea kiwanda cha A TO Z wa kwanza kulia ni queen Lema, David Rwenyagira, Zulfa Mussa, Mack Nkwame na Kulwa Mayombi |
NA SEIF MANGWANGI,ARUSHA
IMEELEZWA kuwa tatizo la ajira nchini litaisha endapo
watanzania watabadilika na kupenda kununua bidhaa zinazozalishwa na
viwanda vya nchini ikiwemo nguo na kuacha kuvaa mitumba.
Hayo yameelezwa juzi na mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha
A to Z Anuj Shah alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wanachama
wa chama cha waandishi wa habari Arusha waliotembelea kiwanda hicho.
Shah alisema Tanzania imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa
ajira jambo ambalo limekuwa likichangiwa na watanzania wenyewe kwa
kupenda kununua bidhaa za nje na hivyo kutoa ajira kwa watu wa nje.
"Ukinunua bidhaa za nje ya nchi maana yake unatoa ajira kwa
watu wa nje na unakosesha watanzania wa ndani, hapa atoz tunazalisha
bidhaa bora na imara na tunazisafirisha nje ya nchi na baadae mnaletewa
mitumba, kama mkinunua bidhaa za ndani mtasaidia watanzania kupata
ajira,"alisema Shah.
Alisema matarajio ya baadae ya kiwanda ni kuendelea
kuongeza ajira zaidi kwa watanzania kutoka 8000 iliyonayo hivi sasa hadi
kufikia 10,000 na kuisaidia serikali katika harakati zake zake za
kutokomeza tatizo hilo.
Akizungumzia mafanikio ya kiwanda Shah alisema kiwanda
hicho kinatarajia kupanuka na kuongeza wigo wa usambazaji wa bidhaa zake
nje ya nchi mara baada ya viwanda vyake viwili kumalizika ujenzi wake
ambapo bidhaa za zaidi ya dola bil79 zitakuwa zikiuzwa.
Hata hivyo alisema matarajio hayo yatafanikiwa endapo
atapata msaada wa kutosha kutoka serikalini pamoja na watanzania kwa
kuanza kununua bidhaa za ndani na kuacha kununua mitumba kutoka nje ya
nchi.
"Ukiangalia nchi kama bangladesh wamekuwa wakiuza bidhaa
zenye thamani ya zaidi ya dola bil70 kwa mwaka lakini ni sababu wanapata
msaasa kutoka serikalini na watu binafsi, kwanini tanzania tushindwe?,
tuna nguvu kazi kubwa lakini hatuitumii,"alisema.
Alisema msaada mkubwa anaotarajia kupata serikalini ni
pamoja na kutathmini viwango vya bei za umeme viwandani na kuzishusha
ili kuwapunguzia gharama za bidhaa wanazozalisha
No comments:
Post a Comment