Thursday, March 21, 2013

UTALII WA NDANI- WAANDISHI WA HABARI WAKIWA NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA MANYARA KATIKA ZIARA YA SIKU MOJA BAADA YA KUMALIZA SEMINA YA SIKU MOJA KUHUSU UANDISHI WA HABARI ZA UTALII NA UTAMBULISHO WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA UTALII TANZANIA

Waandishi wa habari waliohudhuria semina kuhusu uandishi wa habari za utalii na maliasili nchini wakiwa katika picha ya pamoja

Peter Saramba wa Mwananchi mbele kulia akiongozana na Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za utalii na maliasili Doto John kushoto

Waandishi wa habari wakiingia ukumbini, katika hoteli ya Twiga iliyopo mto wa mbu mara baada ya kupiga picha ya pamoja, wa kwanza kushoto ni mwandishi Cynthia Mwilolezi wa Nipashe na anayefuata ni Julius Magodi ambae ni katibu mkuu wa chama cha waandishi wa habari za utalii na maliasini nchini

Mkurugenzi wa miradi wa shirika la Frankfurt zoological society na aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa TANAPA, Gerald Bigurube akihojiwa na waandishi wa habari wa TV mbalimbali nchini katika mji wa Mto wa mbu mara tu baada ya kumaliza kutoa mada yake katika semina ya waandishi wa habari na utambulisho wa chama cha waandishi wa habari za utalii na maliasili nchini

Mkurugenzi wa blogu hii, mwandishi wa habari mkongwe nchini Seif Mangwangi akinawa miguu kwa maji ya moto yanayopatikana katika hifadhi ya Taifa ya Manyara, kwa mujibu wa mhifadhi wa hifadhi hiyo Julie Lyimo, maji hayo hutibu fangasi na ngozi, wa mbele aliyenyanyua kifua ni Daniel Sabuni wa gazeti la Mwananchi, aliyeshika kiuno, Ramadhan Siwayombe wa Tanzania Daima

Monday, March 18, 2013

TANAPA FEES DISCUSSION

Acting TANAPA Director of Tourism Services Dr. Ezekiel Dembe gives his presentation before members of TATO on the new park fees
Some of the members of TATO who attended the meeting organized jointly by TANAPA and TATO

TATO officials from left Mustafa Akunaay and Cyril Ako follow the presentation from TANAPA

Executive Secretary of Tanzania Association of Tour Operators Mr. Mustafa Akunaay giving welcoming remarks during the TANAPA

Richard Beatty from African Environment making his contribution during the meeting to discuss the new park fees



BREAKING NEWS - DALADALA ZA ARUSHA KWA MROMBO ZAGOMA, ABIRIA WATESEKA, WATEMBEA KWA MIGUU KUJA MJINI

TAARIFA ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE, DALADALA ZA KWENDA KWA MROMBO KUTOKA MJINI ARUSHA ZIMEGOMA KUBEBA ABIRIA.

TAARIFA ZAIDI ZINASEMA KUWA KUGOMA KWA DALADALA HIZO KUNATOKANA NA KILE KINACHOELEZWA KUNYANYASWA NA ASKARI WA USALAMA BARABARANI AMBAO WAMEKUWA WAKIWAKAMATA MARA KWA MARA PINDI WANAPOSHUSHA ABIRIA NA KUWATOZA FAINI KUBWA.

ASKARI HAO WAMEKUWA WAKIDAIWA KUWAKAMATA KUFUATIA KUTEREMSHA ABIRIA KWENYE MAENEO YASIYOKUWA NA VITUO JAMBO AMBALO SIO SAHIHI KUFUATIA NJIA HIYO KUTOKUWA NA VITUO VYA KUSHUSHIA ABIRIA KAMA ILIVYOKUWA KWA NJIA ZINGINE.

AKIZUNGUMZA KWA MAOMBI YA JINA LAKE KUTOTAJWA KATIKA BLOGU HII, MMOJA WA MADEREVA HAO ALISEMA NJIA HIYO HAINA VITUO VYA KUSHUSHIA ABIRIA HIVYO WAMEKUWA WAKILAZIMIKA KUSHUSHA ABIRIA ENEO LOLOTE AMBALO LINAKUWA NA NAFASI YA KUFANYIA HIVYO.

ALISEMA KUTOKANA NA HATUA HIYO ASKARI WA USALAMA BARABARANI WAMEKUWA WAKIWAKAMATA NA KUWATOZA KIASI CHA SHILINIG ELFU30 KWA KOSA NA WAKATI MWINGINE HADI THS 60,000.

AIDHA ALISEMA ASKARI HAO WAMEKUWA WAKIWABAMBIKIA MAKOSA MENGINE AMBAYO HAWAKUYAFANYA NA HIVYO KUTOA RUSHWA ILI WAWAACHE WAENDELEE NA SHUGHULI ZAO ZA KUBEBA ABIRIA.

" TUMEKUWA TUKIKAMATWA NA ASKARI AMBAO WAMEKUWA WAKITUOMBA RUSHWA KAMA HUTAKI KUTOA UNABAMBIKIWA MAKOSA AMBAYO HUJAYAFANYA NA UKIPELEKWA POLISI KOSA MOJA KISHERIA NI TSH ELFU 30, HUU NI UONEVU MKUBWA AMBAO TUNAFANYIWA NA HAWA TRAFIKI,"ALISEMA.

ALISEMA WAMEKUWA WAKIWAPA TRAFIKI KIASI CHA THS 5000 HADI 20,000 ENDAPO WATAKAMATWA ILI KUSAMEHEWA KULIPA FAINI YA TSH 30 AMBAYO IMEANISHWA KISHERIA KWA KILA KOSA.

DEREVA HUYO ALISEMA MADEREVA AMBAO WAMEKUWA WAKIENDESHA GARI ZINAZOMILIKIWA NA TRAFIKI WAMEKUWA WAKIKOSA USUMBUFU WA TRAFIKI HAO KWA KUWA WAMEKUWA WAKIJUANA.




Sunday, March 17, 2013

ZIARA YA WAANDISHI WA HABARI KIWANDA CHA A TO Z

Mwandishi wa kampuni ya Habari Corporation na MC Abraham Gwandu, akifungua shampign jana katika hafla fupi iliyofanyika ukumbi wa TEXAS baada ya kumalizika kwa ziara ya kutembelea kiwanda cha A TO Z

Mwandishi wa kituo cha radio cha Radio 5 Ashura mohamedi(katikati), Pamela Mollel (wa kwanza kushoto) wa gazeti la Majira na Bertha Ismail wa kutoka Arusha wakicheza muziki wakati wa hafla fupi baada ya kumalizika kwa ziara ya kutembelea kiwanda cha A to Z.

kutoka kushoto Arusha Mohamed wa Radio 5, Mwandishi wa Channel Tena Jamila Omari na Pamella Mollel wakiserebuka taarab mara baada ya kumalizika kwa ziara ya kutembelea kiwanda cha A TO Z jana

Mwandishi Peter Saramba wa Mwananchi akiwa ndani ya Chandarua kinachotengenezwa na kiwanda cha A TO Z

Meneja Uajiri na msemaji mkuu wa kiwanda cha A TO Z George Abeid akiwaonyesha waandishi wa habari wanachama wa APC bidhaa zinazozalishwa na kiwanda hicho jana

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Arusha wakishuhudia namna ambavyo nishati ya kuendeshea mashine za kuendeshea mitambo ya kiwanda cha ATO Z inavyofanyakazi, anayeonekana mbele ni Asraji Mvungi wa ITV

Burudani ikikolea: Meneja uajiri wa A TO Z George Abedi akimtuza Pamella Mollel baada ya kuridhika na style yake ya kucheza

Sehemu ya tawi linalotumika kama nishati ya kuendeshea mitambo ya kiwanda cha A TO Z

Kassim Kiko akionyeshwa sehemu ya bidhaa zinazozalishwa na kiwanda cha A TO Z

Waandishi wa habari wakiwa ndani ya kiwanda

Wafanyakazi wa A TO Z wakiweka malighafi inayotengeneza chandarua tayari kwa kuyeyushwa ili kutoa nyuzi jana kiwandani hapo

Waandishi wa habari wakishuhudia msitu unaotumika kukatwa matawi na kiwanda cha A TO Z kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya kiwanda hicho

Thursday, March 14, 2013

WAFANYABIASHARA MADINI WAANZISHA CHAMA CHA USHIRIKA, LENGANASA ACHAGULIWA MWENYEKITI, SAMMY MOLLEL MAKAM MWENYEKITI, HARRY MUSHI KATIBU MTENDAJI

Afisa Biashara wa Jiji la Arusha Huruma Kibendwa akitoa elimu kwa wajumbe waanzilishi wa chama kipya cha ushirika cha TMTC  kwa wafanyabiashara wa madini ya vito nchini.

wajumbe wakifuatilia kwa makini

Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa TAMIDA Sammy Mollel akiwa miongoni wa wajumbe waanzilishi wa chama kipya cha ushirika cha wafanyabiashara wa madini ya vito wakimsikiliza kwa makini Afisa biashara wa jiji la Arusha Huruma Kibendwa(Hayupo pichani), kuhusu uanzishwaji wa chama hicho.

Wajumbe wa chama kipya cha ushirika cha wafanyabiashara wa madini TMTC wakimsikiliza kwa makini afisa biashara wa jiji la Arusha Huruma Kibendwa(Hayupo pichani)

Afisa Biashara jiji la Arusha Huruma Kibendwa akitoa maelezo kwa wajumbe waanzilishi wa chama kipya cha usharika cha Tanzanite Mining and Trading cooperative society limited jijini arusha jana

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA KWA UMOJA WA WANAFUNZI WALIOFUKUZWA VYUO NA VIKUU NCHINI UTANGULIZI 14.03.013

Awali ya yote tunamshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema na fadhia ambaye amekuwa ni tumaini la maisha yetu.

Ndugu waandishi wa habari, Mbele yenu ni umoja wa wanafunzi tuliofukuzwa vyuo vikuu nchini. Umoja huu unaitwa UUEST na unahusisha vyuo vikuu vifuatavyo; Chuo kikuu cha Dar es Salaam “UDSM”, Chuo kikuu cha Dodoma “UDOM” na Chuo kikuu cha Mhimbili “MUHAS”,Chuo kikuu cha MWALIMU NYERERE MEMORIAL, MUCCOBS, IFM na STJN. Umoja huu ulianzishwa rasmi tarehe 26/01/2013 baada ya maazimio ya wanafunzi waliofukuzwa kutoka vyuo husika kukubaliana kutengeneza umoja tajwa hapo juu.

Historia ya nchi yetu inaonyesha kuwa timua timua ndani ya vyuo vikuu nchini ilianza miaka ya 1990 [1992] lakini miaka ya 2008 hadi sasa suala hili limezidi kuwa kubwa ndani ya taifa letu,watawala wa vyuo vikuu nchini ambao ni maprofesa na baadhi ya viongozi waliopo serikalini wanalichukulia suala hili la kikatili kama mila na desturi na ni haki yao kimsingi kufukuza wanafunzi wa vyuo vikuu wenye mawazo mbadala, wenye uwezo wa kuhoji mambo, kukosoa uovu uliopo na unaoendelea kutendeka ndani ya vyuo vyetu na ndani ya taifa letu na wenye uwezo wa kutoa ushauri pale inapobidi kwa maslahi ya taifa lao. Ndugu waandishi wahabari, Kimsingi timua timua vyuoni ni janga la kitaifa ndani ya vyuo vikuu nchini na hakika tukilifumbia macho tunalizika taifa letu huku macho yetu yanashuhudia kwa sababu tunaidadi kubwa ya wanafunzi tuliofukuzwa vyuoni bila makosa kama takwimu hapo chini zinavyojionyesha na hatukustahili adhabu tulizopewa, pia tunatambua kunamikakati ya wazi iliyowekwa na baadhi ya viongozi waliopo serikalini wakishirikiana na watawala wa vyuo vikuu kuvizika vyuo vikuu visiwe visima vya fikra huru “think tank of our nation” na hii ni kwa sababu ya mfumo mbovu wa kuwapata watawala wa vyuo vikuu, mfumo huu wa kuteuana unawafanya watawala wa vyuo vikuu kutokuwa huru na kuwaabudu waliowateua, kutumika kisiasa, kukosa utashi wa maamuzi na kushinikizwa kufanya maamuzi ambayo hayaendani na utashi wa taaluma zao. Hii inapelekea vyuo vikuu kutokuwa huru na kuenenda kinyume na Tamko la Ulimwengu la tarehe 29th April, 1990 linalohusu uhuru wa kitaaluma (Academic Freedom) ambalo sisi kama taifa tuliridhia kulisaini hapa Dar Es Salaam ,Tanzania. Tamko hili linasema wazi kuwa ni lazima Vyuo vijiendeshe kwa uhuru kamili bila kuingiliwa na serikali .

Ndugu waandishi wa Habari, baada ya juhudi tulizozifanyandani ya mfumo na nje ya mfumo bila mafanikio na baada ya kupata taarifa mbaya juu yetu ambazo watawala wa vyuo vikuu walizipeleka ndani ya mfumo na nje ya mfumo kwa lengo la kutuchafua, tukaona tunahaja ya sisi wanafunzi tuliofukuzwa vyuo vikuu nchini kutafutana na kuungana kwa ajili ya kupeana taarifa rasmi za ndani ya mfumo na nje ya mfumo na pia tuamue hatima ya maisha yetu kwa kuwa na sauti moja, kupeana matumaini, kufikiri pamoja, kupanga na kufanya juhudi za pamoja ilikuhakikisha kila mmoja wetu anatimiza ndoto zake kielimu kwa namna yoyote ile.

TAKWIMU ZA WANAFUNZI TULIOFUKUZWA VYUONI MWAKA WA MASOMO 2011/2012 Kuanzia mwaka 2011 mpaka sasa, ni zaidi ya wanafunzi 145 wamefukuzwa ndani ya vyuo vyetu nchini. Tukimaanisha UDSM, UDOM, MUHAS, MWALIMU NYERERE MEMORIAL, MUCCOBS, IFM, STJN, na MZUMBE. Sababu zilizofanya wanafunzi hawa kufunzwa vyuoni ni kama ifuatavyo; Kudai mafunzo kwa vitendo,vifaa vya kujifunzia na mazingira bora ya kijifunzia Kudai kurejeshwa kwa serikali ya wanafunzi iliyofutwa na watawala wa vyuo Kudai mikopo ambayo inawasaidia kulipa ada zao na kujikimu maisha wakiwa vyuoni Kimsingi kupoteza ndoto za wanafunzi zaidi ya 145 ambao kiuhalisia wamesomeshwa na kodi za watanzania kwa sababu tu ya kudai haki zao za msingi ndani ya taifa lao ni kitendo kisichokuwa na dira njema kwa taifa.

Kwa sasa tuna msiba wa taifa katika sekta ya elimu, wanafunzi wengi waliofeli kidato cha nne ni watoto wa masikini waliosoma shule za kata, watoto hao hao wanaojitahidi kusoma na kufika vyuoni, wananyimwa mikopo, wananyimwa mafunzo kwa vitendo na wanaposimama kudai haki zao ili wamudu maisha ya kitaaluma vyuoni wanafukuzwa kikatili na kusingiziwa vitu wasivyovitenda. Uhalisia ni kwamba Taifa hili linatengeneza Tabaka la walionacho waendelee kuwaburuta tabaka la wasionacho.

NJIA TULIZOTUMIA KUTAFUTA SULUHU

Mara baada ya kufukuzwa vyuo vikuu nchini, tuliamua kuchukua hatua mbali mbali za kidiplomasia ili kuhakikisha suala letu linapatiwa ufumbuzi. Zifuatazo ni hatua tulizozifanya ndani ya taifa letu;

Tulifanya hatua za ndani ya vyuo vyetu ikiwemo kukata rufaa kwa maamuzi yaliyofanyika zidi yetu, kuomba mabaraza ya vyuo vyetu yapitie upya maamuzi yaliyofanyika kwa kuwaeleza ukweli halisi kinyume na taarifa potofu walizozitoa mbele ya vyombo vya habari bila mafanikio yoyote.

Tuliamua kwenda kwa waziri wa elimu Mh. Shukuru Kawambwa na kutuma taarifa sahihi kinyume na taarifa potofu zilizotolewa na watawala wa vyuo vyetu bila mafanikio yoyote.

Tuliamua kutuma taarifa sahihi kwa waziri mkuu wa nchi, Mh. Peter Kayanza Pinda na kumueleza ukweli halisi kinyume na taarifa potofu zilizotolewa na watawala wa vyuo vyetu, bila mafanikio yoyote.

Tarehe 27/07/2012 tuliamua kutuma waraka wa wanafunzi tuliofukuzwa vyuo vikuu nchini Bungeni kupitia kwa waziri kivuli wa Elimu Mh. Suzan. Lymo ili Bunge nalo lituhukumu kwa uhalisia wa taarifa tuliyoipeleka, Mh.mbunge aliwasilisha taarifa yetu wakati anasoma taarifa yake lakini tarehe 14/08/2012, waziri wa Elimu Mh. Shukuru Kawambwa aliipuuza hoja hii inayohusu mustakabali wa maisha yetu kielimu ndani ya taifa letu. 5. Tuliamua kwenda kamati ya bunge ya huduma za jamii na kuwapelekea taarifa rasmi juu ya matatizoyetu kinyume na taarifa za watawala wa vyuo vikuu bila mafanikio yoyote

6. Tuliamua kuwafuata viongozi mbali mbali ndani ya taifa letu ambao tulihisi watatusaidia kwa namna moja au nyigine, tulichoambulia ni taarifa mbaya zidi yetu ambazo zimepangwa na watawala wa vyuo vikuu wakishirikiana na baadhi ya viongozi serikalini.Ndugu waandishi wa habari; baadhi ya taarifa hizi ni kama zifuatazo ambazo tulizitoa kwa kiongozi nyeti ndani ya taifa hili.

Hatuta soma ndani ya nchi hii mpaka uongozi uliopo madarakani uondoke hivyo tusubiri miaka mitatu minne,

Tuliopo mahakamani tunajisumbua hatuwezi kupata haki katika mahakama,

Hatutadahiliwa chuo chochote nchini.

7. Tuliamua kupeleka taarifa katika asasi mbali mbali zisizo za kiserikali, LHRC, TLS, FORDIA, TAMWA, TAWLA, nk. Ili kuwaambia taarifa za ukweli na kuwaomba msaada wao wanaoweza kutupatia kutokana na tatizo letu. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwani baadhi yetu tulipata msaada wa kisheria toka LHRC na TLS.

8.Tuliamua kwenda katika asasi za kidini, tulituma taarifa sahihi kwa viongozi wetu wa kidini ili kupata msaada wao wa kiroho na kuliombea suala letu, pia wao kama viongozi wa dini kuingilia kati juu ya uonezi uliofanyika lakini mpaka leo bado suala letu halijapata ufumbuzi.

SABABU ZA KUUNDA UMOJA HUU
Tunafahamu kuwa ndani ya taifa letu tuna mihimili mikuu mitatu, Serikali, Bunge na Mahakama, mpaka sasa Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halijawa suluhu ya matatizo yetu na hii ni kwa sababu ya taarifa potofu zilizotolewa na watawala wa vyuo vikuu nchini, na kupelekea kuchafua taswira zetu na kupoteza utu wetu mbele ya jamii. Ndugu waandishi wa habari; Tumechukua hatua stahiki mbali mbali kama ilivyoelezwa hapo juu bila mafanikio yoyote, na tukizingatia matamko ya watawala wa vyuo vikuu kuwa haturuhusiwi kudahiliwa vyuo vyovyote vya umma ndani ya Taifa letu kiuhalisia nisawa na kuwa tumehukumiwa adhabu ya kifo ndani ya Taifa letu na sisi tunaamini hatustahili adhabu hii.

kwa sababu watawala wa vyuo vikuu wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kututenganisha na jamii zetu, familia zetu, ndugu na jamaa, viongozi wetu wa kidini na kisiasa kwa taarifa za uongo kupitia vyombo vya habari tumeona suluhu ya maisha yetu ni kuungana, muungano huu umeundwa kwa sababu zifuatazo;

1.Hatua zote tajwa hapo juu tulizozichukua ndani ya Taifa letu zimeshindikana.

2.Wote tulikuwa tuna tatizo la aina moja la kufukuzwa vyuo vikuu kwa sababu ya uzalendo wetu wa kutetea haki zetu na haki za wavujajasho ndani ya taifa letu
3.Tumeungana kwa sababu nafsi nyingi za wanafunzi tuliofuzwa vyuoni zinakufa, kwa sababu ya kukosa matumaini ya maisha, kukosa msaada kutoka katika familia na jamii tunayotoka, hali hii ilitokana na taarifa potofu zilizotolewa na watawala wa vyuo vikuu wakishirikiana na serikali kupitia vyombo vya habari, kutusingizia kuwa ni vinara wa vurugu, tumepiga wajawazito, tumebaka, tumetengeneza mabomu, tunatumiwa na vyama vya siasa na kashfa mbali mbali ambazo jamii kwa ujumla wake walijengeka kuwa sisi ni watu hatari na hatufai hatimaye kututenga katika mapito yetu.
Kiujumla hizi ndizo sababu zilizotufanya tuungane.

AZIMIO LETU

Tunaiomba serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunamuomba raisi Jakaya Mrisho Kikwete alichukulie jambo hili kwa uzito unaostahili huku akiangalia mustakabali wetu na wa taifa letu. Lakini umefika wakati wetu wa kuwaambia ukweli kwamba tumenyanyaswa, tumepuuzwa,tumebezwa, tumetukanwa , tumeteswa na tumeonewa kwa mda mrefu mpaka hivi sasa kana kwamba sisi ni watumwa kwenye nchi hii.

HITIMISHO

Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini tutambue kwamba sisi ni sehemu ya wanajamii ya kitanzania. Hivyo kwa nafasi yetu tuna haki na ni wajibu wetu kukemea,kurekebisha,kuhoji na kushauri pale tunapoona mambo yanaenda ndivyo sivyo.Vyuo vikuu vimepoteza dira, macho yetu yanashuhudia. Taifa letu limekuwa shamba la bibi, tunashuhudia hayo na bado tupo kimya, vyuo vyetu vinazimwa visiwe visima vya fikra huru. Maadili ya viongozi ndani ya taifa letu yamepotea. Bunge linashindwa kulitendea haki taifa hili kwa sababu ya mvutano wa kiitikadi wasomi tunashindwa kunyosha vidole vyetu kukemea uovu, Tunashindwa kusimama kulisaidia taifa letu, kwa sababu ya mabomu, risasi,virungu tunayopigwa tukisimama kutetea muafaka mwema wa taifa letu, vijana wa taifa hili tufumbue macho. Ikumbukwe kuwa Mwl J.K.Nyerere aliwahi kufika chuo kikuu cha Dar es Salaam wanafunzi walipogoma, alienda akawasikiliza akayapima na akatambua kuwa wanafunzi wanahoja za msingi akaamua aanze kujipunguzia mshahara wake mwenyewe kwanza. Huyu ni mfano kiongozi wa kuigwa ambaye anahitajika ndani ya taifa letu. Suluhu ya matatizo vyuo vikuu nchini sio timua timua, sio vitisho na Mabavu, sio nguvu ya vyombo vya dola, sio mabomu, sio risasi za moto, sio virungu ila ni busara kama aliyoitumia hayati Mwl. J. K . Nyerere kuenda kusikilizana na kupata muafaka sahihi.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA 13/03/2013.

RAI YANGU KWA WATANZANIA.

MIMI KAMA MSEMAJI MKUU WA UMOJA HUU "UUEST".

HII NI TAARIFA SAHIHI KUTOKA KWETU. CHOMBO CHOCHOTE CHA HABARI, MTU YOYOTE YULE ATAYEPOTOSHA UKWELI HUU MFAHAMU ANALENGO LAKE BINAFSI AU AMENUNULIWA.

LAKINI PIA NACHUKUA FURSA HII KUWAOMBA WATANZANIA WOTE YANI VIONGOZI WEMA WALIOKO SERIKALINI, VIONGOZI WEMA WA KIDINI, WABUNGE WOTE BILA KUJALI ITIKADI ZA VYAMA VYETU, ASASI ZOTE ZOTE ZA KISERIKALI NA ZISIZO ZA KISERIKALI, NA WADAU MBALI MBALI AMBAO WANATAMBUA KUWA TULIPOFIKA KAMA TAIFA NI PABAYA NA NI HATARI KWA AMANI YA NCHI HII. WATUUNGE MKONO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE ILI KUHAKIKISHA NDOTO ZA VIJANA ZA KIELIMU ZILIZOPOTEZWA ZINAPATIKANA KWA NJIA YOYOTE ILE. HIVYO KUANZAIA SASA TUNAKUJA KWENU WATANZANIA.

KWA WALE WOTE WALIOPOST KUWA TUMEOMBA MSAMAHA HAMJUI MLITENDALO, MJUE KUWA NI UDHALIMU TU TUMETENDEWA NDANI YA TAIFA LETU . MKIKUA KIFIKRA MTAYAACHA HAYO, HATUNA UGONVI NA NYIE ILA MTAMBUE KUWA TAIFA LETU LINALIA NA TUNAHITAJI NGUVU YA PAMOJA ILI KULIKOMBOA TAIFA BILA KUJALI ITIKADI ZETU ZA KIDINI, KIVYAMA, MAKABILA YETU. ILA KWA PAMOJA TUBEBE ITIKADI YA UTANZANIA, HAKIKA TUTAFIKA.

WANAFUNZI WA VYUO VIKUU LISAIDIENI TAIFA.

MWISHO KABISA NI WAJIBU WA RAISI JAKAYA KIKWETE KULITENDEA HAKI TAIFA HILI. MOYO WAKE UTAMBUE KUWA VYUO VIKUU NI INJINI YA NCHI YOYOTE ILE DUNIANI, NI VISIMA VYA FIKRA HURU NA HUU NI UKWELI AMBAO UTASIMAMA MILELE.KUVIZIMA VYUO VIKUU NI KULIZIKA TAIFA, KITU AMBACHO NAAMINI RAISI WETU HANA LENGO HILO. TUTAITAMBUA DHAMIRA YA RAISI WETU JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA VITENDO NA SI VINGINEVYO.

MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Wednesday, March 13, 2013

PAPA MPYA RAIA WA AGENTINA ATAITWA POPE FRANCIS I

Kadinali Jorge Mario Bergoglio wa Argentina amechaguliwa kuwa Papa mpya wa Kanisa Katoliki.

Kadinali Bergoglio anakuwa mtu wa kwanza kutoka Amerika kusini kuchaguliwa kuwa Papa.

Mara tu baada ya kuchaguliwa alichagua jina la Papa Francis I.

Awali moshi mweupe ulishuhudiwa ukifuka kutoka bomba la kutolea moshi katika kanisa la Sistine Chapel na kufuatiwa na kengele kupigwa. Hii ilikuwa ni ishara kwa walimwengu kuwa makadinali ambao walianza mchakato wa kumchagua Papa mpya hatimae walikuwa wamefaulu katika kazi yao.

Kadinali Bergoglio anachukuwa mahali pa Papa Benedict XVI, ambaye alijiuzulu mwezi uliopita akisema hana nguvu na uwezo wa kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki.

Makadinali 115 wamekuwa faraghani tangu siku ya Jumanne alasiri na wakaanza mchakato wao kwa kupiga kura mara nne kwa siku.

Ilikuwa inahitajika kuwa angalau Makadinali 77 yaani theluthi-mbili wangeliweza kumpigia kura mmoja wao ili aweze kutangazwa kuwa Papa mpya.

Na kabla ya mchakato huo kuanza kulikuwa hakuna dalili za kuonyesha nani angelichaguliwa.

Moshi mweupe

Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali duniani walikwa wamekusanyika katika ukumbi wa Kanisa la St Peter tangu siku ya Jumanne.

Muda mfupi kabla ya Kadinali Bergoglio kujitokeza , maelfu ya watu walionekana wakikimbia kuelekea ukumbi wa St Peters ili kuweza kumshuhudia Papa mpya akitangazwa .
Papa Francis I ni nani?

Alizaliwa Mjini Buenos Aires huko Argentina mwaka1936.

Papa Francis 1 ni mtu wa kwanza katika kipindi cha miaka elfu moja (1,000) kwa mtu kutoka nje ya bara la Ulaya kutawazwa kuwa papa wa Kanisa Katoliki.

Papa Francis 1 ni mwana wa Mtaliano aliyekuwa akifanya kazi katika shirika la gari Moshi kabla ya kuhamia nchini Argentina miaka ya zamani.

Kama kadinali wa Jimbo la Buenos Aires ,Kadinali Bergoglio amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Argentina.

Hata hivyo Kadinali Bergoglio anapendwa sana na wafuasi wa kanisa hilo huko Argentina na hasa watu maskini.

adinali Jorge Bergoglio, mwenye umri wa mwaka 76, kwa karibu miaka yake yote kama Kasisi amehudumu nyumbani kwao Argentina.

Kadinali huyo wa Jimbo la Buenos Aires inasemekana aliibuka nambari mbili wakati Papa Benedict alipochaguliwa mwaka 2005

Papa Francis akijitokeza

Anaaminika kuwa na ujuzi mkubwa ambao wengi wanasema utamsaidia sana katika uongozi wake.

Katika maisha yake ya huduma kwa Kanisa Katoliki huko Amerika Kusini ambapo Kanisa Katoliki lina waumini wengi zaidi duniani, Kadinali Bergoglio ameibuka kuwa mtu anayependa sana udhabiti wa kisiasa katika nchi zilizo katika bara la Amerika Kusini.

Bergoglio anasifiwa kwa kuleta mageuzi makubwa katika Kanisa la Argentina huku katika eneo hilo la Amerika Kusini Kanisa bado linashikilia itikadi za kale.

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM, ABDULRAHMAN KINANA NA BAADHI YA VIONGOZI WA SEKRETARIETI YA CCM WAKIWA KATIKA ZIARA CHINA

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika mazungumzo na Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013, katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou, China. (Picha na Bashir Nkoromo)

katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Martine Shigela akibadilishana mawazo na Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013, katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou,
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkabidhi zawadi ya kinyango cha Kimakonde, Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013, katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou, China. (Picha na Bashir Nkoromo).

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wa pili kulia) akimtambulisha Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengelema, kwa Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013, katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou, China. (Picha na Bashir Nkoromo)

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kushoto) akibadilishana mawazo na Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013, katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou, China. (Picha na Bashir Nkoromo).

Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai ‘akitosi’ kinywaji kwenye kijiglasi maalum cha kinywaji, na Katibu wa Kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013, katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou, China. (Picha na Bashir Nkoromo).

Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (CCM, Dk.Asha-Rose Migiro akimshukuru Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013, katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou,

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Khadija Aboud akisalimiana na Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013, katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou, China. (Picha na Bashir .

Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Khamis Suleiman Dadi akisalimiana na Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013, katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou, China. (Picha na

Tanzania: Wildebeests' May Avoid Kenya This Year!











Early indicators show that the world-famous Serengeti Migration involving mass movement of over 2.5 million herbivores may not enter Kenya's Maasai-Mara this year.

Experts at Serengeti National Park point out that time spent by the ungulates in Maasai Mara has been falling from two months to just a few weeks in recent years, with the shortest time recorded last year (2012) when the animals stayed in Kenya for less than two weeks.

"Increasing human activities at Maasai-Mara which is the Kenyan side of the Serengeti Eco-system is what causes the annual migration of Wildebeests to reduce and eventually stop going into the vicinity altogether," explained Mr Godson Kimaro the senior Park Warden at Serengeti National Park.

He also recalled a scientific study report by the Frankfurt Zoological Society (FZS) which had warned of imminent changes in the wildebeests migratory patterns in future. The trend has started to change.

This year the migration involving 1.5 wildebeests, 400,000 zebras and thousands of antelopes as well as gazelles (with predatory hyenas towing in the rear), seems to be spending more time than usual in the southern part of the Serengeti as well as the Ngorongoro Conservation Area.

It is thus feared that by the time the period to cross to Kenya arrives (around July/ August), the ungulates will still be farther from the border such that when the interval to start moving back south reaches, the animals may be forced to make an about-turn without reaching Maasai-Mara.

Mr Seth Mihayo, the Tourism Conservator at Serengeti National Park warned that the Maasai Mara Reserve of Kenya, which is the recipient of the annual Wildebeests Migration from Tanzania is also suffering mushrooming hotel premises, real estate developments and human activities such as cattle grazing all of which add to the effects that scare animals away.

Climate change is also taking toll in Maasai Mara where depleted natural green cover and shrinking water springs make the area hostile to wild animals.

Previously Dr James Wakibara the Serengeti Ecologist explained that until now no scientists and researchers have been able to find out what exactly causes the over 1.5 million wildebeests, 400,000 zebras and a number of gazelles that form the annual mass movements of herbivores to migrate from Tanzania to Kenya annually.

"Citing food, water, rains or predators as possible driving forces have all been theories that were never proven and likewise the their sudden change in the number of days spent in Kenya or stopping altogether moving there also need thorough study and extensive investigation," Dr Wakibara stated.

Should the wilbeeste stop going to Maasai-Mara this year, tourists and other visitors who usually come to East Africa purposely to watch the spectacular event will be compelled to view it from only Serengeti National Park and especially along the banks of Mara River.

allAfrica.com: Tanzania: Wildebeests' May Avoid Kenya This Year!

PETITION TO: REGISTRAR THE HIGH COURT OF KENYA NAIROBI

 
REPUBLIC OF KENYA
IN THE HIGH COURT OF KENYA AT NAIROBI
CONSTITUTION & JUDICIAL REVIEW pISION 
PETITION NO. OF 2013
IN THE MATTER OF: ARTICLE 22 (1) OF THE CONSTITUTION OF KENYA
AND 
IN THE MATTER OF: ALLEGED CONTRAVENTION OF FUNDAMENTAL RIGHTS AND FREEDOMS UNDER ARTICLES 2 (1), 3 (1) 10 (1) (2), 19 (2), 20 (2), 27 (1), 35 (1), 38(1) (2) & (3), 47 (1) (2), 48, 50 (1)(2), 81 OF THE CONSTITUTION OF KENYA 2010
AND
IN THE MATTER OF BREACH OF THE RIGHT TO INFORMATION 
BETWEEN
ELIUD OWALO...................…………………………………..……………………PETITIONER
VERSUS
INDEPENDENT ELECTORAL BOUNDARIES 
COMMISSION (IEBC)…………………………......... …............….……..1ST RESPONDENT
SAFARICOM LIMITED..............................................................2ND RESPONDENT 
PETITION
TO: REGISTRAR 
THE HIGH COURT OF KENYA
NAIROBI

The Humble Petition of ELIUD OWALLO of P. O. Box care of Rachier and Amollo Advocates 55645-00100 Nairobi in the Republic of Kenya is as follows :- 
THE PARTIES
1. The Petitioner is a male adult of sound mind residing and working in Nairobi and a duly registered voter in the general elections held on 4th March 2013. His address of service for purposes of this suit shall be C/o Rachier & Amollo Advocates, Ralphe Bunche Road, Mayfair Centre, 5th Floor, P.O. Box 55645-00200 Nairobi.


2. The 1st Respondent is the Independent Electoral Commission of Kenya duly established under the Constitution of Kenya (Service of summons shall be effected through the Petitioners Advocate’s office) 
3. The 2nd Respondent is a limited Liability Company duly established under the companies Act Laws of Kenya (Service of summons shall be effected through the Claimant’s Advocate’s office)

LEGAL FOUNDATIONS OF THE PETITION
4. Article 2(1) of the Constitution of Kenya pronounces the supremacy of the Constitution and provides that the Constitution binds all persons and state organs at both levels of government.

5. Article 3(1) of the constitution states that every person has an obligation to respect, uphold and defend the Constitution.
6. Article 10 of the constitution of the Republic of Kenya sets out the national values and principles of government. Among the national values and principles of governance are rule of law, equity, inclusiveness, equality, human rights, non- discrimination, good governance, transparency and accountability.

7. Article 19 of the Constitution of Kenya asserts that the Bill of rights is an integral part of Kenya’s democratic state and is the framework for social, economic and cultural policies and that the purpose of recognizing and protecting human rights and fundamental freedoms.

8. Article 20 states that every person shall enjoy rights and fundamental freedoms in the Bill of rights to the greatest extent consistent with the nature of the right or fundamental freedom.
9. Article 22 of the constitution vests locus standi for the enforcement of the Bill of rights in; among others the petitioner.

10. Article 23 vests authority in this Honourable Court to uphold and enforce the Bill of Rights and highlight some of the remedies that this Honourable Court can grant to uphold and enforce bill of rights.
11. Article 27 of the Constitution provides for equality and freedom from discrimination and in particular provides that every person is equal before the law and has the right to equal protection and equal benefit of the law.

12. Article 28 of the Constitution provides that every person has inherent dignity and the right to have that dignity respected and protected.
13. Article 47 of the Constitution states that every person has the right to administrative action that is expeditious, efficient, lawful, reasonable and procedurally fair.

14. Article 48 of the Constitution states that the state shall ensure access to justice for all persons and, if any fee is required, it shall be reasonable and shall not impede access to justice.
15. Article 258 of the Constitution provides that every person has the right to institute court proceedings, claiming that the constitution has been contravened.

THE FACTS 
16. The Petitioner being a registered voter in Nairobi within the Republic of Kenya duly exercised his right as a voter on the 4th of March 2013 and participated in the General Elections in Kenya as enshrined in Article 38 of the Constitution of Kenya.

17. On perse dates after the said elections, the results of the Elections started streaming in and were projected on screens at the Bomas Tallying Centre.
18. The Petitioner having scrutinized the numbers that were streaming in before the Electronic tallying system collapsed and the results that were announced thereon after is of the strong view that the outcome of the general election has been fraudulently manipulated with the results that his rights under Article 10, 38 and 81 of the Constitution of Kenya 2010 have been infringed and or threatened with infringement. 

19. Owing to the above, the Petitioner drew a letter to the 1st Respondent on the 8th of March 2013 requesting that several information which were in the power, possession and/or custody of the 1st Respondent be released to him. 

20. The documents requested for included the following:
i. All form 34, 35, and 36 from all polling stations and constituencies all over the country in relation to the presidential elections;
ii. All the results that were declared electronically at the Bomas Tallying Centre;

iii. The log files for all short messages that were declared electronically received from Safaricom;
iv. All software contracts between the 1st Respondent and all firms that provided software services to them in connection with the just concluded general elections.

v. Serial numbers of all handheld transmission devises that were actually configured and made ready for use as aforesaid and the constituencies in which they were meant to be used.
vi. Serial numbers of all handheld transmission devises that were configured and the constituencies in which they were meant to be used

vii. The Green book
viii. Provisional register of all registered voters
ix. Final register of all registered voters
21. A similar letter was relayed to the 2nd Respondent who’s services were relied on by the 1st Respondent to relay information from all polling stations where the following documents were requested for:

i. The numbers of all handheld transmission devices that were used to electronically transfer date from polling stations to the tallying centre.
ii. Print out of all messages that were sent through all handheld transmission devices that were used to electronically transfer data from the polling stations.

iii. All contracts signed between the 1st and 2nd Respondent in connection with the just concluded general election.
iv. Record of all information transmitted to the 2nd Respondent Server on the 4th and 5th days of March 2013.

22. The Petitioner relied on his right to information under Article 35 to request for the said documents but the 1st and 2nd Respondent’s have ignored his requests despite the Petitioner undertaking to bear all costs and expenses in connection with the processing and production of the information sought, upon being notified of the cost.

23. The notice period issued by the Petitioner was two (2) days which have already expired without any communication from the 1st and 2nd Respondent.
24. The Petitioner wishes to file a Petition at the supreme court to challenge the presidential election process and wishes to rely on the said information being with held by the Respondents. 

25. The said petition should be filed within Seven days of the announcement of the results a time which expires on the 16th March 2013.
26. If the said documents are not released to the Petitioner his rights will remain infringed. 

VIOLATIONS OF THE CONSTITUTION AND FUNDAMENTAL RIGHTS AND FREEDOMS
27. Violation of Article 10 of the Constitution 
The 1st and 2nd Respondent’s actions of declining to issue the information sought by the applicant contravened the Principles of good governance, integrity, transparency and accountability. 

28. Violation of Article 27 of the Constitution 
the 1st and 2nd Respondent attempt to bar the Respondent from accessing information needed to protect his fundamental rights and freedoms is a violation of the Petitioner’s right to Equality before the law. 

29. Violation of Article 28 of the Constitution.
The 1st and 2nd Respondent’s actions of neglecting the Petitioner’s plea to avail information are a violation of the Petitioner’s right to the Petitioner’s human dignity as the same is an abuse of the Petitioner’s right to information. 

30. Violation of Article 35 of the Constitution
The 1st and 2nd Respondent’s action of deliberately refusing/ignoring/neglecting to give requisite documents to the applicant is a violation of the Applicant’s right to information as the information is required for enforcement of the Fundamental rights and freedoms of the Petitioner.

31. Violation of Article 47 of the Constitution 
The 1st and 2nd Respondent’s actions of failing to release the Requisite documents is a violation of the Applicants right to fair Administrative action as the respondents should be barred by the law.

32. Violation of Article 48 of the Constitution.
The Respondents have barred the Petitioner from accessing information needed in enforcing the Petitioners rights hence they have denied the Petitioners right to Access justice. 

PRAYERS
The petitioner therefore humbly asks for the following orders:
a. An order directing the 1st Respondent to release forthwith all the information in their possession that can be used to support the 1st Respondent’s claim, as listed herein below: 
i. All form 34, 35, and 36 from all polling stations and constituencies all over the country in relation to the presidential elections;
ii. All the results that were declared electronically at the Bomas Tallying Centre;

iii. The log files for all short messages that were declared electronically received from Safaricom;
iv. All software contracts between the 1st Respondent and all firms that provided software services to them in connection with the just concluded general elections.

v. Serial numbers of all handheld transmission devises that were actually configured and made ready for use as aforesaid and the constituencies in which they were meant to be used.
vi. Serial numbers of all handheld transmission devises that were configured and the constituencies in which they were meant to be used

vii. The Green book
viii. Provisional register of all registered voters
ix. Final register of all registered voters
b. An order directing the 2nd Respondent to release forthwith all the information in their possession as listed herein below:
i. The numbers of all handheld transmission devices that were used to electronically transfer date from polling stations to the tallying centre.
ii. Print out of all messages that were sent through all handheld transmission devices that were used to electronically transfer data from the polling stations.

iii. All contracts signed between the 1st and 2nd Respondent in connection with the just concluded general election.
iv. Record of all information transmitted to the 2nd Respondent Server on the 4th and 5th days of March 2013.

c. Interest on (c), (d), (e) to the proposed claimant.
d. Any other relief that this court may deem fit and just do grant to the proposed plaintiff.
WHICH PETITION is grounded on the Affidavit of ELIUD OWALLO annexed hereto and on such other or further grounds as may be adduced at the Hearing hereof.

Dated this ..........................................day of…….…..….………..…….. 2013
RACHIER & AMOLLO
ADVOCATES FOR THE PETITIONER
DRAWN & FILED BY:
RACHIER & AMOLLO
ADVOCATES
MAYFAIR CENTRE, 5TH FLOOR
RALPHE- BUNCHE ROAD
P O BOX 55645-00200
NAIROBI 
TO BE SERVED UPON:
“If the Respondents do not enter an appearance within the time above mentioned such order may be made and proceedings taken as the court may think just and expedient.”