TAARIFA ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE, DALADALA ZA KWENDA KWA MROMBO KUTOKA MJINI ARUSHA ZIMEGOMA KUBEBA ABIRIA.
TAARIFA ZAIDI ZINASEMA KUWA KUGOMA KWA DALADALA HIZO KUNATOKANA NA KILE KINACHOELEZWA KUNYANYASWA NA ASKARI WA USALAMA BARABARANI AMBAO WAMEKUWA WAKIWAKAMATA MARA KWA MARA PINDI WANAPOSHUSHA ABIRIA NA KUWATOZA FAINI KUBWA.
ASKARI HAO WAMEKUWA WAKIDAIWA KUWAKAMATA KUFUATIA KUTEREMSHA ABIRIA KWENYE MAENEO YASIYOKUWA NA VITUO JAMBO AMBALO SIO SAHIHI KUFUATIA NJIA HIYO KUTOKUWA NA VITUO VYA KUSHUSHIA ABIRIA KAMA ILIVYOKUWA KWA NJIA ZINGINE.
AKIZUNGUMZA KWA MAOMBI YA JINA LAKE KUTOTAJWA KATIKA BLOGU HII, MMOJA WA MADEREVA HAO ALISEMA NJIA HIYO HAINA VITUO VYA KUSHUSHIA ABIRIA HIVYO WAMEKUWA WAKILAZIMIKA KUSHUSHA ABIRIA ENEO LOLOTE AMBALO LINAKUWA NA NAFASI YA KUFANYIA HIVYO.
ALISEMA KUTOKANA NA HATUA HIYO ASKARI WA USALAMA BARABARANI WAMEKUWA WAKIWAKAMATA NA KUWATOZA KIASI CHA SHILINIG ELFU30 KWA KOSA NA WAKATI MWINGINE HADI THS 60,000.
AIDHA ALISEMA ASKARI HAO WAMEKUWA WAKIWABAMBIKIA MAKOSA MENGINE AMBAYO HAWAKUYAFANYA NA HIVYO KUTOA RUSHWA ILI WAWAACHE WAENDELEE NA SHUGHULI ZAO ZA KUBEBA ABIRIA.
" TUMEKUWA TUKIKAMATWA NA ASKARI AMBAO WAMEKUWA WAKITUOMBA RUSHWA KAMA HUTAKI KUTOA UNABAMBIKIWA MAKOSA AMBAYO HUJAYAFANYA NA UKIPELEKWA POLISI KOSA MOJA KISHERIA NI TSH ELFU 30, HUU NI UONEVU MKUBWA AMBAO TUNAFANYIWA NA HAWA TRAFIKI,"ALISEMA.
ALISEMA WAMEKUWA WAKIWAPA TRAFIKI KIASI CHA THS 5000 HADI 20,000 ENDAPO WATAKAMATWA ILI KUSAMEHEWA KULIPA FAINI YA TSH 30 AMBAYO IMEANISHWA KISHERIA KWA KILA KOSA.
DEREVA HUYO ALISEMA MADEREVA AMBAO WAMEKUWA WAKIENDESHA GARI ZINAZOMILIKIWA NA TRAFIKI WAMEKUWA WAKIKOSA USUMBUFU WA TRAFIKI HAO KWA KUWA WAMEKUWA WAKIJUANA.
No comments:
Post a Comment