NA MWANDISHI WETU, TANZANIASASA
SHIRIKA la nyumba la Taifa (NHC), limeingia mkataba wa bilioni 5 na Halmashauri ya wilaya ya Monduli kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Halmashauri hiyo kwa lengo la kuwaondolea adha ya
Akitoa taarifa ya ujenzi wa nyumba hizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo, jana wilayani Monduli , Kaimu Mkurugenzi wa ujenzi wa shirika la nyumba la Taifa, Mhandisi Benedict Kilimba alisema shirika la nyumba limeshatenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya ujenzi huo ambao unatarajiwa kuanza mapema Oktoba mwaka huu.
Alisema Halmashauri ya Monduli imetenga maeneo mawili ikiwemo la ekari 1.8 na eneo lingine lenye ukubwa wa ekari tatu ambapo kwa pamoja zitajengwa nyumba za ghorofa moja moja zitakazo kuwa na uwezo wa kukaliwa na familia 40.
“ Pia halmashauri imetupatia eneo lingine lenye ukubwa wa ekari 11 ambazo pia tutajenga nyumba ambazo tutaziuza kwa wananchi wa Monduli na maeneo ya jirani na zitakazobakia tutazipangisha kwa wale
watakaohitaji huduma hiyo,”alisema Kilimba.
Aidha alisema shirika hilo liko kwenye mikakati ya kuanza ujenzi wa miji mwili ya kisasa (satellite Town), jijini Arusha katika eneo la Matevez na Usa river wilayani Arumeru ambayo itakuwa na huduma zote za
kijamii ikiwemo soko la kisasa.
“Shirika limeshapata maeneo mawili jijini Arusha ambayo tunatarajia kuanza ujenzi wa miji ya kisasa ‘satelite town’, katika eneo la Matevez shirika limeshapata eneo la ukubwa wa ekari 500 ambapo
zitajengwa nyumba zaidi ya 7000 na katika mji wa Usa-river shirika limepata eneo la ukubwa wa ekari 3000 na tunatarajia kujenga nyumba zaidi ya 3000,”alisema.
Alisema katika wilaya ya Longido, shirika hilo litajenga nyumba 58 ambapo ujenzi unatarajiwa kuanza Septemba 15 mwaka huu na kwamba wilayani Karatu shirika hilo limepewa ekari 200.
Akizungumzia ujenzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alitoa wito kwa wakazi wa miji ambapo ujenzi wa nyumba hizo unatarajiwa kujengwa kuonyesha ushirikiano kwa shirika hilo kwa lengo la
kufanikisha miradi hiyo kukamilika kwa wakati.
Pia alitoa wito kwa watendaji wa Halmashauri ambazo bado hazijatenga maeneo ya ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika hilo kutenga maeneo hayo haraka ili kuwaondolewa wakazi wa maeneo hayo
ikiwemo wafanyakazi usumbufu wa ukosefu wa nyumba za kupanga.
No comments:
Post a Comment