Wafanyabiashara ndogondogo wa mafuta ya alizeti washamiri stendi ya mabasi singida. Hapa wakionekaba wakiuza mafita kwa abiria wa basi la igembe nsabo kama walivyonaswa na mpiga pivha wetu leo |
WAPENDWA KARIBUNI KATIKA BLOGU YENU MPYA YA TANZANIASASA KWA HABARI MOTOMOTO NA MATUKIO YA KILA SIKU...KWA MAWASILIANO YA MATANGAZO, HABARI KATIKA PICHA, MAONI NA USHAURI, WASILIANA NASI KUPITIA tanzaniasasa@gmail.com au simu:+255 787453855 au +255754000741, karibuni sana!!!
Tuesday, November 26, 2013
biashara ya mafuta ya alizeti yashamiri stendi ya mabasi singida
Sunday, November 24, 2013
TMF YAKUTANISHA WAANDISHI WATEULE WA KUFANYA HABARI ZA UCHUNGUZI DODOMA HOTEL
Mhariri wa gazeti la jamboleo Ebenezer mende akizungumza na mmoja wa washiriki wa mafunzo ya waandishi wa habari za uchunguzi yanayotaiiwa kuanza hivi karibuni
Thursday, November 21, 2013
RC Arusha aagiza OCD kumtia mbaroni diwani kata ya olasiti
Mkuu wa mkoa wa arusha magesa mulongo akitoa agizo kwa mkuu wa wilaya akhakikishe diwani wa kata ya olasiti ismail katamboi anakamatwa kwa kuzuia mradi wa maji usipite ktk kata yake |
Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya vest construction ltd samwel Lugemalila akimweleza mkuu wa mkoa maendeleo ya mradi huo wa maji wa km15 na changamoto ambazo amekuwa akikabiliana nazo |
Sehemu ya mtaro unaotarajiwa kurandazwa mabomba kupeleka maji kijiji cha lukudivinyi kisongo wilayani arumeru |
Tuesday, November 19, 2013
NYALANDU AJITOSA KUINUA VIPAJI VYA WANARIADHA SINGIDA, PIA NI KWAAJILI YA KUHAMASISHA KUPINGA UJANGILI
wanariadha wakiwa njiani kuelekea kumalizia mbio hizo |
Mkurugenzi wa Afrika Wildlife Fund, Pratik Patel akagana na mshindi wa kwanza katika mbio za nusu marathoni Paul Itambo baada ya kumkabidhi zawadi zake |
Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo Paul Itambo akimaliza mbio za km21 |
NA SEIF MANGWANGI, SINGIDA
ZAIDI ya wakimbiaji 400 kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Singida juzi
walishiriki mbio za kwanza za nusu marathoni Mkoani humo zikiwa na lengo kuu l
a kunyanyua vipaji vya wakimbiaji vijana sanjari na kuhamasisha vijana kwenye mapambano dhidi ya ujangili wa tembo nchini.
a kunyanyua vipaji vya wakimbiaji vijana sanjari na kuhamasisha vijana kwenye mapambano dhidi ya ujangili wa tembo nchini.
Katika mbio hizo zilizoandaliwa na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii,
Lazaro Nyalandu kwa upande wa wanaume, mkimbiaji, Paul Itambo aliibuka kidedea kwa
kukimbia kwa saa 1:10 na kuzawadiwa fedha Taslimu Tsh300,000, huku kwa upande
wa wanawake Fabiola William aliishinda kwa kutumia saa1:53 na kuzawadiwa
Tsh300,000.
Mbio hizo
zilizoanzia katika kijiji cha Mitula Darajani na kuishia katika shule ya msingi Ntunduu,
Singida Vijijini, Samuel
Ikungi aliibuka mshindi wa tatu katika mashindano hayo na Emmanuel Samson
alishinda nafasi ya tatu huku kwa upande wa wanawake, Winfrida Hassan aliibuka
kidedea katika nafasi ya pili na Zakhia
Abdallah alishika nafasi ya tatu.
Kwa upande
wa wanaume, mbio za kilometa tano Gabriel Galado aliibuka mshindi, akifuatiwa na Deo Lazaro nafasi ya pili na Jonas
John aliibuka nafasi ya tatu huku kwa wanawake Neema Kisunda aliibuka mshindi
katika mbio hizo za kilometa tano akifuatiwa na Pascalia Sylvester.
Katika mbio
za kilometa mbili na nusu upande wa wanawake, Julitha Anthony aliibuka mshindi
akifuatiwa na Editha Gabriel na Margret Benado, huku upande wa wanaume Petro
Pascal aliibuka mshindi akifuatiwa na Baraka Sebastian nafasi ya pili na Haji
Swalehe alishika nafasi ya tatu.
Akizungumza kwa Niabu ya Naibu Waziri, Nyalandu, Mkurugenzi wa shirika la
Afrika Wildlife Trust(AWT), ambae ni mwanzilishi wa matembezi ya kupinga
ujangili wa tembo nchini katika matembezi aliyoyafanya kutoka Arusha hadi Dar
es salaam, Pratic Patel aliwataka wazazi kuhamasisha vijana kushiriki kwenye
mchezo wa riadha ili kuitagnaza Tanzania.
Pratik alisema Mkoa wa Singida umekuwa kinara wa mbio mbalimbli nchini
hivyo ni wakati wa wazazi na wadau mbalimbali kuwekeza katika mchezo huo mkoani
humo ili waweze kushiriki michuano mikubwa duniani na kuitangaza Tanzania kwa
kuleta ushindi katika mbio watakazo shiriki.
“Riadha ni mchezo ambao utawapatia ajira vijana wengi hasa hapa Singida,
ni wakati sasa kwa wazazi na wafadhili wengine kote nchini kujitokeza kudhamini
riadha ili vijana watakaopatikana waweze kushiriki michuano mikubwa ulaya na
kuiletea sifa Tanzania,”alisema.
Pratik alisema Tanzania imekuwa katika tishio la kupotea kwa wanyamapori
maarufu ikiwemo Tembo hivyo vijana wanapaswa kuwa mabalozi wazuri wa kupingana
na ujangili huo kwa kuwataja watu wanaohusika ili vyombo vya sheria viweze
kuwachukulia hatua za kisheria.
Ends…
Monday, November 18, 2013
WABUNGE EALA WAMPONGEZA RAIS KIKWETE KUHUSU JUMUIYA HIYO
MAHAKAMA ZA KIMATAIFA ZATAKIWA KUSHITAKI WAHALIFU MAHAKAMA YA AFRIKA
Na seif mangwangi, AICC, ARUSHA
Rai hiyo imetolewa leo na waziri mkuu, mizengo Pinda,,alipokuwa akifungua kongamano la kwanzala majaji linalojadili kuwepo msingi imara wa kuteteanakulinda la haki za binadamu kutokana na ukiukwajiunaofanywa katika mataifa mbalimbali.
Amesema kuwa kongamano hilolinaloshirikisha majaji ambao ni wakuu wa vyombo vya kutoa haki ndani ya nchi, mahakamaza kikanda ,mahakama ya afrika na nje kuangaliajinsi wanavyoweza kushirikiana pamoja katika kuangalia swala zima la ulinzi nautetezi wa haki za binadamu.
Pinda, amesema kuwa Tanzania iko msitari wa mbelekutekeleza na kulinda haki za binadamu na imeridhia mikata mbalimbali naitifaki(Protocal) mbalimbali ili kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa .
Amesema kuwa eneo ambalo halijapea nafasi kubwa ni wakati gain kunakuwepo na ukiukwaji wa haki za binadamu ,mashirika au mtu mmoja mmoja anaenda mahakamani kudai haki hizo pindi zinapokiukwa.
Pinda amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 7 zilizoridhia kulindwa kwa haki za binadamu kati ya 26 barani afrika zilizosainimkataba wa kuanzishwa kwa mahakama ya afrika ambayo imetoa uhuru kwa mshirika yasiyokuwa ya kiserikali kwenda mahakamani kudai haki pale zinapokwa .
Kwa upande wake Jaji mkuu Mohamed Othman Chande, amesema kuwa kongamano hilo ni la kwanza tangia kuanzishwa kwa mahakama ya afrika.
alisema katika kongamano hilo majaji mbalimbali majaji wamekutanishwa ikiwemo wa mahakama za kikanda na mahakama ya afrika na za kimataifa na kwamba msingi mkubwa ukiwa ni kujadili namna ya majaji wanavyoweza kushirikiana kutafisiri masharti ya haki za bindamu.
Jaji, Chande amesema haki za binadamu zimekuwa zikilindwa katika katiba za mataifa mbalimbali na kila mahakama ya nchi husika imekuwa ikizitafisiri haki za binadamu kulingana na mazingira yake .
Amesema kuwa kuna maamuzi ya kikanda kwa kila nchi , kimataifa ,ambapo kila mtu ana haki ya kuishi na haki hiyo ipo katika mikataba ambayo imeridhiwa na nchi 26 barani afrika ambapo Tanzania katika kutekeleza hilo imekubali mtu yeyote, kikundi chochote kwenda mahakamani kudai haki za binadamu pindi zikikiukwa.
Awali rais wa mahakama ya afrika, Sophia Akufo, amesema ni lazima haki za jamii na watoto zilindwe.
Akasisitiza kuwa ni muhimu kuzingatiwa kwa haki za binadamu na katiba za mataifa mbalimbali na zilindwe ili kudumisha utawala bora na wa kidemokrasia unaozingatia sheria
Amesema kuwa kongamano hilo linatoa mwelekeo na mtizamo wa siku zijazo wa kuboresha utawala wa sheria na demokrasia ,uchumi na siasa nzuri zinazolinda haki za binadamu kulingana na mikataba na maazimio na matamko mbalimbali ya kimataifa kuhusu haki za binadamu.
Friday, November 15, 2013
MASHINDANO YA ARUSHA GOLF OPEN CHINI YA UDHAMINI WA LODHIA GROUP OF COMPANY YAMALIZIKA
Mwenyekiti wa arusha golf mustafali kushoto akimkabidhi zawadi mwenyekiti arusha gymkhana dkt freezby baada ya kuibuka mmoja wa washindi kwenye mashindano ya arusha open |
Mwenykiti wa kampuni za Lodhia Harun Lodhia katikati akiwa na Mwenyekiti wa Golf Arusha Mustafali kushoto katika michuano hyo iliyomalizika hivi karibuni Arusha |
Harun Lodhia akipiga mpira katika mashindano hayo |
Harun Lodhia akiingiza mpira kwenye shimo |
Mwenyekiti wa kampuni za Lodhia, Harun Lodhia akipiga mpira wa Golf kuingiza ndani ya shimo katika mashindano hayo ambayo aliibuka mshindi wa nne |
Mwenyekiti wa Golf Arusha Mustafal akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo na kutaja washindi |
Mwenyekiti wa Kampuni za Lodhia duniani, Harun Lodhia akimkabidhi mshindi wa kwanza ambae pia ni mwenyekiti wa GOlf Arusha Mustafali Kikombe |
Mwenyekiti wa Makampuni ya Lodhia Harun Lodhia akimkabidhi Mwenyekiti wa Golf Arusha Mustafal zawadi ya mshindi wa kwanza katika mashindano hayo |
Mwenyekiti wa GOLF Arusha Mustafal akifurahia zawadi ya seti ya televisheni aina ya Sumsung kwa kuibuka mshindi katika mashindano hayo |
Jimmy akipokea zawadi kutoka kwa JATN |
NA SEIF MANGWANGI, GHMKHANA ARUSHA
MASHINDANO ya wazi ya mchezo wa Gofu kanda ya Arusha (Arusha Open Golf), yamemalizika jana jijini hapa kwa mchezaji Muzaffar Yusufali kuibuka mshindi wa kwanza wa jumla kati ya wachezaji 78 waliojitokeza kwenye mashindano hayo yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Gykhana jijini hapa.
Katika mashindano hayo yaliyofanyika kwa siku mbili na kudhaminiwa na kampuni ya Lodhia (Lodhia Group of Campanies), Muzaffar alizawadiwa seti ya luninga aina ya Sumsang nchi32, nafasi ya pili ilishikwa na Francis Julius na kuzawadiwa jiko la kupikia, na nafasi ya tatu ilishikwa na Piniel Uliwa na kuzawadiwa seti ya Radio.
Nafasi ya nne ilishikiliwa na Mwenyekiti wa makampuni ya Lodhia (Lodhia Group of Campanies), ambae pia ni mdhamini wa mashindano hayo, Haroun Lodhia na kukabidhiwa Microwave, lakini hata hivyo zawadi hiyo aliitoa kwa mshindi wa tano kutoka timu ya TPC, Frank Roman.
Kwa mujibu wa Rais wa Gold Tanzania, Paul Matinez, Jimmy Mollel aliibuka kidedea kwenye kundi la washindi waliocheza bila kutoa (Gross winner) aliyezawadiwa seti ya radio , akifuatiwa na Issack Wanyeche
aliyezawadiwa Microwave.
“Mshindi kundi la wanawake (Lady Winner), alikuwa ni Madina Iddi aliyepewa Dish, na mshindi kundi la vijana wadogo(Junior) aliibuka James Samweli wa timu ya TPC Moshi na kuzawadiwa Dish, huku kundi la
wachezaji wakongwe (Senior winner), aliibuka kidedea Harbar Janshadar ambae pia alizawadiwa Dish,”alisema Martinez.
Akizungumzia mashindano hayo Matinez ambae pia ni diwani wa kata ya Moshono, alisema mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka yalikuwa yafanyike Aprili mwaka huu lakini kutokana na ukosefu wa udhamini yalishindwa kufanyika.
Alisema baada ya kuona hivyo, walimtafuta mdhamini kampuni ya Lodhia kwa kushirikiana na kampuni ya kimataifa ya usanifu wa madini ya Diamond International yenye ofisi zake jijini hapa kwa pamoja
walikubali kutoa ufadhili wao.
Kwa upande wake mdhamini wa mashindano hayo Mwenyekiti wa makampuni ya Lodhia, Haroun Lodhia alisema kampuni yake kwa kushirikiana na Diamond International imeamua kusaidia mchezo wa Golf nchini ili kusaidia na Serikali kuutangaza mchezo huo kimataifa.
Subscribe to:
Posts (Atom)