Na seif mangwangi, AICC, ARUSHA
Rai hiyo imetolewa leo na waziri mkuu, mizengo Pinda,,alipokuwa akifungua kongamano la kwanzala majaji linalojadili kuwepo msingi imara wa kuteteanakulinda la haki za binadamu kutokana na ukiukwajiunaofanywa katika mataifa mbalimbali.
Amesema kuwa kongamano hilolinaloshirikisha majaji ambao ni wakuu wa vyombo vya kutoa haki ndani ya nchi, mahakamaza kikanda ,mahakama ya afrika na nje kuangaliajinsi wanavyoweza kushirikiana pamoja katika kuangalia swala zima la ulinzi nautetezi wa haki za binadamu.
Pinda, amesema kuwa Tanzania iko msitari wa mbelekutekeleza na kulinda haki za binadamu na imeridhia mikata mbalimbali naitifaki(Protocal) mbalimbali ili kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa .
Amesema kuwa eneo ambalo halijapea nafasi kubwa ni wakati gain kunakuwepo na ukiukwaji wa haki za binadamu ,mashirika au mtu mmoja mmoja anaenda mahakamani kudai haki hizo pindi zinapokiukwa.
Pinda amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 7 zilizoridhia kulindwa kwa haki za binadamu kati ya 26 barani afrika zilizosainimkataba wa kuanzishwa kwa mahakama ya afrika ambayo imetoa uhuru kwa mshirika yasiyokuwa ya kiserikali kwenda mahakamani kudai haki pale zinapokwa .
Kwa upande wake Jaji mkuu Mohamed Othman Chande, amesema kuwa kongamano hilo ni la kwanza tangia kuanzishwa kwa mahakama ya afrika.
alisema katika kongamano hilo majaji mbalimbali majaji wamekutanishwa ikiwemo wa mahakama za kikanda na mahakama ya afrika na za kimataifa na kwamba msingi mkubwa ukiwa ni kujadili namna ya majaji wanavyoweza kushirikiana kutafisiri masharti ya haki za bindamu.
Jaji, Chande amesema haki za binadamu zimekuwa zikilindwa katika katiba za mataifa mbalimbali na kila mahakama ya nchi husika imekuwa ikizitafisiri haki za binadamu kulingana na mazingira yake .
Amesema kuwa kuna maamuzi ya kikanda kwa kila nchi , kimataifa ,ambapo kila mtu ana haki ya kuishi na haki hiyo ipo katika mikataba ambayo imeridhiwa na nchi 26 barani afrika ambapo Tanzania katika kutekeleza hilo imekubali mtu yeyote, kikundi chochote kwenda mahakamani kudai haki za binadamu pindi zikikiukwa.
Awali rais wa mahakama ya afrika, Sophia Akufo, amesema ni lazima haki za jamii na watoto zilindwe.
Akasisitiza kuwa ni muhimu kuzingatiwa kwa haki za binadamu na katiba za mataifa mbalimbali na zilindwe ili kudumisha utawala bora na wa kidemokrasia unaozingatia sheria
Amesema kuwa kongamano hilo linatoa mwelekeo na mtizamo wa siku zijazo wa kuboresha utawala wa sheria na demokrasia ,uchumi na siasa nzuri zinazolinda haki za binadamu kulingana na mikataba na maazimio na matamko mbalimbali ya kimataifa kuhusu haki za binadamu.
No comments:
Post a Comment