wanariadha wakiwa njiani kuelekea kumalizia mbio hizo |
Mkurugenzi wa Afrika Wildlife Fund, Pratik Patel akagana na mshindi wa kwanza katika mbio za nusu marathoni Paul Itambo baada ya kumkabidhi zawadi zake |
Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo Paul Itambo akimaliza mbio za km21 |
NA SEIF MANGWANGI, SINGIDA
ZAIDI ya wakimbiaji 400 kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Singida juzi
walishiriki mbio za kwanza za nusu marathoni Mkoani humo zikiwa na lengo kuu l
a kunyanyua vipaji vya wakimbiaji vijana sanjari na kuhamasisha vijana kwenye mapambano dhidi ya ujangili wa tembo nchini.
a kunyanyua vipaji vya wakimbiaji vijana sanjari na kuhamasisha vijana kwenye mapambano dhidi ya ujangili wa tembo nchini.
Katika mbio hizo zilizoandaliwa na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii,
Lazaro Nyalandu kwa upande wa wanaume, mkimbiaji, Paul Itambo aliibuka kidedea kwa
kukimbia kwa saa 1:10 na kuzawadiwa fedha Taslimu Tsh300,000, huku kwa upande
wa wanawake Fabiola William aliishinda kwa kutumia saa1:53 na kuzawadiwa
Tsh300,000.
Mbio hizo
zilizoanzia katika kijiji cha Mitula Darajani na kuishia katika shule ya msingi Ntunduu,
Singida Vijijini, Samuel
Ikungi aliibuka mshindi wa tatu katika mashindano hayo na Emmanuel Samson
alishinda nafasi ya tatu huku kwa upande wa wanawake, Winfrida Hassan aliibuka
kidedea katika nafasi ya pili na Zakhia
Abdallah alishika nafasi ya tatu.
Kwa upande
wa wanaume, mbio za kilometa tano Gabriel Galado aliibuka mshindi, akifuatiwa na Deo Lazaro nafasi ya pili na Jonas
John aliibuka nafasi ya tatu huku kwa wanawake Neema Kisunda aliibuka mshindi
katika mbio hizo za kilometa tano akifuatiwa na Pascalia Sylvester.
Katika mbio
za kilometa mbili na nusu upande wa wanawake, Julitha Anthony aliibuka mshindi
akifuatiwa na Editha Gabriel na Margret Benado, huku upande wa wanaume Petro
Pascal aliibuka mshindi akifuatiwa na Baraka Sebastian nafasi ya pili na Haji
Swalehe alishika nafasi ya tatu.
Akizungumza kwa Niabu ya Naibu Waziri, Nyalandu, Mkurugenzi wa shirika la
Afrika Wildlife Trust(AWT), ambae ni mwanzilishi wa matembezi ya kupinga
ujangili wa tembo nchini katika matembezi aliyoyafanya kutoka Arusha hadi Dar
es salaam, Pratic Patel aliwataka wazazi kuhamasisha vijana kushiriki kwenye
mchezo wa riadha ili kuitagnaza Tanzania.
Pratik alisema Mkoa wa Singida umekuwa kinara wa mbio mbalimbli nchini
hivyo ni wakati wa wazazi na wadau mbalimbali kuwekeza katika mchezo huo mkoani
humo ili waweze kushiriki michuano mikubwa duniani na kuitangaza Tanzania kwa
kuleta ushindi katika mbio watakazo shiriki.
“Riadha ni mchezo ambao utawapatia ajira vijana wengi hasa hapa Singida,
ni wakati sasa kwa wazazi na wafadhili wengine kote nchini kujitokeza kudhamini
riadha ili vijana watakaopatikana waweze kushiriki michuano mikubwa ulaya na
kuiletea sifa Tanzania,”alisema.
Pratik alisema Tanzania imekuwa katika tishio la kupotea kwa wanyamapori
maarufu ikiwemo Tembo hivyo vijana wanapaswa kuwa mabalozi wazuri wa kupingana
na ujangili huo kwa kuwataja watu wanaohusika ili vyombo vya sheria viweze
kuwachukulia hatua za kisheria.
Ends…
No comments:
Post a Comment