Chifu wa Kasulu Kigoma, Isambe Gilbert Isambe |
Chifu wa Kasulu mkoani Kigoma Isambe G. Isambe wa kwanza kushoto, Chifu wa Old Moshi, Gerald Madara |
Na Seif Mangwangi, Arusha
TAMASHA kubwa la utamaduni
linalokutanisha zaidi ya machifu 120 wa kabila mbalimbali nchini, linaanza leo
katika uwanja wa mpira wa miguu wa Shekh Amri Abeid jijini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari
jana jijini hapa, Mkurugenzi wa kampuni ya Utamaduni Training, Janeth Jonas alisema
tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza nchini likiwa na lengo la kuenzi
utamaduni wa Mtanzania kwa vizazi vilivyopo.
Chifu wa Kasulu Kigoma Isambe G Isambe akiwa katika vazi la kitamaduni la jamii yake |
Alisema katika tamasha hilo la siku
tano linalotambulika kwa jina la ‘MTU KWAO’, washiriki zaidi ya 10,000
wanatarajiwa kushiriki ambapo shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwemo kuonyesha
mavazi, ngoma za asili za makabila hayo na elimu ya tamaduni zao.
Janeth alisema wasanii mbalimbali
watakuwepo kutumbuiza katika tamasha hilo ikiwemo Mrisho Mpoto, Jambo Squard,
Dogo Janja, Wema Sepetu, Roma Mkatoliki,Weusi na Daniel Sekuo kutokana nchini Kenya.
“Mbali ya wasanii hawa pia kutakuwa
na ngoma za asili kwa kila kabila ikiwemo ngoma ya Mtingo kutoka Moshi,
Hadzabe, Maasai, Datoga n.k, lakini pia kutakuwa na tamaduni mbalimbali
zitakazoonyeshwa,”alisema.
Alisema siku ya mwisho ya kilele
cha Tamasha hilo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti ambae pia ni Chifu
katika jamii yake anatarajiwa kuwa mgeni rasmi ambapo shughuli mbalimbali pia
zitafanyika.
Kwa upande wake chifu kutoka wilaya
ya Kasulu, Mkoa wa Kigoma, Isambe Isambi
alisema Tamasha hilo linafanyika ikiwa ni kukumbusha watanzania utamaduni wao
ambapo miongoni mwa shughuli zitakazofanyika ni pamoja na kutoa elimu ya
tamaduni ambazo zinaweza kuendelea kuenziwa na kuondoa ambazo zimepitwa na
wakati.
No comments:
Post a Comment