WASHIRIKI WAKIMSIKILIZA MWAKILISHI WA TANAPA ALIPOKUWA AKITOA SALAMU ZA SHIRIKA HILO |
WAANDISHI WAKIFUATILI SALAMU KUTOKA KWA WADAU MBALIMBALI IKIWEMO TANAPA |
WAANDISHI WAKOGWE WAKIONGOZWA NA EDA SANGA WA KWANZA KUSHOTO WAKIFUATIA HOTUBA ILIYOKUWA IKITOLEWA NA WAWAKILISHI WA MASHIRIKA YA TANAPA NA NCAA |
MENEJA MAWASILIANO WA TANAPA, PASCAL SHELUTETE AKITOA SALAMU ZA TANAPA |
NA MWANDISHI WETU, ARUSHA
WAANDISHI wa habari wameelezwa kuwa
na nafasi kubwa ya kuzuia matukio ya ujangili yanayoendelea kwa kasi nchini
jambo ambalo linaweza kuathiri shughuli mbalimbali za maendeleo ya Taifa
kutokana na pato linalopatikana kutokana na sekta hiyo.
Wito huo umetolewa leo jijini hapa
na Mkurugenzi wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi katika
salamu zake zilizowasilishwa kwa niaba yake na Meneja mawasiliano wa shirika
hilo Pascal Shelutete katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari
Duniani.
Shelutete alisema ujangili umekuwa
ni jambo ambalo linapaswa kupingwa na kila mtanzania katika sekta aliyokuwepo
badala ya kuiachia Tanapa kwa kuwa hifadhi za Taifa zimekuwa zikiliingizia
Serikali mapato mengi ambayo yamekuwa yakitumika kwenye shughuli za maendeleo.
“Waandishi wa habari naombeni
muungane na Tanapa na serikali kwa ujumla kupambana na vita dhidi ya ujangili,
tunajua nguvu ambayo mmekuwa nayo kupitia kalamu zenu, hii ni vita mbaya kwa
kuwa inahatarisha uhai wa nchi,”alisema Shelutete.
Alisema mchango wa waandishi wa
habari unaotikana na uandishi mzuri kuhusu hifadhi za Taifa umekuwa ukionekana
kutokana na wageni wengi kufika nchini kutembelea hifadhi hizo na kuiingizia
Serikali mapato mengi
Shelutete alitoa wito kwa waandishi
kuendelea kuandika taarifa mbalimbali za hifadhi za Taifa ili kuvutia zaidi
wageni kuja nchini na kwamba shirika hilo litaendelea kushirikiana na waandishi
wa habari.
Kwa upande wake, Meneja mawasiliano
wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, Adam Akyoo alisema tunaposherehekea siku
ya uhuru wa vyombo vya habari ni wakati wa kutathmini visa na mikasa ambayo
waandishi wamekuwa wakikabiliana nayo.
Alitoa wito kwa mamlaka za Serikali
kuheshimu tasnia ya uandishi wa habari kwa kutoa sheria nzuri na ambayo itaweza
kueleza maudhuni mazuri ya tasnia hiyo nchini.
Ends…
No comments:
Post a Comment