·
wafanyabiashara
watakiwa kuanzisha kituo cha utalii wa chakula cha asili
Na
Seif Mangwangi, Tanzaniasasablog
WAFANYABIASHARA wametakiwa kubuni mbinu mpya ya kutangaza
sekta ya utalii nchini kwa kuanzisha vituo cha utalii wa vyakula vya asili ili
kuvutia watalii wanaotembelea jiji la Arusha kujionea vyakula hivyo na hatimaye
kupata mlo kamili wenye asili ya makabila ya Tanzania.
|
Mratibu wa Sensa mkoa wa Arusha Bi.Magreth Martin akizungumza na wadau
pamoja na wakazi wa jiji la Arusha waliofika kwenye tamasha hilo |
Rai hiyo inetolewa jana jijini hapa na Mratibu wa takwimu Mkoa wa Arusha, Magreth Martin katika hotuba
yake wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani iliyoazimishwa sambamba
na tamasha la chakula cha asili cha kiafrika (African food festival) chini ya uongozi
wa mgahawa wa umbrella.
Alisema Tanzania
imebarikiwa kuwa na aina mbalimbali za utalii ambazo zimekuwa zikivutia wageni wa
ndani na wengine kutoka nje ya nchi lakini hakuna kituo cha utalii wa vyakula
vya asili ambapo wageni mbalimbali wanaweza kutembelea na kupata chakula.
Magreth alisema tamasha
la chakula cha kiasili lililoandaliwa na uongozi wa Umbrella ni mfano mzuri wa
kuigwa na kutoa wito kwa uongozi huo kuangalia namna ya kuanzisha kituo rasmi
cha mapishi ya asili ili kuvutia wageni wa ndani na nje ya nchi wanaotembelea jiji
la Arusha kwa shughuli mbalimbali.
|
Meneja wa Saccos katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Christine Julius
akizunguka katika tamasha hilo |
“ Watanzania
tumebarikiwa kuwa na vivutio vingi sana vya utalii, lakini hatujaweza kuvitumia
ipasavyo, ninachowaomba watanzania wenzangu, embu angalieni namna bora ya
kuanzisha kituo cha utalii wa vyakula vya kiasili ili wageni wanaokuja Arusha
na watalii kutoka nje ya nchi waweze kujua makabila yetu kwa njia ya vyakula
lakini pia waweze kupata mlo mzuri kupitia vyakula hivyo,”alisema.
Alisema tunapoazimisha
siku ya wanawake duniani lazima tuangalie na namna ya kuwakumbuka na kutambua
umuhimu wao na kwamba maadhimisho hayo yaliyoenda sanjari na chakula cha asili
ni siku muhimu sana kwa kina mama.
“Naamini siku ya leo ni
muhimu sana, lakini isiishie tu kufanya
tamasha hili, itapendeza kama mtaanzisha kituo cha utalii wa chakula cha asili
ili wageni mbalimbali wanapokuja arusha waweze kupata chakula halisi na
kujionea utamaduni wa mtanzania, hata kama ni nyie umbrella fanyeni, hii
itawajengea heshima sana,”alisema Magreth.
Mkurugenzi wa mgahawa
wa Umbrella, Elihuruma Msengi alisema huwezi kumkumbuka Mwanamke kama
hutotambua majukumu yake katika jamii ikiwemo utayarishaji wa chakula cha asili
ili kuhakikisha afya ya familia yake inakuwa bora na imara.
Alisema wameamua
kuanzisha tamasha hilo la chakula cha asili kwa lengo la kuonyesha umuhimu wa
vyakula hivyo kwa afya ya binaadam na kuhamasisha jamii kuacha kutumia vyakula
vyenye kemikali ambavyo vimekuwa vikielezwa kuchangia maradhi mengi katika afya
ya binaadam.
“Uongozi wa Umbrella umepanga
kufanya tamasha hili mara kwa mara ili kuwahamasisha watanzania matumizi ya vyakula vya asili
lakini pia tunachukua mawazo ya Mama yetu kuona namna ya kuanzisha kituo cha
utalii wa vyakula vya asili ili na wageni wanaotembelea nchini waweze kuona
asili yetu katika chakula,”alisema.
Katika tamasha hilo
lililovutia wakazi wengi wa jiji la Arusha, watu walipata nafasi ya kula
vyakula mbalimbali vya asili kama vile mlenda kwa makabila ya kanda ya kati na
pwani, loshoro inayoliwa na wamaasai, matoke, kisamvu, supu ya pweza, bada, maghimbi, maboga, mihogo,viazi, .
|
wakazi wa Jiji la Arusha waliofika wakichukua chakula |
|
Wakazi wa Jiji la Arusha wakimsikilia mgeni rasmi Meneja wa Saccos ya Mkoa wa Arusha katika tamasha la chakula cha asili ya kiafrika katika mgahawa wa Umbrella |
|
wakazi wa Arusha waliofika kwenye tamasha la Africa Food Festival wakiteta |
|
mgeni rasmi katika Tamasha hilo Christine Julius akizungumza na wageni walifika katika tamasha hilo |
|
mfanyakazi wa kituo cha radio 5 cha jijini Arusha, Ashura Mohamed akipata chakula cha asili, mkononi akiwa kashikilia mlenda |
|
wadau wakipata chakula |
|
mtoto akishangaa chakula aina ya makande kinacholiwa na kabila la wapare |
|
mmoja wa wageni akipakuliwa mboga aina ya kisamvu |
|
mboga za aina mbalimbali kama hapa inavyoonekana ni dagaa waliopikwa kwa ustadi wa hali ya juu |
|
wakazi wa jiji la Arusha wakipakuliwa chakula cha aina mbalimbali |
|
mmoja ya wakazi wa jiji la Arusha ambae jina lake halikuweza kupatikana mara moja akipakua mchuzi wa pweza |
|
wafanyakazi wa kituo cha radio5 wakisubiri kupakua chakula |
|
Nyama choma pia ilikuwa ikipatikana katika tamasha hilo |
|
waandishi wa habari wakizungumza na uongozi wa mgahawa wa umbrella |
|
wasanii aika na nareel wakitumbuiza jukwaani katika tamasha hilo |
|
mkurugenzi wa umbrella garden, Elihuruma Msengi akizungumza kukaribisha wageni katika tamasha hilo |
|
wakazi wa arusha pia walipa fursa ya kuona nguo za asili katika tamasha hilo |
|
wadau wakiwa katika viwanja vya umbrella |