Monday, March 9, 2015

TAMASHA LA VYAKULA VYA ASILI LILIVYOFANA UMBRELLA GARDEN SIKU YA WANAWAKE

        ·       wafanyabiashara watakiwa kuanzisha kituo cha utalii wa chakula cha asili

Na Seif Mangwangi, Tanzaniasasablog

WAFANYABIASHARA  wametakiwa kubuni mbinu mpya ya kutangaza sekta ya utalii nchini kwa kuanzisha vituo cha utalii wa vyakula vya asili ili kuvutia watalii wanaotembelea jiji la Arusha kujionea vyakula hivyo na hatimaye kupata mlo kamili wenye asili ya makabila ya Tanzania.
Mratibu wa Sensa mkoa wa Arusha Bi.Magreth Martin akizungumza na wadau
pamoja na wakazi wa jiji la Arusha waliofika kwenye tamasha hilo

Rai hiyo inetolewa jana jijini hapa na Mratibu wa takwimu Mkoa wa Arusha, Magreth Martin katika hotuba yake wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani iliyoazimishwa sambamba na tamasha la chakula cha asili cha kiafrika (African food festival) chini ya uongozi wa mgahawa wa umbrella.


Alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na aina mbalimbali za utalii ambazo zimekuwa zikivutia wageni wa ndani na wengine kutoka nje ya nchi lakini hakuna kituo cha utalii wa vyakula vya asili ambapo wageni mbalimbali wanaweza kutembelea na kupata chakula.
Magreth alisema tamasha la chakula cha kiasili lililoandaliwa na uongozi wa Umbrella ni mfano mzuri wa kuigwa na kutoa wito kwa uongozi huo kuangalia namna ya kuanzisha kituo rasmi cha mapishi ya asili ili kuvutia wageni wa ndani na nje ya nchi wanaotembelea jiji la Arusha kwa shughuli mbalimbali.
Meneja wa Saccos katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Christine Julius
akizunguka katika tamasha hilo 
“ Watanzania tumebarikiwa kuwa na vivutio vingi sana vya utalii, lakini hatujaweza kuvitumia ipasavyo, ninachowaomba watanzania wenzangu, embu angalieni namna bora ya kuanzisha kituo cha utalii wa vyakula vya kiasili ili wageni wanaokuja Arusha na watalii kutoka nje ya nchi waweze kujua makabila yetu kwa njia ya vyakula lakini pia waweze kupata mlo mzuri kupitia vyakula hivyo,”alisema.
Alisema tunapoazimisha siku ya wanawake duniani lazima tuangalie na namna ya kuwakumbuka na kutambua umuhimu wao na kwamba maadhimisho hayo yaliyoenda sanjari na chakula cha asili ni siku muhimu sana kwa kina mama.
“Naamini siku ya leo ni muhimu sana,  lakini isiishie tu kufanya tamasha hili, itapendeza kama mtaanzisha kituo cha utalii wa chakula cha asili ili wageni mbalimbali wanapokuja arusha waweze kupata chakula halisi na kujionea utamaduni wa mtanzania, hata kama ni nyie umbrella fanyeni, hii itawajengea heshima sana,”alisema Magreth.
Mkurugenzi wa mgahawa wa Umbrella, Elihuruma Msengi alisema huwezi kumkumbuka Mwanamke kama hutotambua majukumu yake katika jamii ikiwemo utayarishaji wa chakula cha asili ili kuhakikisha afya ya familia yake inakuwa bora na imara.
Alisema wameamua kuanzisha tamasha hilo la chakula cha asili kwa lengo la kuonyesha umuhimu wa vyakula hivyo kwa afya ya binaadam na kuhamasisha jamii kuacha kutumia vyakula vyenye kemikali ambavyo vimekuwa vikielezwa kuchangia maradhi mengi katika afya ya binaadam.
“Uongozi wa Umbrella umepanga kufanya tamasha hili mara kwa mara ili kuwahamasisha  watanzania matumizi ya vyakula vya asili lakini pia tunachukua mawazo ya Mama yetu kuona namna ya kuanzisha kituo cha utalii wa vyakula vya asili ili na wageni wanaotembelea nchini waweze kuona asili yetu katika chakula,”alisema.
Katika tamasha hilo lililovutia wakazi wengi wa jiji la Arusha, watu walipata nafasi ya kula vyakula mbalimbali vya asili kama vile mlenda kwa makabila ya kanda ya kati na pwani, loshoro inayoliwa na wamaasai, matoke, kisamvu, supu ya pweza,  bada, maghimbi, maboga, mihogo,viazi, .  


wakazi wa Jiji la Arusha waliofika wakichukua chakula

Wakazi wa Jiji la Arusha wakimsikilia mgeni rasmi Meneja wa Saccos ya Mkoa wa Arusha katika tamasha la chakula cha asili ya kiafrika katika mgahawa wa Umbrella

wakazi wa Arusha waliofika kwenye tamasha la Africa Food Festival wakiteta

mgeni rasmi katika Tamasha hilo Christine Julius akizungumza na wageni walifika katika tamasha hilo

mfanyakazi wa kituo cha radio 5 cha jijini Arusha, Ashura Mohamed akipata chakula cha asili, mkononi akiwa kashikilia mlenda

wadau wakipata chakula

mtoto akishangaa chakula aina ya makande kinacholiwa na kabila la wapare 

mmoja wa wageni akipakuliwa mboga aina ya kisamvu

mboga za aina mbalimbali kama hapa inavyoonekana ni dagaa waliopikwa kwa ustadi wa hali ya juu

wakazi wa jiji la Arusha wakipakuliwa chakula cha aina mbalimbali

mmoja ya wakazi wa jiji la Arusha ambae jina lake halikuweza kupatikana mara moja akipakua mchuzi wa pweza

wafanyakazi wa kituo cha radio5 wakisubiri kupakua chakula 

Nyama choma pia ilikuwa ikipatikana katika tamasha hilo

waandishi wa habari wakizungumza na uongozi wa mgahawa wa umbrella

wasanii aika na nareel wakitumbuiza jukwaani katika tamasha hilo 
mkurugenzi wa umbrella garden, Elihuruma Msengi akizungumza kukaribisha wageni katika tamasha hilo 



wakazi wa arusha pia walipa fursa ya kuona nguo za asili katika tamasha hilo 


wadau wakiwa katika viwanja vya umbrella

No comments: