Na
Mwandishi Wetu, TANZANIASASA
MAMIA
ya wakazi wa jiji la Arusha, juzi walijitokeza katika uwanja mdogo wa ndege
Arusha kuwapokea watu walioandamana kwa kutembea kwa miguu kutoka Arusha hadi
jijini Dar es Salaa kupinga vitendo vya ujangili na biashara ya pembe za ndovu.
Maandamano
hayo yaliyozinduliwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo Agosti 24,
mwaka huu na kupokelewa jijini Dar es Salaam Septemba 12, mwaka huu na Naibu
waziri wa Utalii na Maliasili, Lazaro Nyalandu, yaliandaliwa na kuongozwa na
Mtanzania mwenye asili ya Asia, Pratik Patel kupitia Taasisi ya African
Wildlife Trust ya jijini Arusha.
Pamoja
na Patel, muandamanaji mwingine aliyeanzia safari yake kutoka Arusha katika
eneo la jengo la Mkuu wa mkoa hadi Dar es Salaam ni raia wa Marekani, Maraya
Cornel.
Akizungumza
mara baada ya mapokezi hayo, Patel aliwataka Watanzania wote kushiriki vita
dhidi ya ujangili na biashara ya pembe za ndovu kwani jukumu la ulinzi wa
marasilimali za taifa linahusu raia wote bila kujali tofauti zao kiuchumi,
kisiasa na kimaeneo (kikabila).
“Taasisi
kama Shirika la hifadhi za taifa (TANAPA) na Mamlaka ya bonde la Ngorongoro
(NCAA) na mamlaka zingine za serikali zimepewa tu dhamana ya kusimamia na
kuongoza shughuli za uhifadhi. Lakini ukweli ni kwamba sote tuna wajibu wa
kulinda rasilimali zetu kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo,” alisema Patel
Kwa
upande wake, mmoja wa waongoza watalii aliyehudhuria mapokezi hayo, Engbeth
Quorro aliwaomba viongozi serikalini na wale wa kisiasa kuwa na dhamira safi
katika usimamizi wa maliasili na rasilimali za taifa.
“Wote
wenye dhamira mbaya na rasilimali zetu wadhibitiwe mara moja bila kujali
nyadhifa zao hata itakapobainika kuwa miongoni mwao wamo viongozi wa serikali
au wanasiasa wenye ushawishi,” alisema Quorro
Awali
akizindua maandamano hayo wiki tatu zilizopita, Mkuu wa Arusha, Mulongo alisema
ni wajibu wa kila Mtanzania kushiriki vita dhidi ya ujangili kwa kutoa taarifa
zitakazosaidia kuwatia mbaroni wanaojihusisha na biashara haramu ya meno ya
tembo.
“Wahifadhi,
wasimamizi na watekelezaji wa sheria za uhifadhi watimize wajibu na majukumu
yao kwani wasipofanya hivyo hawatabaki salama katika msako dhidi ya majangili
unaoendelea,” alisema Mulongo
Kaimu
Mkuu wa Kikosi cha kupambana na ujangili Kanda ya Kaskazini, Michael Melakiti
alisema kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita pekee, watuhumiwa 64 wametiwa
mbaroni kwa makosa ya kujihusisha na ujangali katika kanda hiyo ambapo 51 kati
yao walipigwa faini ya Sh. 10.6 milioni.
Melakiti
alisema kipindi hicho kinachoanzia Juni mwaka jana hadi Juni mwaka huu,
watuhumiwa 11 walifikishwa mahakamani na kesi zao ziko katika hatua mbalimbali
huku mmoja akipewa onyo kwa maandishi.
Alisema
katika kipindi hicho, jumla ya Tembo 29 waliuawa na nyara zake kuchukuliwa na
majangili. Tembo hao waliuawa katika wilaya za Ngorongoro, Rombo, Monduli,
Longido na Simanjiro.
Licha
ya kukabiliwa na changamoto kadhaa, sekta ya utalii nchini inachangia asilimia
17 ya pato la taifa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment