Wednesday, September 18, 2013

UKARIMU WA WATANZANIA KWA WAGENI NI TATIZO KWA WAJASIRIAMALI - MKURUGENZI MPINGO SUMMIT


Mkurugenzi wa Global Skills Bakiri Angalia akifungua mafunzo ya wajasiriamali katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa AICC jijini Arusha hivi karibuni 

Kaimu Katibu Mkuu wizara ya habari na utamaduni Elisante,  akitoa mada katika mkutao huo 

Kutoka kushoto Mkurugenzi wa REPOA Professa Wangwe,  Mkurugenzi wa Kidot Love, Jocket Mwegelo, Mkurugenzi wa Global Skill na waandaaji wa mkutano wa MPIGO SUMMIT Bakili Angalia, Mkuu wa chuo cha MS-TCDC Dkt Kaare na MC maarufu nchini Taji Liundi wakimsikiliza kaimu Katibu Mkuu wizara ya Habari na utamaduni (hayupo pichani), Dkt Elisante alipokuwa akiwasilisha mada katika mkutano huo.


IMEELEZWA kuwa kutokuwa makini wafanyabiashara wa kitanzania na ukarimu wao dhidi ya wageni wanaokuja nchini kwa lengo la kuwekeza katika sekta mbalimbali ni hatari kwa maslahi ya nchi jambo linaloweza kusababisha kuporomoka kwa uchumi wa nchi.

Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Mkurugenzi wa kampuni ya Global Skill and education ya jijini Arusha, Bakiri Angalia katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa wajasiriamali na wafanyabiashara
unaofanyika jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC.

Angalia alisema viongozi wa nchi nyingi duniani wamekuwa wakiwaeleza wananchi wa nchi zao kuwekeza nchini kufuatia watanzania kuwa wakarimu katika Nyanja mbalimbali jambo ambalo ni hatari kwa uchumi wa nchi kufuatia wageni hao kutumia mwanya wa watanzania kutokuwa makini kufaidi tunu ya taifa.

Alisema uwekezaji ni jambo zuri ambalo kila kiongozi katika nchi analifurahia lakini hata hivyo wenyeji wanatakiwa kuwa makini  na uwekezaji huo kama ambavyo imekuwa ikifanyika katika nchi zingine
ikiwemo Kenya na Uganda.

“ Katika hotuba ya mmoja wa mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini alishawahi kusema kuwa kuwekeza Tanzania ni vizuri sana kwa kuwa watanzania ni wakarimu tofauti na nchi zingine kama za Kenya na Uganda, mimi binafsi nilisikitishwa sana na kauli hii kwa kuwa watanzania hatuko makini tunaweza kujikuta tunaumizwa kwa uwekezaji huo,”alisema.

Akiwakilisha mada katika mkutano huo, Mkuu wa chuo cha maendeleo cha MS-TCDC, Dkt.Suma Kaare alitoa wito kwa watafiti na wakufunzi katika vyuo vikuu mbalimbali nchini kufanya utafiti katika biashara za ndani ili kupata jibu la kutofanikiwa kwa wafanyabiashara hao.

“ Ukiwa shuleni utapata uzoefu kutoka biashara za wafanyabiashara wakubwa nje ya nchi lakini ni wakati sasa kwa wakufunzi na watafiti nchini kufanya utafiti wao kwa wafanyabiashara wa nchini ili kujua
tatizo ambalo limekuwa likisababisha kuanguka kwa biashara zao na kuwa somo kwa wafanyabiashara wengine,”alisema Dkt.Kaare.

Aliwataka wafanyabiashara kujifunza kwa wafanyabiashara wengine namana ambavyo wamefanya na kufanikiwa ili kuboresha biashara zao na kuvifanya kuwa endelevu.

No comments: