Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal Shelutete akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha |
Katika gazeti la Jamhuri Toleo Namba 129 Machi 25-31, 2014 kulikuwa na habari iliyoandikwa chini ya kichwa cha habari “Nyalandu ‘auza’ Hifadhi” ambapo maelezo ya habari hiyo yaliitaja Hifadhi ya
Taifa ya Katavi
kuwa inatarajiwa kukabidhiwa kwa wawekezaji kutoka nchini Afrika Kusini ikiwa
ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe…. Lazaro Nyalandu.
Shirika
la Hifadhi za Taifa linalosimamia Hifadhi ya Taifa ya Katavi pamoja na Hifadhi
nyingine 15 nchi nzima linapenda kukanusha habari hiyo iliyoandikwa kwa lengo
la kupotosha umma kama ifuatavyo.
Mosi,
hakuna mpango wala uamuzi wowote uliopo au uliokwisha kufanywa wa kuingia Mkataba
wa
Uendeshaji wa aina yoyote ile baina ya Shirika la Hifadhi za Taifa naMwekezaji yeyote kutoka
nchini Afrika ya Kusini ikiwa ni pamoja na African Parks Network waliotajwa
katika habari husika.
Pili,
Sheria inayosimamia uanzishwaji wa maeneo ya Hifadhi za Taifa ikiwemo Katavi
imelipa dhamana hii pekee shirika kusimamia maeneo haya kwa niaba ya Watanzania
na ni kinyume cha sheria kukabidhi kwa wawekezaji kwa ajili ya usimamizi kama
ilivyobainishwa katika habari hiyo.
Tatu,
Shirika la Hifadhi za Taifa bado linao uwezo thabiti wa kusimamia uendeshaji wa
Hifadhi ya Taifa ya Katavi ili kuhakikisha rasilimali za wanyama na mimea
zinaendelea kutunzwa kwa miaka mingi ijayo kama ambavyo imekuwa ikifanya tangu
kuanzishwa kwa hifadhi hiyo mwaka 1974.
Aidha,
kama ambavyo shirika limekuwa likipanga katika mipango yake ya maendeleo mwaka
hadi mwaka, katika mwaka mpya wa fedha ujao shirika limepanga kuongeza idadi ya
watalii katika Hifadhi za Kusini ikiwemo Katavi,Saadani,Mikumi na Ruaha.
Mkakati
huu utahusisha kuongeza ubora wa utoaji huduma ikiwa ni pamoja na malazi ili
kukuza utalii wa ndani. Shirika litafungua ofisi Jijini Dar es Salaam na
kuimarisha ofisi za Mwanza na Iringa ili watalii wapate taarifa za Hifadhi na
kuweza kufanya
‘bookings’
kwa urahisi. Aidha, kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa masoko ya nje, Shirika
sasa litaanzisha ‘Road shows’ mbalimbali kwa soko la ndani na nchi za jirani.
Vilevile, Shirika litaongeza kujitangaza kupitia Mitandao ya Jamii, TV,
majarida na tovuti ya Shirika itaboreshwa katika kuarifu wadau masuala
mbalimbali yanayojiri kwenye Hifadhi zetu.
Tayari
Shirika limeanzisha Kurugenzi mpya ya Utalii na Masoko kwa ajili ya kutekeleza
mkakati huu wa kuzifanya hifadhi za ukanda wa kusini kuvutia watalii wengi
zaidi.
Imetolewa
na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi
za Taifa Tanzania
30.03.2014
No comments:
Post a Comment