Na
Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Jeshi la Polisi
Mkoani hapa limemkamata mtu mmoja aitwaye Ally Rashid Salimu (23) mfanyabiashara wa pikipiki maarufu kama “Boda Boda” mkazi wa kata ya Sombetini
jijini hapa akiwa na bunduki aina ya shortgun Mossberg yenye namba T292166
ikiwa na risasi sita.
Akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake leo saa 5:30 asubuhi Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Liberatus Sabas alisema kuwa, tukio hilo lilitokea Aprili 28, mwaka huu saa 3:00 asubuhi katika
maeneo ya Shamsi jijini hapa.
Alisema siku ya
tukio dereva huyo wa pikipiki akiwa katika eneo hilo akiendesha pikipiki aina ya Skymark yenye namba za usajili T. 615 BZL huku akiwa amebeba
begi lililooonekana kutuna, askari Polisi walimshuku na kumsimamisha lakini alikataa na kukimbia.
Kamanda Sabas alisema askari hao walilazimika kumfukuza na hatimaye kumkamata na walipompekua walimkuta akiwa amebeba silaha hiyo aliyoihifadhi nadai ya begi alilokuwa amebeba.
“Mara baada ya
kufanikiwa kumkamata askari hao walipekua begi hilo na kukuta silaha hiyo ikiwa na
risasi sita na kisha kumfikisha mtuhumiwa huyo katika kituo kikuu cha polisi
cha hapa Arusha mjini”. Alifafanua Kamanda Sabas.
Kamanda Sabas
alisema upelelezi juu ya tukio hilo bado unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani
pindi utakapokamilika.
Tukio hilo la
ukamataji wa bunduki hiyo limekuja wiki tatu tu baada ya jeshi hilo kukamata
bastola moja pamoja na risasi 41 kutoka kwa watuhumiwa waliokuwa wanahusishwa
na matukio ya kumjeruhi Sister Mary Shobana na kisha kumnyang’anya fedha
taslimu Tsh 30,000,000/= (Milioni thelathini) eneo la Notre Dame Njiro lililopo
jijini hapa, fedha ambazo alitoka kuchukua benki ya Exim tawi la Shoprite.
No comments:
Post a Comment