mmoja wa majeruhi wa mabomu akiwa kalazwa katika hospitali ya mtakatifu Elizabeth jana akiendelea kupata matibabu |
Polisi nchini Tanzania
inawashikilia watu wa nane kwa madai ya
kuhusika na mlipuko wa siku ya jumapili katika kanisa Katoliki la Olasit
viungani mwa mji wa Arusha. Miongoni mwa washukiwa ambao wako mikononi
mwa polisi ni raia wanne wa Saudi Arabia, na wengine wanne ni raia wa
Tanzania.
Uchunguzi wa tanzaniasasa umebaini kuwa hadi jana idadi ya watu waliofari dunia kufuatia mlipuko huo
ni wawili na wala sio watatu kama ilivyoripotiwa hapo awali. Polisi
mjini Arusha vile vile wamethibitisha kuwa waliokufa wakati wa tukio
hilo la kigaidi ni watu wawili.
Kwa wakati huu polisi wanachunguza
ni kulipuzi aina gani kilitumika wakati wa shambulizi hilo.
Katika tukio hilo hakuna hasara yoyote iliyopatikana zaidi ya majeruhi walioumizwa katika mlipuko huo na vifo vya watu wawili..
Mlipuko huo uliotokea majira ya
saa tano asubuhi katika kanisa katoliki la Olasiti nje kidogo ya mji wa
Arusha nchini Tanzania na wengine kadhaa kujeruhiwa huku balozi wa papa
na watawa waliokuwa katika shughuli hiyo maalumu ya uzinduzi wa parokia
mpya ya mtakatifu Yosefu mfanyakazi wakinusurika pia.
No comments:
Post a Comment