Friday, May 10, 2013

PINDA AWAASA MADIWANI KUTOFANYA BIASHARA NA HALMASHAURI ZAO KUEPUKA KASHFA



 Na Mwandishi Wetu, Tanzaniasasa

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewakataza mameya wa majiji,wenyeviti wa halmashauri na madiwani  nchini kufanya biashara na halmashauri zao kwakua siku zte watajiingiza katika migogoro na kashfa za kutofikia kiwango bora cha miradi wanayotakiwa kuifanyia kazi.

Waziri Mkuu Pinda ametoa katazo hilo leo alipokua akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 29 wa jumuiya za serikali za mitaa unaofanyika katika hoteli ya Sundown Carnival jijini Arusha na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 500 kote nchini.

Alisema vionozi hao wa halmashauri hata kama watafuata taratibu zote katika kuifanya miradi watakayopewa na halmashauri zao kwa kwango gani lazima wataingia katika migogoro na halmashauri hizo kwakuaa wataaonekana wameshiniki kupata kazi hizo na kwamba ili kuepuka hayo ni vyema wakajitoa kuwaania kazi hizo.

Pinda alitolea mfano wa diwani mmoja katika haalmashauri moja hapa nchini ambaaye alipewa kesi yake ya kushindwa kufanya kazi aliyopewa na halmashauri yake na hivyo kujikuta katika matatizo makubwa kutokana na kazi hiyo.

Aidha amesema serikali imeshindwa kuzianzisha halmashauri nne mpya kati ya 37 zilizoazimiwa kuanzishwa kutokana na sababu mbalimbali alizozita za kitaalamu ikiwemo ya uchache wa kata katika halmashauri hizo hali inayozinyima sifa ya kuwa halmashauri.

Alisema sababu nyingine inayokwamisha kuanzishwa kwa halmashaauri hizo ni pamoja na kuhitajia kwa uchaaguzi kufanyika baada ya zilizopo kugawaanywa jambo ambalo madiwani wa kata zilizopo kutounga mkono jambo la kugawanywa kwa halmashauri hizo.

Alisema pamoja na kushindikana kwa halmashauri hizo nne tayari mchakato wa kuanzishwa kwa nyingine 33 umeshakamilika ikiwemo kusaini taratibu nzima za uanzishwaji wake kutokana na kukidhi vigezo vya kuanzishwa kwake ikiwemo wingi wa kata.

Alizitaja halmashauri hizo kuwa ni pamoja na Handeni,Tunduma,Nzega na Kasulu na kusisitiza kuwa pamoja na kuwepo kwa vikwazo hivyo serikali itahakikisha jambo hilo linafanyika kwakua tayari lilishaingizwa katika mpango na lazima litatekelezwa.

“unajua jambo hili linakua gumu kwasababu hiyo lakini mbali na hiyo pia zile kata tayari zina madiwani sasa unafikiri watakubali uchaguzi urudiwe baada ya kugawanywa kwa kata zao sasa wanasema hapana nyie serikali hamtutakii mema kwa jambo hili lakini hamna naamna tutaona jinsi ya kulifanya hili”alisema Pinda.

Pia amesifu mradi mpya unaoeneshwa na Tasaf katika halmashauri mbalimbali nchini wa kuwatambua watu masikini na kuwawezesha kwa namna mbalimbali ikiwemo kusomesha watoto wa familia hizo,kuwapatia huduma za afya na huduma za makazi ili kuwawezesha kuwa na maisha mazuri.

Aliwataka viongozi wa jumuiya ya ALAT katika mkutano wao mwingine kuishirikisha ofisi yake kwa karibu ili nae aweze kuchangia maoni mbalimbali aliyonayo badala ya kuwakusanya mawaziri wote kufika ili kutoa mada jambo ambalo lingewezekana kufanyika na ofisi yake.

Nae mwenyekiti wa ALAT taifa ambaye pia ni meya wa jiji la Dar es salaam Dk.Didas Masaburi alimwonga waziri mkuu kwa niaba ya serikali kuangalia namna ya kudhibiti vitendo vya kuondolewa wa mabavu kwa mameya na viongozi kwasababu za kisiasa.

Alisema ni lazima taratibu sahihi za kuondolewa kwa viongozi haao madarakani zifuatiliwe ikiwaa ni pamoja na tuhuma zinazomkabili kufikishwa kwa mkuu wa mkoa au waziri mwenye dhamana kwaajili ya kufanyiwa kazi baadaala yaa kukurupuka.

Alisema vitendo vya kukurupuka katika maamuzi ya kisiasa vinasababisha kudharaulika kwa viongozi hao pamoja na kusababisha kukosa mwamko katika kufanya kazi zao ambapo hata baadae huja kugundulika kuwa taarifa hizo hazikua za ukweli.

“hapahapa tu nawez kutolea mfano wa meya wa Bukoba ambaapo aalitolewa kisiasa halafu tume ikaundwa kuchunguza na baadae ikaja kugundulika kuwa tuhuma zilizokua zikielekezwa kwak hazikua za kweli sasa hii inakosa maana tuache hayo”alisema Masaburi.

Mwisho.

No comments: