Na Mwandishi Wetu,
Tanzaniasasa
ARUSHA
KIJANA mmoja wa
jamii ya kimasai Lomayani Mitewasi juzi alinusurika kupewa adhabu ya
kuchapwa viboko 70 aliyokuwa apewe na viongozi wa jamii hiyo baada ya
kutuhumiwa kusambaza taarifa ya uongo kwenye mitandao ya kijamii.
Adhabu nyingine
aliyokuwa apewe kijana huyo ambaye ni mkazi wa kata ya Elerai ni pamoja
na kulipa ng’ombe dume kwa kosa la kukiuka mila za kimasai kwa kutoa
taarifa za uongo
Mwenyekiti wa MAA akizungumza katika kikao hicho |
“Wazee wangu
naomba mnisamehe nilighafilika ninakiri kuandika habari za uongo katika
mitandao hiyo mimi binafsi sikijui kimasi huwa nina sikia neo mojamoja tuu japo
nilikuwepo kwenye mkutano uliopita sikujua hata mlizungumza nini kwa kuwa
mlikuwa mnazungumza kilugha”
Kwa mujibu wa
kijana huyo mbele ya malaigwanani alisema kuwa aliandika kuwa malaigwanani wagawanyika
katika makundi mawili moja linatetea CCM na Lingine CHADEMA jambo ambalo ni
uongo
Pia aliandika
Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Goodluck Ole Medeye
amewatumia malaigwanani kuvuruga uchaguzi mdogo wa Arusha
Mitewasi pia
aliandika kuwa kikao hicho kililenga kubagua wakazi wa Arusha kwa tofauti za
makabila yao, alilazimika kufuta kauli yake hiyo na kuomba radhi mbele ya
Malaigwanan hao kwa kile alichodai alighafilika
Awali akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari jana, Katibu wa Baraza la MAA, Amani Lukumay
alisema kuwa wazee hao wamesikitishwa sana na taarifa hizo za uongo
ambazo zilisambazwa katika mitandao ya kijamii ambayo ina lengo la
kuvuruga amani ya jiji la Arusha lakini pia kuwagawanya wazee hao
Lukumay alisema
kuwa lengo la kukutana kwa wazee hao wiki iliyopita ililikuwa na lengo la
kuzungumzia amani ya katika mkoa wa Arusha na kwamba hakuna kitu kingine
lichozngumzwa katika kikao hicho
“Onyo hili
halilengi chama chochote cha siasa, bali tunavionya vyama vyote vinavyofanya
shughuli za kisiasa Arusha kwa sababu Malaigwanan hatufungamani na itikadi za
vyama kwani miongoni mwetu wamo wanachama wa vyama tofauti vya kisiasa,”
alisema Amani.
Katibu huyo
alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya Malaigwanan hao waliokutana kwenye
kikao cha Julai 12, mwaka huu katika eneo lao maalum ya ibada za jadi lililoko
ndani ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC), kudaiwa kutoa kauli zenye
muelekeo wa kisiasa unaolenga kukinufaisha CCM dhidi ya Chadema.
Wakati huo huo
wazee hao waliwataka waandishi wa habari kuzingatia maadili ya kazi yao
kutokana na baadhi ya magazeti kuandika taarifa za uongo juu ya kikao cha mila.
waliwataka
walioandika taarifa hizo kukanusha ili kuuhabarisha umma ukweli wa
kilichozungumzwa na kuitoa doa jamii hiyo dhidi ya jamii zingine kama
ilivyoripotiwa katika vyombo hivyo.
No comments:
Post a Comment