Viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai na wale wa Manispaa ya Arvidsjaur katika kusainiana makubaliano ya ushirikiano |
Watendaji wa Manispaa ya Arvidsjaur na halmashauri ya wilaya ya Hai wakibadilishana mkataba wa ushirikiano |
Na Richard Mwangulube,Hai
Halmashauri ya wilaya ya Hai,imeingia mkataba wa miaka minne wa ushirikiano na Manispaa ya Arvidsjaur nchini Sweden unaolenga katika maeneo ya kiuchumi na kijamii
ukiwemo wa teknolojia ya kisasa ya udhibiti wa takataka kiuchumi kwa
kuziwezesha kutengezwa upya bidhaa kwa ajili ya matumizi.
Mkataba huo
ulitiwa saini wakati wa ziara ya ujumbe wa viongozi wa wilaya
ya Hai uliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya
Hiyo, Novatus Makunga hivi karibuni katika makao Makuu ya Manispaa hiyo nchini Sweden.
Wajumbe wengine
Katika ziara hiyo ya siku tano ambao ndiyo waliosaini mkataba huo ni pamoja na Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Clement Kwayu, Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri hiyo Melkizedeck Humbe pamoja na Afisa Mipango wa
Halmashauri Ester Mbatian.
Kufuatia
mkataba huo, Halmashauri ya Wilaya ya Hai itapaswa kuandaa na
kuwasilisha katika Manispaa ya Arvidsjaur miradi mbalimbali inayolenga
katika Nyanja za biashara na viwanda vidogo na vya kati.
Maeneo mengine
ya shirikiano huo ni pamoja na elimu na
utoaji wa taarifa, uboreshaji na usimamizi wa mazingira
endelevu pamoja na miradi inayolenga masuala ya ajira
kwa vijana.
Akizungumza na
waandishi wa habari mjini Hai mwishoni mwa wiki,Makunga amesema kadhalika
ushirikiano ho unalenga katika kuimarisha
shughuli mbalimbali zinazohusiana na masuala ya sekta ya utalii na utawala
bora kuanzia ngazi ya chini kabisa.
“Kwa
kushirikiana na wenzetu tunaandaa mkakati wa kuimarisha mafunzo kwa jamii
katika masuala ya uchumi na shughuli za maendeleo ya Kijamii na lengo kubwa
zaidi ni kwa kundi la vijana”. Amefafanua Makunga.
Ameeleza kupitia
Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweden[SIDA] ushirikiano huo pia utatoa
fursa kwa Manispaa ya Arvidsjaur kushirikiana na wilaya ya Hai katika ujenga
uwezo kwa halmashauri juu ya namna ya kupata taarifa mbalmbali za
maendeleo na kiuchumi kutoka maeneo ya vijijini nakuzifanyia kazi.
Amesema pia
ushirikiano huo umelenga katika kuhakikisha halmashauri ya Hai inaingia katika
mfumo wa kisasa wa namna ya kusimamia ukusanyaji wa mapato na matumizi ya
fedha za maendeleo, kuboresha mawasiliano na wadau mbalimbali ikiwemo kupitia kituo cha halmashauri hiyo cha
redio Boma FM.
Amesemasa Manispaa
hiyo ya Sweden itasaidia katika
ujenzi,uboreshaji na uendelezaji wa kituo cha mafunzo kwa ajili
ya maendeleo ya jamii katika wilayani Hai pamoja na kusaidia katika
kuboresha huduma za afya.
Masuala mengine
yatakayotekelezwa kutokana na mahusiano hayo ni pamoja na Manispaa ya Arvidsjaur kusaidia
katika teknolojia ya urudufishaji wa taka ambapo unawezesha taka ngumu na taka
maji kuweza kutumika tena.
Makunga amesema
kuwa suala la udhibiti wa takataka ni changamoto kubwa katika mji wa Hai ambao
hauna dampo huku kukabiliwa na ongezeko la kasi la watu wanaopenda kuweka makazi
ya kuishi na kuendesha shughuli zao za kazi Arusha,Moshi,Siha na Simanjiro.
“Kwa wenzetu taka ni rasilimali,
inachambuliwa kuanzia ngazi ya familia na kupelekwa eneo la kutupa taka, kwa
kupangwa kuangalia na aina, na hutumika kutengeneza bidhaa mbalimbali vikiwemo
vikombe, vijiko, sahani na umeme pamoja na mafuta ya kulainishia vyuma kutumika
upya,”amefafanua.
Ametaja mengine
ambayo yatatiliwa mkazo kutokana na ushirikiano huo ni pamoja na Manispaa
hiyo kusaidia katika kukuza uchumi na kuimarisha miundo mbinu ya kiuchumi.
Makunga ameeleza
kuwa manispaa hiyo ambayo inamiliki uwanja wa ndege wa kimataifa imeonyesha
kuvutiwa kusaidia uimarishaji wa uwanja
wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) uliopo
wilayani Hai kwa kuongeza shughuli za biashara za Anga pamoja na
kuboresha miundo mbinu katika Uwanja huo.
Ujumbe huo
uliweza kupata taarifa juu ya shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Manispaa
hiyo zikiwemo za kuchumi, kijamii pamoja na usimamizi bora wa ukusanyaji
na matumizi ya Mapato.
Kwa mujibu wa nchi
ya Sweden, Mamlaka zote za Serikali za Mitaa zinajulikana kama
Manispaa zinaongozwa kwa sheria ya bunge la nchi hiyo ambapo hivi sasa kuna
Manispaa zipatazo 260 nchini Sweden
Manispaa hizi zinawajib
wa kusimamia masuala ya elimu kuanzia ngazi ya chekechea hadi
Sekondari pamoja na kujenga na kusimamia vituo vya malezi ya wazee na
wasiojiweza.
Kadhalika manispaa
hizi zinawajibu wa kusimamia vituo vya zimamoto na uokoaji,kusimamia
ujenzi na uendeshaji wa viwanja vya ndege,kusaidia walemavu pamoja
na kuunganisha wajiri na waajiriwa
Pia Makunga
ameeleza kuwa Manispaa hizi zinajukumu la kusimamia vituo vya elimu ya
ujasirimali kwa vijana na masuala ya Utalii ambapo Sweden kila siku
hupokea watalii zaidiya 500,000 wanaotembelea vivutio mbalimbali katika
Manispaa hizo kutoka nchi za ulaya.
No comments:
Post a Comment