Wednesday, July 3, 2013

BREAKING NEWS, MAKACHERO WA POLISI WAUA JAMBAZI SUGU, LAKUTWA NA BASTOLA MOJA AINA YA BERETA

 Na Mwandishi Wetu, TANZANIASASABLOG

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas akiwaonyesha waandishi wa habari bastola ndogo aina ya Bereta iliyofutwa namba, katika eneo la Sokon I, jijini Arusha
JESHI la polisi mkoani hapa limefanikiwa kumuua jambazi sugu Lembris Taiko (35) maarufu kwa jina la “Dkt Mbushi” "ambaye alikuwa anasakwa na jeshi hilo tangu mwaka jana.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani hapa Liberatus Sabas jana alisema   Jambazi huyo aliuwawa majira ya saa 11:15 asubuhi katika mtaa wa Onjaftan  Sokoni one katika jiji la Arusha

Kwa mujibu wa Sabas  alisema polisi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa jambazi hilo na wenzake wawili   walikuwa ndani ya nyumba moja inayomilikiwa na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Swalehe ambapo wakati wa tukio hakuwepo katika nyumba hiyo.

Alidai kuwa baada ya polisi kuizingira nyumba hiyo baadhi waliingia ndani na kuwataka watu wote waliokuwa katika nyumba hiyo wajisalimishe ghafla ilifyatuliwa risasi kutoka vyumba vya ndani kupitia ukutani na kumkosakosa askari moja

Kufuatia  hali hiyo  ililazimu polisi hao kujibu mapigo kwa majibiazano kali ya risasi na kufanikiwa kuumua jambazi huyo sugu aliyekuwa akilifyatua risasi kwa kutumia bastola ambapo wenzake wawili
ambao majina yao hayakupatikana walifanikiwa kutoroka.

“Baada ya kufanikiwa kumuua waliipekuwa maiti hiyo na kubaini kuwa ni jambazi sugu ambalo lilikuwa linatafutwa na jeshi la polisi kwa muda mrefu kufuatia matukio ya mauaji, unyang’anyi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali katika jiji la Dar es Salaam, Arusha pamoja na mkoa
wa Kilimanjaro” alisema Sabas

Aliongeza kuwa walipekuwa  nyumba hiyo na kukuta Bastola moja aina ya bereta iliyofutwa namba ikiwa na risasi moja chemba,ganda moja la risasi iliyofyatuliwa na jambazi hilo risasi tatu za bunduki aina ya SHORTGUN, funguo mbalimbali 26 pamoja na moderm moja ya kampuni ya Airtel

Awali Sabas alisema kuwa marehemu huyo alikuwa anasakwa na jeshi hilo tangu Agosti 26 mwaka 2012 ambapo marehemu huyo akiwa na wenzake walipora bastola yenye namba T620-11J00491 aina ya Titas

 Alitaja tukio lingine kuwa lilitokea Agosti 29 mwaka 2012 ambapo katika tukio hilo jambazi huyo alijeruhiwa na polisi mguni akiwa katika harakati za kufanya ujambazi ambapo alifanikiwa kukimbia ambapo mwenzake aliyefahamika kwa jina Peter Toshi aliuwawa katika majibizano ya risasi na polisi na kukutwa na bastola aina ya Titas inayoaminika kuwa ndiyo iliyoporwa ikiwa imefutwa namba

Aidha Kamanda alisema kuwa jeshi la polisi linaendelea kumsaka mmiliki wa nyumba hiyo ili aweze kohojiwa juu ya mahusiano yake na jambazi aliyeuwawa pamoja na hao wawili walikiambia na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti  katika hosptali ya mkoa ya Mt Meru

No comments: